Naliona anguko la Kibanda

Kibanda anatumia staili walootumia akina Salva wakati ule wa Rai na Mtanzania kuwamaliza mapema wapinzani wa mtu wake (Prof Mwandosya) katika kinyang'anyiro cha Urais 2015. Anajua Sitta ana nguvu na ushawishi mkubwa hata kama yeye mwenyewe hatagombea. Maandishi ya Kibanda hata kwenye Tz Daima ya leo yana mwelekeo huo.
Akina Salva walipogundua FTS, SAS ni tishio kwa Urais wa JK mwaka 2005 waliandika hasa. YAliyobaki sasa ni historia.
 
.
Kwangu mimi Rostam, Sitta, Lowassa, Chenge, Mwakyembe na wengine wote ni vyanzo muhimu vya habari na kwa Tanzania Daima wana nafasi sawa kihabari. Msimamo wangu huo uko bayana na kimsingi hatufungamani na upande wowote.

Msimamo makini huu.....

Aaah wait!! aaggghh....mbona umeshachukua upande tena??

.

Nilikataa tangu mapema kujiingiza katika vita ya ufisadi inayopiganwa na akina Sitta na akina Mwakyembe kwa sababu nimejiridhidhs kwamba ni vita ya kitapeli.
 
mbona jukwaa lilishapoteza muelekeo kitambo sana-wanajamii wamegawanywa na posts za kijinga zinazoshabikiwa na mods-posts zenye kuwagawa wanajamii kwa misingi ya imani, hapa mara nying Posts zinazoshabikiwa sizo za kiuchunguzi na wala hazina masilahi ya Taifa lakini zenye maana kwa jamii watu huponda na kutusi na mods hukaa kimya-mara kadhaa binafsi nimekuwa nikijitahidi kuzungumzia masuala haya bila mafanikio. mara nyingi watu imefikia wakitukanana hapa jamvini kwasababu ya Posts za kidini na kujikuta nguvu yao ikigawanyika wakati wa kujadili issues zenye masilahi ya Taifa. mfano nimebaini kuwa kuna watu wanadhani ukiwa mwana chadema lazima uwe MKIRISTU na vinginevo sio sawa, ni kwa misingi hiyo hata mimi na wanaonizunguka imefika mahali tumelazimika kuondoka chadema kwasababu tunaona kama inawezekana kuna hidden agenda kati ya chadema vs UKIRISTU-nilipenda sana Falsafa za Chama lakin sasa nalazimika kuamini kauli za Mh Zitto-ndugu zangu tubadilike. wanaharakati wengi watadhaifishwa na contributions wa wajingawajinga hapa janvini
 
KIBANDA KWA HILI TUKO PAMOJA ! sema tu, nimekuelewa na ninatayarisha nakala ya kutetea na kuuelewesha umma unamaanisha nini! just simple logic is needed!


Kama ni simple logic tu ndio inahitajika kwa nini usitueleweshe hapahapa, matayarisho ya nini?
 


Kabla hujashangaa, jiulize kama Freeman Mbowe anaweza kuwa mfuasi mzuri wa Dk. Slaa!
Ni kwamba Slaa yuko peke yake, akizungukwa na wasanii kama Mbowe na Zitto Kabwe. Mbowe hawezi kuwa safi, hata kwa OMO. He is a business man, and that says it!
CHADEMA wanatakiwa waanzishwe gazeti lao, TV yao na Redio yao. Tanzania Daima is hijacked.
You can't trust Mbowe, I am sorry.......
 


Nakuunga Mkono, sijawahi kumsikia Mbowe akitoa tamko lolote kupinga utapeli wa richmond na dowans. Kama kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani alitakiwa kuwa mstali wa mbele kutetea pesa za walipa kodi. Binafsi huwa sina imani na Mbowe, hasa ninaposikia kuwa ni rafiki mkubwa wa EL.
 

Si lazima kila aliyechukiwa na mwalimu ni dhalimu. Pia with time anaweza akawa amejifunza kitu na akabadilika. At the end of the day, tunaangalia leo anaongea nini na kama kina maslahi kwetu. Nasema Samwel Sitta na Mwakyembe wanaongea lile linalowaumiza zaidi wananchi. Mpaka hapo Sitta ni shujaa.........usitupotoshe.
Ni mtizamo wangu, na si lazima uwe sawa na wa Mwalimu!
 

Only if you mean it.....maana unaweza kuwa thabiti katika mrengo ovu......
 
Je,ndugu wadau, hamuoni kwamba inawezekana Kibanda anatumiwa na Mbowe kuzidi kumpa hasira Sitta & Co. dhidi ya Chama na serikali??
 
