Naliona Bunge kibogoyo katika awamu ya tano

Void ab initio

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
5,720
5,659
Katika awamu ya NNE tulishuhudia bunge lenye meno, likiwa limebeba utetezi wa wananchi.

Tulishuhudia mijadala mbalimbali motomoto ikihusisha kashifa mbalimbali zilizopelekea kuitikisa serikali na baadhi ya Viongozi kujiuzulu.

Lakini katika awamu hii naliona bunge likiwa gizani na wananchi kutokujua nini hasa kinaendelea na silioni bunge lenye meno tena.

Naiomba serikali inayojinasibu kutumbua majipu hadharani bila kuficha ituonyeshe na bunge hadharani bila kuficha.
 
Wanajisifu eti mambo yote hadharani lakini bunge linaendeshewa vyumbani.Kwa kweli kama hii hali itaendelea kama ilivyo,hii serikali ndo itakuwa ya kidhalimu kuliko awamu zote zilizopita.Pamoja na kupenda sifa lkn kwa hili hapana.
 
unachokikosa nini kutoka bungeni ambacho unnadhani ni special kwako? wabunge wako kazini wewe hauna kazi ya kufanya unasubiri kuona bunge mkuu?
Mkuu, heshima kwako Mimi kuwa na kazi au kutokuwa na kazi sio sababu ya kutokuonyesha bunge. Ni sababu Mfu, ingekuwa ni hivyo Channel zote zisingerusha matangazo na vipindi mbalimbali muda wa kazi.
 
Mkuu tarifa si tunazipata, tatizo mlizoea kuona vijembe na matusi kutoka kwa wabunge hao wanaoitwa watoto.tulia nchi inafuliwa karibu inatakata mkuu.
 
Jana kwenye mkutano na hao ma ccm kajinasibu kuwa atawasema waovu wanaoliibia taifa hadharani lakini yeye hataki wananchi waone serikali yake ikikosolewa hadharani.hii siasa ya hovyo kabisa.
 
unachokikosa nini kutoka bungeni ambacho unnadhani ni special kwako? wabunge wako kazini wewe hauna kazi ya kufanya unasubiri kuona bunge mkuu?
Si lazima kusema kwani hata mjinga akinyamaza huonekana ana hekima
 
Mtoa Mada ungesoma mambo uyaelerwe ndo ulete uzi sio kukurupuka
soma mipaka ya kimamlaka baina ya mihimili ya dola
 
Magufuli alishajionyesha udikteta wake alipoliamuru bunge kupeleka hela za tafrija yake hospitalini kinyume na taratibu.

Kuanzia hapo alishaweka precedent ya kuliamuru bunge.
 
unachokikosa nini kutoka bungeni ambacho unnadhani ni special kwako? wabunge wako kazini wewe hauna kazi ya kufanya unasubiri kuona bunge mkuu?
Si Magufuli kasema anataka mambo hadharani?

Sasa wanaficha nini?
 
Back
Top Bottom