Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

Manzile

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
717
Reaction score
1,933
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama asingekuwa na maisha ya dhiki hakika asingeuza hilo eneo. Ila kwa vile ana maisha ya dhiki ndiyo maana kauza. Ingawa umejaribu kumsifia hapo juu. lakini ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa your Dad is deadly broke.

BTW, mfungulie kesi ya madai ambapo utamuunganisha yeye na huyo aliyenunua hilo eneo.

Pia, unaweza kwenda kutoa taarifa polisi kuhusu hilo kosa alilotenda ili afunguliwe kesi ya jinai.
 
Inaumiza,lkn nakushauri muheshimu baba yako na usiendelee kumdai.Kama uliweza kuzipata hizo mali,utapata tena. Mwenyezi alituamuru tuwashimu,kumbuka pia ww n mwanaume,ipo siku utafanya makosa kama yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndgu siwezi kuwa mpumbavu namna hii, katelekeza familia miaka zaidi ya 6 nahangaika kusomesha watoto wake bado kuna mengi nimesahe yeye ameenda kuchukua mwanamke ana watoto wakubwa wa wanaume wenzake kamjengea nyumba nzuri kwa jasho langu na miradi huku wanae, nimuache Mali zangu zifaidishe ukoo mwingine huku wadogo zangu wanateseka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kwa uchungu sana, Hawa wazee kuna wengine wanafeli sana...

Naomba nikushauri kitu hata mkienda mahakaman nna uhakika hakuna kitu ambacho utarudishiwa kwa namna yoyote ile zaidi ya kupoteza muda
ila kama unao muda wa kufatilia kesi za madai fanya.

Umesema wadogo zako wengine wapo chuo anza kuwaingiza kwenye miradi yako kama ambavyo wajomba zako walikufunza wewe.

Anzisha mradi ambao utakua unalisha familia na kusomesha ambao bado wanahitaji kusomeshwa inaweza isiwe ule mkoa ambako mzee wako yupo au kama huko bas shirikiana na wadogo zako ambao wapo pale bila mzee wako kufaham chochote.

Ushajishusha kwa mzee wako imetosha chakufanya sasa badilisha namna ya kusaidia hao waliobakia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama asingekuwa na maisha ya dhiki hakika asingeuza hilo eneo. Ila kwa vile ana maisha ya dhiki ndiyo maana kauza. Ingawa umejaribu kumsifia hapo juu. lakini ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa your Dad is deadly broke.

BTW, mfungulie kesi ya madai ambapo utamuunganisha yeye na huyo aliyenunua hilo eneo.

Pia, unaweza kwenda kutoa taarifa polisi kuhusu hilo kosa alilotenda ili afunguliwe kesi ya jinai.
Mkuu Hana maisha ya dhiki kivile sema huyo kimada wake anampelekesha hata akiwa Hana pesa atatafuta means yoyote aipate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jambo kama hilo ndugu kheri nusu Shari kuliko Shari kamili. Ukimuacha atakuchukulia poa sana lazma uoneshe msimamo wako apo lasivyo mtajikuta wote mnarudi chini tena chini haswaa.
 
Hapana sitaki kumroga nataka Mali zangu azirudishe mahakamani yeye aendelee na maisha yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu, huyu mzee alikutunza vyema wakati hajaanza kufanya huo unaoita upumbavu au alikuwa hivyo tangu zamani?

Je ana mgogoro na mkewe yaani mama yako.?

Umewahi kufuatilia japo kujua chanzo cha yeye kurudi nyuma kiuchumi ni nini.?
 
Mkuu siku zote hasira huenda isitende haki. Kuna jambo la kufanya, najua nia yako ni kumkomoa ila hautaweza kumkomoa kwa pigo la kumpeleka ktk vyombo vya sheria.

Una pesa za kuendesha maisha yako si ndivyo? Mpaka sasa unavyoona pasipo hivyo viwanja kuna kitu ambacho kimeharibu maisha yako? Utaingia mgogoro na Mzee ila kiuhalisia familia nzima itatikisika ktk hili.

Utamfunga ila watakuja wengi wakikwambia ulotenda ni kubwa, either jamii, ndugu ama marafiki. Ishu za mtoto na mzazi ni ngumu. Ni wewe ndie unayesikia uchungu, wao hawafeel vile ambavyo wewe unafeel. Sio ajabu kwao kuja kukwambia umekosea kumpeleka vyombo vya sheria.

Mimi nnachokushauri ni hiki, achana na mzee. Ikiwezekana kata naye mawasiliano kabisa. Hizo fedha zitatumika mwisho kabisa zitaisha. Mzee atakumbuka fadhila za nyuma zote alizotendewa, na hapo ndipo atakapomkumbuka mkewe wa kwanza na msaada wako.

Hatoweza kufanya lolote zaidi ya moyo wake kumuhukumu, ogopa saana moyo wako ujihukuku kwa mabaya uliyomfanyia mtu, hata usingizi huwezi ukaupata kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom