Nakukumbusha mambo 50 kuhusu mkeo

Nakukumbusha mambo 50 kuhusu mkeo

Umeandika vingi vizuri ila walio wengi wanataka yale ya Mke hapaswi kugusa simu yako, mke hapaswi kuuliza ukichelewa kurudi, Mke mmoja analemaza lazima uwe na mchepuko na mengine mengi yasiyojenga na hayo ndio wanapenda kuyasikia. Ila haya mmh.

Pia nikupongeze Mkuu sababu kwa wenye akili baadhi yatawafaa tena sana tu.
Upo sawa kabisa. Mimi ni mwanaume, ila sipendi wanawake wanyanyaswe katika ndoa. Ndoa sio jela, inapaswa kuwa paradiso kwa mume na mke kabla kifo hakijatenganisha. Uwa najiuliza nitajikiaje nikiona dada yangu au binti yangu akija kunyanyaswa? Hivyo ukiheshimu mwanamke na kumtunza vema ni heshima na faraja sio kwake tu bali kwa kaka zake, baba zake, wajomba zake ambao ni wanaume wenzako. Asante.
 
Acheni drama
Kwanza nyie wanawake mshaambiwa ni wanyonyaji tu (sio wote) ndio maana wengi wenu hamtaki kufanya kazi mnataka mkae nyumbani tu, na ikitokea mkatoa support kwa mwanaume basi mtamsimanga mwaka mzima.
 
Umeandika vingi vizuri ila walio wengi wanataka yale ya Mke hapaswi kugusa simu yako, mke hapaswi kuuliza ukichelewa kurudi, Mke mmoja analemaza hivyo lazima uwe na mchepuko na mengine mengi yasiyojenga na hayo ndio wanapenda kuyasikia. Ila haya mmh.

Pia nikupongeze Mkuu sababu kwa wenye akili baadhi yatawafaa tena sana tu.
Yamekugusa!
 
Sawa umeongea points za maana.
Lakini je wanaelewa yawapasayo kutenda na wao?

Ni mambo mazuri sana ukimpata mnayeendana kimatendo na mawazo ya kulijenga na kuliendeleza penzi motomoto.
 
Mwanamke ukimdekeza sana anakuzoea....sometimes makofi ya uso yanawapaga adabu....
 
Wanawake kwa kujisifuuu aah haya eh😀😀😀😀😀
Na ndiyo maana wana VYAMA kibao mpaka na siku yao... kuanzia vya vya madaktari, wanasheria, benki ya wanawake..etc etc... lakini badooo
 
Unajua wanawake wanapigana "senseless war", kuna "matrixs" walishapewa kuhusu ukandamizaji toka kwa wanaume, sasa rejea asili, hapa tutumie tuu andiko la asili ya binadamu, "Vitabu vitakatifu/tukufu", haki inatokana na wajibu, MUNGU aligawaa duties tofauti, kwa nini tupate haki sawa?. Yaani haki ya mwalimu achukue afande😀😀😀

yaani nilimuuliza mwanamke mmoja, akaniambia kwamba anataka kuwa kama mwanamume, and she real fights, sasa unajiuliza ina maana mwanamume ndie mwanadamu kamili au? what if akapigana kuwa yeye kama yeye, wanasiasa wamewalisha matangopori. 😀😀😀
 
Na ndiyo maana wana VYAMA kibao mpaka na siku yao... kuanzia vya vya madaktari, wanasheria, benki ya wanawake..etc etc... lakini badooo
mlevi akishajijua ni dhaifu, hurudi kwake akiwa anajihami kwa maneno ya kujifariji njiani.😀😀😀
 
MAMBO 50 KUHUSU MKEO

1. Mkeo sio mkamilifu, msamehe.

2. Mkeo ndio uti wako wa mgongo, usiuvunje.

3. Mkeo ni tunu, mthamini.

4. Mkeo ni kito adimu, mtunze.

5. Mkeo ni rafiki yako bora, mfanye kuwa rafiki yako.

6. Mkeo ni furaha yako, mnawirishe.

7. Mkeo anatakiwa kuwa bora kabisa, mchangamkie.

8. Mkeo ni pande la mwili wako, mstawishe.

9. Mkeo sio ibilisi, usimpige teke.

10. Mkeo sio mzuri tu kitandani, mshirikishe katika kila jambo.

11. Mkeo sio adui yako, mshajiishe.

12. Mkeo sio kikaragosi, usikubali akachezewa na watu.

13. Mkeo sio hasimu wako, usishindane naye.

14. Mkeo ni mwanamke, mheshimu.

15. Mkeo sio mtu wa kawaida, usimlinganishe na wengine.

16. Mkeo sio sahani ya kunawia, usimdhalilishe.

17. Mkeo ni kama chombo laini, shughulika naye kwa uangalifu.

18. Mkeo ni malkia maridhawa, muadhimishe.

19. Mkeo sio bondia, usipigane naye.

20. Mkeo sio begi la mazoezi ya ngumi, usimpige.

21. Mkeo sio mchezo, usimchezee.

22. Mkeo anahitaji kunyegeshwa, msimbake.

23. Mkeo ni sumaku, nasa kwake.

24. Mkeo ndio gwiji wa mahabba, msifu.

25. Mkeo ni mtu muhimu, mpe taadhima.

26. Mkeo ndiye mkeo, mkubali.

27. Mkeo ndio mzinga wa asali yako, mfukuzie.

28. Mkeo anahitaji taadhima yako, usimuaibishe hadharani.

29. Mkeo sio kisu, ishi naye kwa wema.

30. Mkeo ni wa kipekee, usimdhihaki.

31. Mkeo ni mwenye kukuenzi, usimtilie shaka.

32. Mkeo sio mpumbavu, sikiliza ushauri wake.

33. Mkeo sio habithi, usimfanyie uhabithi.

34. Mkeo ndio rafiki mwenye muamana, mfanye kuwa rafikiyo.

35. Mkeo sio leso, usimtumie vibaya.

36. Mkeo sio mfanyakazi wako wa ndani, msaidie jikoni.

37. Mkeo ni mwenye ashiki, usiache kumuenzi.

38. Mkeo ni muhimu sana kwako, usimtelekeze.

39. Mkeo ni malkia muadhama, usizozane naye.

40. Mkeo ndio mmiliki wa kiti cha moyo wako, msaidie akikalie vizuri

41. Mkeo ana akili, usimshushe thamani.

42. Mkeo ni jukumu lako, mhudumie.

43. Mkeo ndio wewe mwenyewe, usimtenge kitandani.

44. Mkeo ni namba moja katika maisha yako, mpe kipaumbele.

45. Mkeo ni hazina yako, ilinde na uitunze.

46. Mkeo anahitaji usaidizi wako, msaidie.

47. Mkeo anahitaji umakini wako, usimakinike kwenye T.V

48. Mkeo ni mwenye thamani, muongezee thamani.

49. Mkeo ndio taji lako, usimuache.

50. Mkeo ndio Layla wako, uwe Majnun wake.
Tatizo wanawake wa sasa hata ukawafanyia jema gani hawaridhiki kabisa, ila sio wote japokuwa wengi wao sasa hv hawana mapenz ya dhat,mwanaume ukipenda na kujali ndo wanakuona mjinga..
 
Back
Top Bottom