Naliona jimbo la Moshi mjini likirudi CCM

Naliona jimbo la Moshi mjini likirudi CCM

Wadau kama mtakumbuka hivi majuzi kwenye kura za maoni CCM wamempitisha kijana tajiri David Mosha (ambaye anasemekana ndio wa kwanza na wa mwisho kununua gari ghali zaidi na la kifahari hapa Tanzania-lamborghini) na CHADEMA wamempitisha aliyekuwa meya wa Moshi Mjini na diwani wa Uswazi (Pasua, Matindigani co.) masikini mwenzangu Jafary Michael.

Davis Mosha ni mtu wa level ya akina Mzee Ndesa pesa ambaye kiuhalisia pesa zake zilikuwa zinambeba sana kwenye ubunge pamoja na kuwa alikuwa hawezi kufanya chochote kutokana na umri wake.

2010 wakati Ndesa-CHADEMA akishindana na Salakana-CCM alifikia hatua kwenye kampeni anawaambia wana-Moshi kuwa ''huyu Salakana alikuwa mfanyakazi wangu kwenye sheli. leo hii hiki kiburi cha kushindana na boss wake amekitoa wapi''!

Na kwa kweli wana Moshi bila ajizi walimpa kura mzee Ndesa, na kwa sababu hiyo basi, wana-Moshi sera yao ni kuwa kiongozi masikini atahubiri umasikini na tajiri atahubiri utajiri na pengine kuwaambuza huo ukwasi.

Naziona mwaka huu kura wana Moshi zikimuangukia kijana tajiri David Mosha kwenye ubunge.

Msije kusema sijawatonya.

Nasikia Devic kakatwa.
 
Kwanza najua ujui moshi watu walioshindwa moshi ni watu wenye heshima na wanajulikana na vijana wazee na kina mama naanza na mama minde akuna asijejua uwezo wa mama minde na pesa zake na alivyokuwa msitari wa mbele kutetea akina mama lakini alishindwa Thomas ngawaiya na kujulikana kwake na pesa zake alishindwa huyo unayemsema kuwa ana pesa aligombea udiwani kiboroloni muulize alipata alichokifanya jaffari moshi akiwa meya kila mpenda maendeleo ameona Leo mpka mitaani kuna lami mji umeendelea kuwa safi mapato yameongezeka Leo tuje kumpa MTU kura kauli mbiu yake eti ataifuta chadema moshi kwani chadema ndio matatizo ya moshi
 
hv leo mengi,mzee wa azam,rostam,manji wakigombea urais watapata kwa vile ni matajiri?
 
Back
Top Bottom