Nakumbuka nilivyofedheheka

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,271
2,401
Haya mapenzi kweli ni shida. Nakumbuka kitambo kidogo nikiwa A level sekondari moja ya bweni mkoani kaskazini huko. Ikatokea nilivutiwa sana na head girl. Alikuwa mzuri. Hope bado mzuri.

Asubuhi moja kabla ya assembly nikajivika ujasiri nikasema lazima nimueleze. Nilitoka bwenini na kuzunguka kiasi na haikuwa shida kumuona kwani alikuwa akisimamia usafi eneo fulani. Huku moyo ukinidunda nilimsogelea na kumsalimia. Kiukweli sikuwahi kuwa na mazoea nae wala maongezi nae. Nakumbuka yeye alikuwa kidato cha nne.

Nilisafisha koo nikampa salamu yangu...

Itaendelea.

Mwendelezo uko post ya 19
 
Haya mapenzi kweli ni shida. Nakumbuka kitambo kidogo nikiwa A level sekondari moja ya bweni mkoani kaskazini huko. Ikatokea nilivutiwa sana na head girl. Alikuwa mzuri. Hope bado mzuri.

Asubuhi moja kabla ya assembly nikajivika ujasiri nikasema lazima nimueleze. Nilitoka bwenini na kuzunguka kiasi na haikuwa shida kumuona kwani alikuwa akisimamia usafi eneo fulani. Huku moyo ukinidunda nilimsogelea na kumsalimia. Kiukweli sikuwahi kuwa na mazoea nae wala maongezi nae. Nakumbuka yeye alikuwa kidato cha nne.

Nilisafisha koo nikampa salamu yangu...

Itaendelea.
Kama bando limeisha sema tukuchangie kamanda
 
Hahahaaaa... Muendelezo huo...
Sasa baada ya kumfikia na kutakasa koo nikamsabahi. Aliitikia japo kwa wasiwasi. Nikaanza kumweleza ya moyoni...

Hapa niwaambie vujana nyie kuwa haya mambo ya kuassume tu si mazuri. Unachowaza si nwenzio awazacho. Ni sawa na kumkanyaga paka wako mkia. What do you expect? Tuendelee. Nukamwambia kiukweli nampenda na ningetamani awe wangu.

Head girl alinitazama kama asiyeamini anachosikia. Alibadilika hadi ule uzuri wake ukapotea ghafla. Nikajusemea moyoni, nimeharibu! Na kweli nilikuwa nimeharibu. Alinikazia macho akaniuliza, 'unasemaje?
Nikamjibu huku mate yakianza kukauka mdomoni, 'umenisikia, Joyce (si jina lake). Hapo pamoja na baridi ile ya asubuhi nilitamani kuvua shati.
Joyce akiwa kanikazia macho akaniambia, 'sikuja kuendekeza mapenzi mimi! Nimekuja kusoma. Kawafuate hao hao uliozoea...! Na mengine sikuweza kukumbuka muda ule.

Sikujua kama waliokuwa jirani waliweza kusikia au la. Sikuwa tena na sera. Yale yote niliyopangilia kumwambia ikiwa ni pamoja na kupangua hoja zake viliyeyuka. Nilimjibu tu kinyonge kuwa sawa nimemwelewa. Taratibu niligeuza na kuanza kuondoka. Sikumbuki kama nilitazama nyuma.

Moyoni nilijutia kwa uamuzi ule wa pupa asubuhi ile. Sikutegemea reaction ile. Nilidhani angenijibu tu kwa taratibu. Pengine haukuwa muda muafaka. Nillijiambia. Nilirudi hadi bwenini. Wakati huo ni wa usafi wa nje. Kukaa bwenini na ukakutwa ni kosa. Sikijali. Nilikuwa nimechoka asubuhi ile. Niliingia bwenini na kujilaza deka ya chini. Mimi nilikuwa nalala juu. Kulikuwa na baadhi ya wanafunzi mle bwenini wakiwa wakowako tu. Muda si mrefu kengeke ya assembly ikaita. Tangu muda huo sikujitambua tena. Sikumbuki kama nililala usingizi au nilizirai, au nilizama tu kwenye mawazo. Nachokumbuka nilikuwa nawaza ile scenario ilivyokuwa. Wapi nilikosea, kwa nini nilikosea, kwa nini sikuwa na subira, alimaanisha kweli? Na kadhalika nyingine.

Assembly kwa kawaida huwa tunasimama kwa nusu saa hivi ikowa ni pamoja na ukaguzi, sala, matangazo, n.k. Nilikuja kushtuka mlango wa bweni ukifunguliwa kwa pupa. Nilikiwa nimejilaza deka la mwanzo tu upande wa kulia unapoingia ndani. Sikuamini kwamba sikwenda assembky. Sikuamini kuwa sikusikia chochote toka huko nje kwa muda wote huo. Wala wakati wenzangu wanatoka kwenda assembly sikujua. Nulijiuliza ni nini kimenipata? Ni kupatwa kwa Jouce tu? Niliamka taratibu nikijiandaa kwenda darasani

Itaendekea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom