Nakukumbuka sana mdada.....

Nakukumbuka sana mdada.....

Yeah though sometimes with too much pain,we fall down but God helps us rise again.Am pretty sure God will rise somebody for you oneday that will help you cure your wounded heart.
Thank you, but life is going on.
 
"YOU WILL NEVER HURT SOMEONE YOU LOVE." sarikoki ni kweli hii??
:focus: Pole kwa yaliyokukuta mkuu.. Ni kweli wanawake wanawapendaga waseminari sijui kwa nini!!

Kweli kabisa WI-FI ,you will never.....unless you dont love that someone anymore. Hehehehe...waseminarist....wanajua watapata chakula cha kiroho.:smiling:
 
Duuuuuuuuuuum aisee umenikumbusha mbali, machozi yananitoka! wengi tumekutwa na masahibu kama haya. U loose someone with whom u had special moments in life!
 
Tunatoka mbali eehh.

Kaunga nimependa hii ..........When you run out of rope; grab onto faith.......... T.B Joshua,

Na kwa kuongezea ni kwamba hamna zambi mbaya kama ya kukata tamaa......if you grab onto faith nothing is impossible.
 
Kaunga nimependa hii ..........When you run out of rope; grab onto faith.......... T.B Joshua,

Na kwa kuongezea ni kwamba hamna zambi mbaya kama ya kukata tamaa......if you grab onto faith nothing is impossible.

Inasaidia sana when the goings are tough!
 
Kweli kabisa WI-FI ,you will never.....unless you dont love that someone anymore. Hehehehe...waseminarist....wanajua watapata chakula cha kiroho.:smiling:

ha ha sio kwamba wanataka watu wakuwaendesha/kuwaonea??
 
ha ha sio kwamba wanataka watu wakuwaendesha/kuwaonea??

Aisee....sikuwa nimelifikiria hilo kwa kweli.....na ukiangalia wanaume wote wapole wanapendwa na badgirls..ili wawakalie...du!
 
Na it will never get easy kwa hapa duniani....lazima kuna milima na mabonde.

Kitu kingine nilichojifunza ni kumtupia Yesu mambo yangu yale ambayo kwa nguvu zangu siyawezi; so l stop worrying n thinking about them na kama miujiza vile solutions zinapatikana. I use to worry about almost everything, kiasi kwamba sleepless nights was my order of the day.
 
story imenifurahisha,ingawa mwisho wake imenisikitisha.eti nasikia ukiwa na lafudhi ya kichaga hata ukae mjini miaka mingapi huwa haiondoki.ni sawa na lafudhi za kipemba.jee mpaka leo unayo lafudhi ya kichaga?
 
