Nakuuliza CHADEMA

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,657
1,992
Kweli Chadema mmefanikiwa kufanya mkutano mkuu pamoja na uchaguzi kwa mafanikio, kwa hilo nakupa hongera
je chadema mmejua au mmefanya utafiti nakujua ni watu wangapi walifatilia mkutano wenu?

Je mnajua nguvu ya vyombo vya habari katika kupeleka habari, kuhamasisha na kuhabarisha?

Kama kweli mnajua:

Kwanini mlishindwa kuonyesha mkutano wenu mbashara ili watu wafwatilie, wahamasike na wajue kinachoendelea?
najua mtakuja najibu jepesi kuwa vyombo vya habari vya hapa vyote viliogopa lkn kweli mlishindwa kujiongeza zaidi yangu hapo?

Mimi sitaki kuamini kwamba kulikuwa hakuna njia nyingine mbadala walau kufanya mkutano wenu uonekane live.
Nasema hivi sababu huko tuendako kama chadema itashindwa kupata vyombo vya habari ambavyo vitakuwa vinahabarisha umma nn kinacho fanyika, usambazaji wa sera za Chama, uhamasishaji wa wananchi basi Chadema ijiandae kwa anguko kubwa zaidi sababu kwa dunia ya leo bila vyombo vya habari kila ukifanyacho ni kazi bite.

Ushauri wangu wa bure kwenu:

Kuanzia sasa anzeni kuweka mahusiano na mikatabana Television za nchi jirani hasa Kenya.
Nunueni vipindi kule, walipeni waowafanye kazi hiyo kwani Tv za ndani zimeshindwa kufanya hivyo kwa hofu kuu ya kumuudhi bwana mkubwa na kufungiwa.

Kwa bahati nzuri Tv za nje zinapatikana katika ving'amuzi vyetu kama Azam, DStv na Startimes. Nunueni vipindi kwa mfano, muwe na CHADEMA Tv ambavyo itaonyesha kazi mbalimbali za Chama. Sera zake ni hotuba mbalimbali za viongozi wa chama.

Kuweni wabunifu la sivyo mtapotea kabisa huyu mpenda malaika wa kufunga mtandao ya jamii amedhamiria kuwafuta kabisa kwa hiyo iwe vita ya jasho na damu muweze kusimama imara.

Msitegemee Sana hii mitandao kwani waliyonayo ni wachache Sana Bali watanzania wengi wanategemea kupata habari kiurahisi kupitia Tv, redio na magazeti.

Kazi yenu iwe ni kutangazia sisi wananchi kuwa vipindi vyetu viko katika Tv gani na lini na nina hakika watu watafuatilia tu kujua nini kinachoendelea.

Mwisho niseme hongereni sana wote mliochaguliwa kwa kuwa mpinzani ni lazima uwe na roho ngumu kama ya mwenda wazimu hivi.

MWENYE MASIKIO ASIKIE HILI
 
Siasa ni imani kama ilivyo imani ya Dini, kuna watu ambao hawakujaaliwa kujenga misikiti wala kuwa na kanisa ila bado ni waumini wazuri tu..kwa nguvu kubwa inayotumika kufifisha upinzani unadhani hizo online TV watazisajilia nje ya nchi?
 
Tuna Smart phones na mkutano uliangaliwa tija vijijini.
kweli wewe inayo lkn kuna watanzania wangapi ambao hawana ambao ndio wapiga kura wazuri?
Kumbuka asilimia karibia 80 ya watanzania wanaishi vijijini
 
Hapo kwa Kenya unawaingiza chaka, Wakenya hawawezi kuangalia wala kufwatilia uchaguzi wa chadema, hivyo hizo TV zitakula hasara tu na chadema kupoteza fedha, hata Bongo wengi hawana mpango na chadema. Azam, star hawawezi rusha chadema.
 
Hapo kwa Kenya unawaingiza chaka, Wakenya hawawezi kuangalia wala kufwatilia uchaguzi wa chadema, hivyo hizo TV zitakula hasara tu na chadema kupoteza fedha, hata Bongo wengi hawana mpango na chadema. Azam, star hawawezi rusha chadema.
Nilicho sema ni hivi hizi TV za Kenya zipo ktk ving'amuzi vyetu kwa hiyo zinapatikana hata hapa kwetu Tanzania na zinaonekana Hivyo wakilipia sisi tutaangalia
 
Back
Top Bottom