Nakusuburi Tanganyika kwa vilio

Nakusuburi Tanganyika kwa vilio

albab

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
2,000
Reaction score
3,395
Salam kwenu waungwana.

Nakulilia mama Tanganyika, umeitwa na vijana urejee kwa hamu kubwa Je uko Tayari kurejea?? Je unarejea ukiwa katika hali gani?? Kama hauko tayari je mchakato wako wa utayari utakamilika lini na nani ataukamilisha; na mwisho nini matokeo ya mchakato mzima wa marejeo yako??

Kabla ya marejeo yako naomba nimuongelee mwanao wa kwanza TANZANIA. Baada ya muda mrefu hatimae kajaribiwa rasmi na muda si mrefu anaenda kuwa jalala lenye kila aina taka, kutakua na nzi, mbu, panya, mende, mbwa na wadudu wote wachafu tunaowafahamu wapo watazaliwa katika jalala hilo na wengi watatoka kwenye majalala ya nje kufuata harufu yako mbaya.

Wanaosifiwa kwa kuitwa wazalendo leo, wapambania jalala lijalo na wanaochukiwa wataikimbia harufu mbaya ya Jalala Tanzania wengi wataenda kwa mwanao wapili wengine hawatokuepo kabisa na walishaanza kupekeka mali zao, watoto wao na wengine tayari wana makazi ya kudumu kwa majirani. Walio itwa wazalendo watakucheka na maisha yao yataendelea kwa furaha tele ila dhamira na nafsi zao zitaendelea kuwasuta.

Jalala hili litajaa mfumuko wa bei sukari itauzwa 20,000 kwa kilo, unga hautouzwa dukani tena bali italazimu kusaga na utauzwa mara 10 ya ilivyo sasa, halitakua na ngano wala udhibiti wa mchele. Wanyama wake watauzwa nje ya nchi.

Hakutakua na ulinzi tena mitaji ya watu itateketea, polisi watakua wamechoka kwa kudharauliwa na ndugu zao kuuwawa na mali zao kuteketezwa, wawekezaji hawatokuwepo tena na waliopo watahamisha mitaji yao, viwanda vitabaki magofu. Walioitwa wanajeshi wataongoza magenge ya kihalifu, askari watakodisha silaha kwa wahalifu.

Je unakumbuka MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE.. ndipo Jalala linapoelekea usafiri hautokua salama tena, mapori yatajaa vikundi vya uhalifu na ugaidi utapia humo, rasilimali zinazopiganiwa leo zitakua za wachache na zitavuka na kuondoka nchini kama maji yatiririkayo.

Gen Z waliopigana usiku kucha watageuka takataka na vichekesho mbele ya wote wanaowapongeza leo... Watakao kuwa wameumia sio walioondolewa mana hawatokuwepo tena nchini bali ndugu na jamaa zao. Kilichokua kitovu cha biashara AKA Bandari Salama kitageuka KICHEKESHO na eneo lenye miundombinu ya hovyo bila usafi.

Sio LISSU, HECHE, SAMIA, JWTZ, WARIOBA MANGE, MWAIPAYA, MBOWE au yeyote atakaeweza kulisafisha jalala tena itakua ni harufu kila sehemu... vinyesi, maiti, damu, moshi, machozi na jasho vitandelea kutoa marashi mazuri kwa Jalala Letu pendwa. Vijana wengi wataangamia kwa madawa ya kulevya na jalala litakua soko huria la kete na unga wa sembe na dona.

Jalala Halitatawalika tena na utakua mwisho wa zama zake za kusifiwa sio Larry, sio CNN wala Aljazeera, TBC, BBC, ITV, CITIZEN sio Jambo tv, JF wala The chanzo watasifia bali watafanya biashara ya documentary itakayoonesha bandari na majengo pacha vs magofu na vijana wakiwa wametapakaa mitaani bila msaada mate yakiwadondoka.

Werevu watapaza sauti kuwaita vijana mezani itakua too late, hakutakua na muda wa maridhiano tena... Jalala litakua limefurika taka, zitamwagika na kusambaa, maiti kila kona tai, kunguru na panya watashiba kwa mizoga, maji hayatakua salama tena ya dukani hayatanunulika au pengine yasiwepo kabisaaa.

Nakulilia mama Tanganyika, Tanzania amekuponza.

Endapo utazaliwa utakua dhaifu kuliko yeyote duniani

Umeponzwa na vitukuu vyako baada ya kulindwa na wanao na wajukuu zako. Wamejiona bora, wanaitaka demokrasia, wanakutaka wewe... Njoo TANGANYIKA NA UTAKUA TANGANYIKA KWELI yule wa miaka ya 1940 je tutaweza kukujenga tena??

Mwerevu na aaelewe

Andiko hili litaishi kuiona kesho, kesho ya vijana, kesho iliyojaa uhuru, haki na demokrasia, kesho iliyojaa vibaraka waliojifunika mwamvuli wa uzalendo wenye matobo yenye kupitisha matone ya damu inayonyesha kutokea angala lako. Kesho itakayoongozwa na mitandao ya kijamii

KARIBU TENA TANGANYIKA JALALA LA VIJANA WALIO KUBALI PROPAGANDA ZA NEO GEN-Z.

MAJUTO NI SASA..... ZIMEBAKI SIKU CHACHE TUKUPOKEE TANGANYIKA KWA VILIO VIKUU, VIDONDA, MAUTI, DAMU, UDINI, UKABILA, UFISADI NA TAKATAKA ZOTE.

SALAAM.
 
Back
Top Bottom