Mchumia Rungu
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 1,439
- 826
Mheshiwa Sugu ni miongoni mwa wabunge waliochaguliwa kwa kishindo kiasi kwamba wananchi walifulika eneo la kuhesabia kura kulazimisha matokeo yatangazwe halaka na ikawa hivyo Sugu akawa mbunge.
Tangu aingie bungeni impact yake kwenye jimbo lake la uchaguzi haijaonekana na pengine imefika mahala baadhi ya watu wameanza kufikiria tofauti juu ya mbunge huyo na pengine kusema wazi kuwa hana anachofanya zaidi ya kubishana bungeni kwa mambo ambayo hayana msaada kwa jimbo lake la uchaguzi.
Kikubwa kinachosubiriwa Mbeya Mjini ni uchaguzi mkuu ili wakazi wa Mbeya waamue vinginevyo na uzuri wa watu wa Mbeya wanachagua mtu si chama kwa hiyo itategemea Sugu atapambana na nani toka vyama vingine ktk uchaguzi mkuu ujao.
Mkuu huna uhusiano na Kibwetere? Sijakuelewa! Ingekuwa vema ukaeleza ni impact gani ulitaka uione tokana na ubunge wa Sugu hapo Mbeya Mjini. Ukijenga tabia ya kulalamika tu bila sababu ni hatari. Kandoro amewafanyia nini ukilinganisha na Mwakipesile mliyemkataa?