A
Anonymous
Guest
Shule ya Longido Secondary iliyopo mkoani Arusha Wilaya ya Longindo imekuwa mateso kwa wazazi na wanafunzi, wana michango mingi pembeni kila mfano Kidato cha Tatu kila mwanafunzi anatozwa Tsh. 30,000, ukipiga hesabu kwa Wanafunzi 600 utajua mwenyewe hapo unapata kiasi gani.
Wanadai kiasi hicho ni kwa ajili tu ya motisha kwa Walimu, mtoto kama hataenda na kiasi hicho anachapwa viboko wakati ambaye hana fedha ni Mzazi/Mlezi.
Shule ilikuwa na wanafunzi 700+ mpaka sasa wamebaki 600+ takribani 100+ wamehama kwasababu tofauti ila mojawapo ni hili kuwarudisha na kuwapa adhabu na michango ya muundo huu.
Unajua sisi wazazi wengi hatuna uzoefu sana na masuala ya elimu kwenye vikao inakuja kama agenda kutoka kwa Walimu ni ngumu sana kwa wazazi wengi kukataa, hivyo wenye mawazo tofauti matokeo ndiyo kuhama na kukaa kimya kwa kuzidiwa na nguvu ya majority, hatukatai sasa ndiyo mpaka kumpiga mtoto kwa sababu hajaja na hiyo fedha.
Mwanzo kulikua na group la whatsap wazazi kulalamika kule likafutwa hatusei popote pale, ilikuwa kwa mwezi 10k sasa hivi wanasema 30k kwa quarter yaani tulipe na kidato cha tatu wabaki shuleni.