Siku ya valentine wengi wanaikumbuka kwa mazuri na wengine kwa machungu.....
Mimi nakumbuka wakati niko chuo nimetoka mkoani, alitokea dada mmoja kunipenda sana pale chuo......huyu dada alikua ni mtoto wa mujini....alikua akijua mambo mengi sana ya town kuliko mimi, (mfano kama wa Lara 1 ivi). alikua ni badgirl ninaweza kusema.
Huyu dada alitumia muda mwingi sana kunibadilisha ili niwe kama vijana wengine, mimi nilisoma shule ya dini kwa hiyo nilivyokuja mjini nilikua bado nina yale maadili ya kila siku saa kumi na mbili lazima niudhurie misa kabla ya darasa..pia nilishiriki sana shughuli za kanisa kama kumsaidia padre na mda mwingi wa ziada niliutumia kwenda kufanya shughuli za kanisa.
Huyu dada nakumbuka alitumia mpaka pesa zake kuninunulia suruali za jeans na shati za bahama.....alikua anakunywa pombe na kwenda disco...alikua kila siku akirudi usiku lazima aje agonge chumbani kwetu aniamshe aanze kunipigisha story.....nilikua nampa ushauri na kumsihi aache tabia hizo....tulizoeana sana mpaka nIkajikuta na mimi ameanza kunichukua na kunipeleka kwenye starehe........Na kote tulikoenda alikua na company ya wasichana wenzake. Alinifanya marafiki zake wengi wanipende jinsi nilivyo.....nilihisi ushamba wangu na jinsi nilivyokua naongea lafudhi ya kichaga ndio kiliwavutia manaa walinifanya ze comedy, kila nilichoongea kilikua kichekesho kwao, nilikua siendani nao hata kidogo kuanzia mavazi hata muonekano...kila nilipokaa nilizungukwa na wasichana.....na mara nyingi niliwafanyia asignment zao na kuwafundisha. nahisi ingekua ni sasa watu wangefikiri nilikua gay.
Namkumbuka huyu dada siku kama ya leo kwa sababu ndiye wa kwanza kunipeleka dinner , namaanisha dinner kwenye hotel ya kisasa. Aliniletea shati jekundu ,suruli nyeusi nilikua nayo....... nilijua tunaenda kula kama ninavyoagiza hapa canteen.... tulipofika kwenye hiyo hotel nilitaka nirudi....sikuwai kuingia kwenye hotel kama ile.....aliuweka mkono wangu kwapani kwake, aliubana kwa nguvu huku akinivuta na kwa sauti ya kunong'oneza alinisihi nisibadilishe mawazo. Tulifika tukakaa......... meza ilijaa vijiko na visu vingi sikujua ni vya nini vyote hivyo......alikuja muhudumu akanipatia kijitabu, kilikua na kurasa kama sita hivi...kwa kweli sikujua nianzie wapi...nilihisi nguo zote zinanibana.....kwa uso wa tabasamu na furaha alini sogelea akanisaidia kunielekeza jinsi ya kuchagua chakula.....chakula kipokuja nilijikuta nikilalamika kuwa wamesahau kijiko...... nilichoka zaidi aliponiambia nitumie umma na kisu......nilimsihi amuite mhudumu alete kijiko la sivyo naondoka..... alikubali ombi langu na mhudumu aliniletea kijiko.
Sikuwai kumuona huyu dada akicheka kama siku hiyo....wakati tunarudi ,njia nzima mpaka tunafika chuo alikua akinicheka kwa ushamba na vituko nilivyomuonyesha pake hotelini hasa pale nilipocomment ndio alicheka mpaka alikaachini.....mimi pia nilifurahi sana.

Mpaka leo nakukumbuka mdada...namshukuru Mungu kwa mda aliotukutanisha kwani ulibadilisha maisha yangu......ni wewe ndio ulinikumbusha kuwa duniani kuna wasichana na pia hukunifundisha tu kutumia umma na kisu pale mezani.....ulinifundisha pia kitandani.
Najiuliza sana hivi ungekuwepo hai mpaka sasa ingekuaje? Sijapata jibu mpaka sasa.
Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi mdada.

Natamani kujua alikufa kwa ugonjwa gani? Sijui kwa nini
 
story imenifurahisha,ingawa mwisho wake imenisikitisha.eti nasikia ukiwa na lafudhi ya kichaga hata ukae mjini miaka mingapi huwa haiondoki.ni sawa na lafudhi za kipemba.jee mpaka leo unayo lafudhi ya kichaga?

Unautani wewe.... ila nafikiri uko sawa...... kwa sisi tuliozaliwa nakukulia kule kijijini lafudhi haiwezi potea....hata kama ukiilazimisha ipotee kuna maneno mengine lazima utakosea tu...labda kwa vijana wetu tuliowazaa hapa mjini. Wachaga wa Dar.
 
Kitu kingine nilichojifunza ni kumtupia Yesu mambo yangu yale ambayo kwa nguvu zangu siyawezi; so l stop worrying n thinking about them na kama miujiza vile solutions zinapatikana. I use to worry about almost everything, kiasi kwamba sleepless nights was my order of the day.

Hii ni kinga moja kubwa sana.....hamna kitu kitakuogopesha dunia hii if you rely on Jesus. Hata wachawi nao wanaomba Mungu...sasa cha kushangaza binadamu wanapopata matatizo wanakimbilia kwa waganga na wachawi.....its so sad.
 
Mimi kwa jinsi nilivyo mpenda wangu. Niliweka nadhiri mbele ya halaa kifo akiwezi kututenganisha. Leo nipo nagaragara juu ya kaburi lake, nimelipamba maua tu. Kwa hakika nampenda
 
Back
Top Bottom