Kibanda ni mtu makini lakini kuendelea kuwakumbatia watu ambao jamii inawaona ni wachafu na wanakashfa tele za kifisadi kwa kisingizio cha kumpa kila mtu nafasi hilo haliwezi kuwa na nafasi sawa kwa kila fikra. Mimi ni msomaji na huwa sikosi makala ya tanzania daima.

Unahitaji kubadili mwelekeo wa kuwapa nafasi watuhumiwa wa ufisadi kwenye tanzania daima maana wengi wanaliona kuwa ni gazeti lisilo kumbatia uchafu, huhitaji kuwa na lundo la uchafu kama una taka mazingira safi. Vinginevyo uamue kuchafuka na kuendelea kuruhusu watu wachafu ili wote mfanane kwa uchafu.

M. M.
 
Wanajamvi:
Hii stori katika Tanzania Daima imekaa vipi? Kwa maoni yangu naona ni ya uzushi tu yenye lengo fulani hasa katika kuonyesha kwamba nyaraka zozote zilizotolewa au zitakazotolewa kuhusu ufisadi na hujuma kubwa RA aliyowafanyia wananchi wa Tanzania ni za kughushi tu. Ni katika harakati za kujihami kabla (pre-emption) kwani kwa sasa hakika maji yamemfika shingoni.


Huyu RA ni mtu hatari kweli kweli, kwani kutokana na nguvu zake za kipesa anaweza kushawishi magazeti fulani yakaandika kitu chochote anachokitaka. RA ana magazeti yake lakini anajua fika kwamba hayana kabisa credibility mbele ya umma kwa hivyo analitumia hilo ambalo mhariri wake mkuu ni swahiba wake -- Absolmi Kibanda.

Kibanda anaonekana kuwa mmoja wao -- kati ya wale wanaoshiriki katika kudhoofisha jitihada za kulikomboa taifa hili kutoka kwa mafisadi kwa sababu tu ya pesa kidogo.

Nashangaa kwa nini Mbowe, ambaye ni mmiliki wa gazeti hilo asimtimue huyu – kwani jinsi siku hadi siku zinavyokwenda naye (Mbowe) binafsi atakuwa anatiliwa mashaka katika udhati wake wa vita dhidi ya ufisadi ambayo chama chake ndicho kinashika bendera. Isitoshe gazeti likizidi kuandika habari positive za RA huenda likapoteza usomaji, kitu ambacho kimekuwa kinajijengea vizuri.


**************

Msaidizi wa Rostam atishiwa maisha

* Atakiwa kutoa nyaraka zenye saini ya bosi wake
* Rostam ataharuki, asema sasa tumefika pabaya


na Mwandishi wetu


MSAIDIZI wa Rostam Aziz ambaye ni Mbunge wa Igunga, Tabu Omar, ametishiwa maisha na mtu aliyefika ofisini kwake akimtaka ampe nyaraka muhimu yoyote yenye saini ya bosi wake huyo.

Vyanzo vya habari toka katika ofisi ya msaidizi wake huyo vililidokeza gazeti hili kuwa Tabu alikumbwa na mkasa huo wakati akitoka ofisini kwake majira ya jioni mwanzoni mwa wiki hii.

Gazeti hili lilipomtafuta Tabu kufahamu kuhusu tukio hilo alikiri na kusema kuwa mtu mmoja ambaye hakumfahamu alifika katika ofisi hizo siku ya Jumanne wiki hii na akamvizia wakati akitoka kwenda nyumbani.

Alisema wakati anatoka kazini, ilikuwa ni majira ya saa 11 jioni na alipofika katika geti la ofisi hizo alikutana na kijana huyo ambaye alimbembeleza ampatie nyaraka yenye sahihi ya Rostam akimuahidi kumpa shilingi milioni tano endapo atafanikisha adhma yake hiyo.

“Aliponiambia hivyo…nilikataa nikamwambia siwezi kufanya hivyo, lakini nilipomjibu hivyo akaniambia ikifika siku ya Alhamisi (juzi) niwe natembea na nyaraka hizo na nisipofanya hivyo ataniiua,” alisema Tabu.

Tabu alisema kuwa alishtushwa na kauli ya mtu huyo ambaye hajapata kukutana naye kabla na hivyo siku ya pili yake alilazimika kwenda kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Shtakishari kilichoko eneo la Tazara.

Alisema alipofika hapo alifungua jarada katika kituo hicho na kupewa RB namba yenye namba STK/RB/2212/2011 na kwamba polisi wamemtaarifu kuwa wanaendelea na uchunguzi wao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, Rostam alisema hizo ni dalili za mwanzo kwamba kama taifa tumefika mahali pabaya.

