Nakumbuka tu zamani

  • Thread starter Deleted member 421398
  • Start date
D

Deleted member 421398

Guest
Kipindi sisi tunasoma miaka hiyo ya nyuma madaftari yetu yalipambwa na picha za sungura, mbuni na wanyama wengine katika kurasa zetu za mbele na zikapambwa na hesabu za kuzidisha (table ya 1 hadi ya 12) na baadhi ya vipimo mbali mbali vya kimahesabu kuanzia hesabu za maumbo, hesabu za vipimo vya joto na kadhalika na kiukweli vilitufanya yujue vitu hata tukiwa majumbani baada ya kutoka shuleni.
Lakini maajabu ya sasa ni kwamba daftari za watoto wetu na ndugu zetu wa sasa zimepambwa na mapicha picha tu kama hilo hapo juu sasa sijui wanajifunza nn kwa mfano. Naona sasa elimu imekuwa kama biashara ya ndizi tu kwamba tutanunua na kupika na kula halafu biashara inaishia hapo hapo na kwa mfumo huu hatuwezi kuisimamisha elimu yetu kwasababu mambo madogo madogo kama haya yakiachwa yaendelee yanaharibu akili za watoto ambao watakaa kuyafikiria mapiki piki na wachezaji mpira na wacheza mieleka. Na kwa maana hii unadhani ni kwanini watahiniwa wa kidato cha nne wasikuchoree mazombi sijui wakina Messi na Ronaldo ni kwasababu ni vitu ambavyo wanaviona kila leo si kwenye Televisheni tu bali hata katika madaftari yake ya shuleni.
[HASHTAG]#thelawyer[/HASHTAG]
 
Desimali,
Desimita

Nyuzi jito ya mwili wa bin adam.
.
.
.
Sana tu asee yaani sasa hvi hakunaga hivyo vitu tena sasa hivi ni messi na ronaldo tu
 
Back
Top Bottom