Ndefu sana ebo!
Duh! kumbe umeona?watu wanachoka kusoma summarize
Mnaweza kutuwekea Article Nzima ili Tuijadili Hiyo Article? Maana msipoiweka watu wataanza Kumjadili Mtu badala ya Article yenyewe
Kama hajachakachuliwa, mbona siku hizi yuko busy kutuandikia habari za Lowasa?? hata gazeti la uhuru halimpi coverage yoyote Lowasa lakini Kibanda siku hizi imekuwa bandika bandua Lowasa hakosi kwenye front page.
Ni dhahiri kwamba kibanda ameshachakachuliwa, na siku zake zinahesabika, yuko njiani kuelekea kwa bosi wake muya fisadi papa
si umeona kuna mhariri mmoja tayari ameshachoropoka na kuingia zizini?
Nashukuru kwa bwana Kibanda,kujitokeza na kutoa msimamo wake,ila hata mimi ckubaliani nae kwa lugha aliyoitumia,ni lugha kali na ya kufedhesha hasa kwa mtu mzima kama 6(acha suala la vyeo),ungeweza tumia lugha nzuri na ya staha,yenye hoja na ujumbe ungefika tena vizuri,kumbuka 6,ni mume wa m2 na pia ana watoto,.chondechonde waandishi kalamu zenu ni kali kuliko risasi,so msitumie vibaya hizo kurasa zenu,na wala ninyi sio watu special sana,ni mgawanyiko wa kikazi,naomba kuwasilisha
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, anafanya kazi part-time kwenye magazine inayomilikiwa na Edward Lowassa inaitwa UMOJA. Pia Kibanda amekuwa anatoa habari za kumbeba Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye Tanzania Daima mara nyingi. Kwa kupokea maagizo na malipo kutoka kwa Lowassa na Rostam Aziz, Kibanda pia amekuwa akiandika habari na makala nyingi za kuwakashifu Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli.
Tanzania Daima ni moja ya magazeti yanayotumiwa na fisadi Rostam Aziz kutetea ufisadi mbalimbali, ikiwemo malipo kwa Dowans kwa nguvu zote. Wanaitumia Tanzania Daima kwa kuwa gazeti linaaminika kuwa ni huru na ni rahisi ku-brain wash watu kuliko kutumia Mtanzania/Rai ambayo Watanzania hawayasomi tena sasa baada ya kugundua kuwa yanamilikiwa na Rostam.
Cha kushangaza ni kuwa mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaachia tu gazeti lake litumiwe na mafisadi kupitia kwa Kibanda kuangamiza nchi.
Mbona hatuwaulizi viongozi wa dini ambao siku zote wanamualika Lowassa kwenye shughuli zao? Nao wamechakachuliwa? Mbona hatushangai iweje CCM impitishe kuwa mgombea ubunge Monduli, nako huko chama chake kimechakachuliwa? Kwa nini akiandikwa gazetini iwe nongwa? Msimamo wangu ni thabiti LOwassa akizungumza mambo ya msingi habari zake zitaandikwa Tanzania Daima, akifanya mambo yasiyostahili ataandikwa pia kwa uzito ule ule. Hakuna aliye salama Tanzania Daima hususan kama ni kiongozi wa kitaifa.
Kesho Jumatano katika Tanzania Daima nimeandika sehemu ya pili ya makala hiyo. Kwanza nimemuomba radhi Sitta na Watanzania kwa lugha kali niliyotumia dhidi yake na dhidi ya Watanzania wenzangu. Naamini katika kukosoana. Nimekiri mapungufu katika maandishi yangu. Hata hivyo nimesisitiza msimamo wangu kuhusu Sitta uko pale pale. Nimejaribu kutumia lugha ya staha kueleza kile ninachoamini kuhusu sakata la Dowans na vitanzi tulivyojifunga
tutahakikishaje km mikono yako ni safi kwani kuna cku ulijadiliwa juu ya suala km hili lkn haubadiliki
Mtumikie kafiri upate mradi wako. We know your type mate.
Waandishi kama wewe ndio mmekuwa makuwadi wa kina RA, EL et al. Tanzania ya leo sio ile ya jana ya kulala lala ... ... No retreat no surrender haiingii akilini kuona vimburu kama wewe mnanakuja hapa kutaka ku-justfy utumbo ambao unaandika.
Kesho Jumatano katika Tanzania Daima nimeandika sehemu ya pili ya makala hiyo. Kwanza nimemuomba radhi Sitta na Watanzania kwa lugha kali niliyotumia dhidi yake na dhidi ya Watanzania wenzangu. Naamini katika kukosoana. Nimekiri mapungufu katika maandishi yangu. Hata hivyo nimesisitiza msimamo wangu kuhusu Sitta uko pale pale. Nimejaribu kutumia lugha ya staha kueleza kile ninachoamini kuhusu sakata la Dowans na vitanzi tulivyojifunga
For sure nimekuwa ni mpenzi wa makala za Kibanda lakini tangu nimesoma hiyo makala nimemuweka kundi chafu ka RA.Ukitaka kumjua Kibanda vizuri soma toleo la kwanza na la pili la Magazine ya Umoja utagundua jinsi anavyopamba rushwa, ufisadi na kuponda wapambanaji dhidi ya ufisadi.Ni ukweli ulio wazi kwamba,nimeweka msimamo wa kutosoma makala za huyu bwana tena.Ni uchafu mtupu na amenunuliwa.Bila shaka ana gawio kubwa kwenye dili la Dowans
Naamini katika nguvu ya hoja siyo hoja za nguvu kama zako. Umeandika jambo gani la maana katika jamvi hili. Umechoka kufikiri wewe, huu si uwanja wako fungua majarida na magazeti ya udaku usome.