“Chuki na uhasama huu wa siasa unaopandikizwa kwa kutumia vyombo vya habari, ndio umetukifisha hapa kwa watu baada ya kukosa uthibitisho wa uongo wao sasa wanatafuta saini za watu ili wakaghushi nyaraka na kuendeleza fitina,” alisema Rostam.

Tukio hilo la kutishiwa maisha kwa msaidizi wa Rostam limetokea wakati jina la mwanasiasa huyo likitajwa kwa namna tofauti kwenye sakata la kampuni za Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania Ltd ambazo hivi karibuni zilishinda kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) dhidi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

ICC katika hukumu yake ambayo imesababisha mvutano mkubwa katika jamii, imeiamuru TANESCO kuilipa Dowans fidia ya dola za Marekani milioni 64 (sawa na sh bilioni 94) kwa kosa la kukiuka mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura.

Chanzo: Tanzania Daima
 
RA mwacheni kwanza. Tutamnyongea katika uwanja wetu wa Tahrir -- yaani Jangwani -- siku itakapowadia. Lakini hata hivyo nasikia serikali inataka kuanza kugawa viwanja pale jangwani kwa hofu ya kutokea mikusanyiko ya kuiondoa siku itakapofika!
 
Kwani hilo gazeti linamilikiwa na nani? je mmiliki anahusikaje na habari za kumsafisha RA? Hivi mnataka watu waamini kuwa mmiliki hahusiki na kama hahusiki na hizo habari unazodai kuwa za kumsafisha RA amechukua hatua gani? Tusije tukawa tunajidanganya kumbe hata tunaodhani hawapo kumbe wamo mmesahau ya mchungaji Mtikila kupewa pesa na RA? Hivi kweli kuna mtu aliweza kulifikia suala kama lile lingewezekana? Mimi nisingefikiria kuwa linawezekana sijui wewe mwenzangu........................
 
hata kwenye mtanzania, gazeti la rostam, imeandikwa habari hii. Nakubaliana na wewe mkuu counterpunch kwani magazeti mawili tu ndio yameandika habari hii, hili la kibanda na la rostam mwenyewe.
kwa umaarufu wa Rostam habari hii ingekuwa kweli magazeti mengi yangeandika.
Rostam can do anything possible and imposible kujisafisha.
 
Waache waendelee lakini tujihadhari kwani wagombanapo fahari wawili...
 
Rostam atafanya kila juhudi kutaka kujisafisha, simuani katika hii story. Muongo kama Pinda na fisadi Kikwete:sick:
 
Hii story haina mantiki hasa kweli kama mwandishi angekuwa mtu makini, maswali yafuatayo au mambo yafuatayo ni muhmi kujiuliza na kuyafahamu; Iwapo watu wana uwezo wa kufoji sahihi hata za viongozi wakubwa, mihuri na nyaraka mbalimbali hadi kukwapua kwenye mabenki na sehemu nyingine nyeti ( kama ilivyowahi kuripotiwa sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi) bila kutumia nguvu ya aina yoyote, iweje huyu atumie nguvu kama sio Uongo???

Pili, kulikuwa na umuhimu gani hasa wa kumfuata TABU badala ya kutumia mbinu kibao ambazo zipo? yaani huyo anaehitaji hiyo sahihi alikua mjinga kiasi gani hadi amfuate Katibu wa RA huku akijua fika uhusiano wa karibu kati ya Tabu na RA ( kama ilivyowahi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari nchini).

Tatu, je ni vigumu sana kuipata sahihi ya RA hadi aende ofisini kwake? yaani hakuna nyaraka nyingine zozote ambazo RA ameweka sahhihi ni hadi ofisini kwake?

Nne, kwa nini amsubiri wakati anatoka ofisini huku akijua fika kuwa hawezi kuwa anatembea na document zenye sahihi, hapa huyu mtuhumiwa ambaye mimi naamini hayupo, ni mjinga kiasi gani amsubiri Tabu atoke ofisini ndio amfuate??

Tano, angewezaje (Mtuhumiwa hewa) kutoa pesa kidogo hivyo (5M) hali akijua nafasi ya Tabu na kipato chake, kweli Tabu angekuwa radhi kutoa sahihi ya Bosi wake kwa Million tano tu??? labda kama hawafahamu vizuri.

Mwisho, ni vyema unapotunga stori, jiulize kwanza baadhi ya maswali mwenyewe, yaani, jiweke kwenye position ya msomaji na sio kuvutiwa na hisia zako tu. Naombeni ushauri kwa haya machache. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…