Nakusudia kumshtaki baba yangu

ugomvi baina ya wanaume chanzo ni uwa ni K au madaraka (power) tu.
 
Mmm mkuu nimekuPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti nipe mchango wa ndoa, mzazi hata hajui mwanae yuko wapi[emoji134]

Inatia hasira balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebwanae eeh!

Jike shupa limeshafanya yake[emoji134]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii story ilishawahi kuwekwa humu jamvini naona umethrowback kiaina.
 
Naomba mtag mwenye Uzi mkuu, niusome pia huo uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikusomesha? una maarifa siyo? wewe ndiyo mjinga? kubali nikwambie kitu!
 
Umekaa na Baba yako miaka 20 Unashindwa kumuelewa tabia yake? tena afadhali huyo anakupigia na simu mnaongea! wengine anajiona Matawi, Haongei na Failure wa Shule, tena maskini, haya kwenye Misiba wapwa zake ndiyo wasemaji wakuu wenye akili. nyinyi mlio wake ni wasugua Masufuria ya Msibani na kutafuta kuni. kifupi nyumbani kwenu ni km Matahaira msio kuwa na Dira.

Km haitoshi unakuja likizo toka Shule Kabla ya kukaa, anakwambia ''Mbona unakuja bila taarifa? sababu tu umekuta ana gonga Menu nene na Kihawala chake Nyumbani kwenu! Ukipata Shule kali ambayo utapasua kuliko yeye, anakwambia Masomo hayo Magumu, ntapoteza hela zangu bure! anakutafutia vi-course vya hovyo!

Haya yamepita hayo, ameumwa sasa!!! mnamuuguza na kumpa hela, bado ana Mind na kurudi kwa michepuko na kuipa hela zako, hafurahi kuwa na wewe km anavopenda vitoto vya hawala haramu! mbele yenu, tena kwako mpaka mkeo anashangaa, anauliza mbona baba yuko hivi? huyo huyo Mzee kachoka anakwambia Mshauri mama yako nioe mwanamke mwingine! si niwazi hakutaki?

Unapomsaidia ki hivyo, ndiyo anaona wewe Fara kabisa hujitambui ulisharogwa na Dada zake akili imepotea ndo maana unafanya mambo ya *******. anakuona km takataka! huyo ungembana kisaikolojia mpaka ajambe cheche! hampigani wala kumpeleka Mahakamani sijui Polisi, Mfilisi kwa akili tu. halafu mtulize eneo moja ale ugali dagaa tu! hawapendagi Nyama hao! Usilogwe uendeleze miradi yake bali hamisha mtaji wake kijanja.
 
Mimi Sina moyo wa uvumilivu mzee Kama huyo naachana nae kabisa na ndio sikubahatika kupata wazazi Kama hao.

Mzazi akiwa MJINGA familia nzima inakuwa hatarini kimuelekeo wa maisha kwenye maisha ni bora umtose MJINGA uokoe maisha ya wengi hakuna laana hapo kuliko kupoteza muelelekeo wa familia nzima kwa ajili yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba Mkuu kumbuka na Mazuri pia alokufanyia awali, wkt utotoni mnacheza karata!! halafu ujue wanaume wanarogwa mno, na michepuko, labda umsaidie umkomboe kutoka kwenye umateka wa mchepuko! hasa km baba akiwa na kijana Afya , Handsome, na hela fulani hivi wee!!!!

si unaona vidume maskini walivo salama, hakuna kushobokewa na wanawake michepuko? ale nini mtu ana baiskeli tu.... familia zao?

Kumbuka na wewe ni mwanaume unaelekea huko! hapo ujue kuna baadhi ya Mashangazi zako wanamuonea wivu Mama yako! watamshauri babako aoe ttu! ili nyie na mama yenu mkose maisha. mtaabike. ...mchawi ndugu paka katumwa!

kuwakomesha tafuta Mpunga hasa uwe hata mara kumi yake ndo dawa!
 
Eti nipe mchango wa ndoa, mzazi hata hajui mwanae yuko wapi[emoji134]

Inatia hasira balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilimjibu kuwa unajua nilipo?
Unajua nakula nini?
Alikaa kimya na alibadilisha maongezi na kusema kuwa alikuwa ananishirikisha nisije kusema kuwa sikutaarifiwa kuhusu ndoa na Michango..... Hii dunia acheni tu! I hope tutafika mwisho.
 
Pole sana mkuu. Ukiliendea vibaya hilo suala,mzee atakuachia na laana kabisa,anaharibu kabisa uzao wako. Tatizo wazazi wa kukuzaa wana nguvu sana kiroho,sijui kwa nini Mungu aliamua hivyo. Akikupiga laana yoyote hata kama yeye ndiye mkosaji inakuandama

Tumia hekima sana sana mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna utata mkubwa sana hapo ndugu,ni kweli una uchungu na hasara lakini pia jambo la kumshitaki litabeba sula mbaya kubwa sana kwenye ukoo,wapo watakao kuelewa ambao watakua ni wachache sana na watakao kulaumu watakua wengi,na yamkini usipate chochote juu ya mashitaka yako,na ukipata yamkini mzee na ujinga wake akafungwa na wewe kuishia kunyooshewa kidole kila unapopita na watu wasiojua uchungu wako wewe kua huyo jamaa kamfunga baba yake mzazi kwa sababu ya peaa

Cha kufanya anza kuendesha mambo yako huku ukimsaidia mama tu,mzee muishie salamu na umuache na shida zake,utazua mengi sana japo wewe utaona kwamba bora lawama kuliko hasara lakini hilo litakutafuna kwa miaka mingi sana ktk historia ya maisha yako,na huko mbele ndugu na jamaa wote hawatajua uchungu wako wewe juu ya mzazi wako zaidi ya wao kukupa maneno ya fedheha kua uliwahi kumfunga baba yako kwa sababu ya pesa

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Pole Sana mkuu..
Najua unaumia Sana na unapata uchungu,hata Mimi hiyo Hali nimeipitia.
Kikubwa kaa,tulia,kabla hujafanya maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mchangia mada sio muhusika mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…