Naliona anguko la CCM mwaka 2025

Naliona anguko la CCM mwaka 2025

CCM ni limbuyu likubwa hamliwezi jameni, msubiri labda mwaka 3040 litaunguka lenyewe likiwa limetimiza life span yake.
 
Tulipokua wanasiasa huko udogoni tuliaminishwa kua wakiweka hivi tunapenya hiyo ni maana ya kutumiaa mianya
Hivyo mianya ikitumika vizuri tunaweza kuona kitu cha tofauti
 
Nikiangalia mwenendo wa nchi na siasa za Tanzania naliona ANGUKO LA CCM 2025 kama wapinzani wakiwa na mkakati kabambe

Nini maoni yako?


#mtotowaafrika
#kazindokazi
Chadema ndio kuna anguko kubwa bado wanasiasa za kishamba sana ,hawataki kubadilika kabisq japo ccm hakuna watu sahihi lkn hapana kuwapa chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiangalia mwenendo wa nchi na siasa za Tanzania naliona ANGUKO LA CCM 2025 kama wapinzani wakiwa na mkakati kabambe

Nini maoni yako?


#mtotowaafrika
#kazindokazi
Haliwezi kutokea anguko kama la 2020 mumshukuru tu shetani kwani ali-play part yake vizuri.
 
Ujinga wa nchi hii ni ujinga waliopandikizwa na wakauamini, CCM itatawala milele kwa ujinga wa kuzira kupiga kura,
Ujinga wa kujitenga na mfumo WA siasa eti haikuhusu ni tope kichwani
Ujinga wa Haku a Chama kilicho na Nia ya madaraka
Ujinga wa nikiwachagua wanaenda kushibisha matumbo yao
Sasa unataka Nani akufanyie kazi wewe kama mtoto mdogo
 
Shida yetu bongo ni moja tu..hakuna mpinzani wa kweli..wote wachumia tumbo tu,mm nikaonaga nikae pembeni kushabikia siasa
Kwani mpinzani wa kweli anakuaje??
 
Sijui Kwanini mnakuwa na mtazamo hasi juu ya mabadiliko.

Ikitokea hivyo kitakuja kingine bora zaidi tatizo litakuwa wapi ?

Watanzania tunawazaje juu ya mambo ?

Je ni maslahi ya watanzania kwanza au chama fulani cha siasa kwanza?

Chama ni means/medium tu lakini muhimu ni maslahi ya watanzania,

Yaani kuna ujinga fulani umo vichwani mwa wengi kuhusu kuzani Eti chama chama.

Lazima tuanze kwa kubadili namna yetu ya kufikiri juu ya mambo ndipo tutapiga hatua kwenda mbele ya maendeleo,

Tukiendelea kuwaza vile vile tangu Uhuru huku tukitarajia mabadiliko yenye tija katika utendaji itakuwa Sawa na uendawazimu (according to studies).
 
Doing the same thing by using the same methods by expecting better results ni sawa na uwendawazimu

We have to start to change our mindsets
 
Upinzani goli lipo wazi ni wao tu wabutue au wafunge goli
 
Nikiangalia mwenendo wa nchi na siasa za Tanzania naliona ANGUKO LA CCM 2025 kama wapinzani wakiwa na mkakati kabambe

Nini maoni yako?


#mtotowaafrika
#kazindokazi
Anguko la mgombea wa KIJANI nimeliona,

Bt anguko la CCM!!! Ntasema baadae.
 
Nikiangalia mwenendo wa nchi na siasa za Tanzania naliona ANGUKO LA CCM 2025 kama wapinzani wakiwa na mkakati kabambe

Nini maoni yako?


#mtotowaafrika
#kazindokazi
Iangushwe CCM ? Na nani na hawa watoto wa mjini vyama vya upinzani ambao vijijini hawako ambako asilimia 80 ya watanzania ndio wanajoishi na matawi ya CCM yako vijiji vyote

Upinzani Tanzania bado sana tu
 
CCM ilianguka rasmi 2015 ila haikufa bali ikabaki chumba cha mahututi kwa msaada wa dola
Uongo

Chadema haikuwa na mizizi vijijini kwenye wananchi walio wengi asilimia 80 ya watanzania

Ushabiko wa chadema ulikuwa zaidi mijini tu na majiji na miji midogo ya njiani sio vijijini
2025 Chadema itapigwa tena na kitu kizito

Hawawekezi vijijini wanahsngaika tu mijini ambayo wapiga kura ni asilimia 20 tu ya kura zote

Vyama vya upinzani ni vyama vya wahuni wa mijini
 
Wapinzani wa Tanzania na vyama vyao wote ni wachumia tumbo tu

Na ndio maana hata hao wapinzani wenyewe hawawezi kukaa meza Moja wakapanga jambo la maana

Vile viti vya ubunge na udiwani walivyokuwa wanavipata sio kama labda wapinzani walikuwa vizuri la hasha ila wananchi walikuwa na hasira na CCM
 
hili likitokea litapendeza zaidi maana CCM wametugeuza watanzania mazombi wanafanya siasa zao uchwara matokeo yake athari zinakuja kwa wananchi,kila kitu wanafanya siasa wananchi tangu uhuru mpaka leo wanahangaika na vitu basic kabisa kwa binadamu kama maji,umeme,barabara nzuri halafu kila baada ya miaka 5 tunachagua viongozi hakuna mabadiliko wakimaliza wanaingia wengine wanaacha mambo yaleyale sijui shida ni nini.
 
Back
Top Bottom