Nakujibu mwanasheria Halima Mdee kama nilivyomjibu David Kafulila

Chikawe Jr

Member
Jun 6, 2017
23
85
NA
Juma George Chikawe.

Nimeona katika mitandao ya kijamii baadhi ya hoja ambazo zinasemekana zilitolewa na upinzani kupitia kwa kiongozi wao wa BAWACHA, Halima Mdee. Kwa taaluma Halima Mdee ni mwanasheria na anajinasibu kuwa yeye amebobea katika mambo ya sheria siku zote katika majukwaa mbalimbali, hii ni ishara kuwa hoja alizozitoa katika PRESS yake amemezeshwa na watu wanaowaandikia habari hizi siku zote. Kuna makosa ya msingi yanayojitokeza pale unapolishwa jambo na kuagizwa ukaliseme mbele ya watu huku ukiwa hujui hicho ulicholishwa na kuambiwa ukakiongee ni kitu gani. KIUJUMLA HALIMA MDEE alichoongea ni "Rubbish" Tu.

Mnamo tarehe 17, Mwezi wa 4,2017 nilimjibu Kafulila baada na yeye kutoa hoja za kitoto alipozungumzia UCHUMI katika ngazi ya TAIFA kama mwanafunzi wa sekondari. Kidogo Kafulila haikunipa tabu kwa sababu ni 'Mate' wangu High level akiwa anasomea nadharia za uchumi kwa mchepuo wa EGM, ilikuwa rahisi kumrudisha darasani akanielewa kwa urahisi tu na hakuwa na neno. Hata huyu mwanasheria nitamwelekeza tu hata kama alisoma HGL na Sheria, najua ujumbe huu utawafikia na wale wanaowalisha hawa vitu ambavyo sio sahihi na wao kuja kuongea tu bila kujua anaongea nini.

HALIMA MDEE alikuwa anajinasibu eti msemaji wa serikali hakujibu HOJA zao, wanataka awajibu HOJA zao. Hoja zenyewe eti ni
1) Kupungua kwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ruzuku ya mbolea 78b mpaka 10b.
2) Akiba ya chakula 2015 ilikuwa Tani 406,846 ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo ni tani 74,826.
3) Bei za vyakula kupanda kwa kulinganisha mwaka 2015 na 2017 na katoa mfano 'mahindi na mchele'.

Anachojisifu kuwa ni HOJA na kutaka zijibiwe KIUCHUMI ni RUBBISH tupu, lakini nitamjibu tu ili siku nyingine asitumwe bila kujua kabebeshwa mzigo gani, maana kinachobebeshwa mzigo na hakijui kimebeba nini ni PUNDA tu peke yake.

Nikianza na hoja yao ya kwanza, Kupungua kwa fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo kutoka 78b mwaka 2015 mpaka 10b mwaka 2017. Hii sio hoja hili ni swali na nadhani walishajibiwa Bungeni na Waziri husika. Pia swali lake halina mahusiano kabisa na halijawahi kuwa economic variable in the so called "Economic Equestion". Kupanda au kushuka kwa mgawo wa fedha za bajeti ni matokeo ya utafiti wa mahitaji ya gharama husika za mbolea kutokana na shughuli za kilimo zilivyo hivi sasa hapa nchini. Tafiti zinaonyesha mahitaji ya pembejeo katika nchi yetu *YALIKUZWA* ili watu wajipatie fedha zisizo halali. Katika maeneo muhimu ya mafisadi kiibia serikali yetu mojawapo ilikuwa pembejeo za kilimo. Aidha pembejeo ambazo walisema zinafikia 78b kama budget ya 2015 inavyoelekeza sio kiwango halisi cha pembejeo zinazotumiwa na wakulima kwa sasa. Kimsingi pembejeo zinazotumika na wakulima wetu kwa sasa zinatosha kabisa kwa bajeti hiyo ya 2017 ya 10b. Hii inatokana na aina na muundo wa kilimo chetu nchini. Hivyo katika bajeti ya 78b serikali ilipoteza fedha kwa kuwa gharama hizo hazikuwa halisi na malalamiko mengi ya *UFISADI* yalitokea. Serikali imechukua hatua ikiwemo ya kuwataka waliochukua fedha hizo kuzirudisha. Hii itasaidia kufanya 'Gap Analysis' katika kilimo chetu hasa katika mahitaji ya pembejeo katika kuboresha kilimo nchini.

Hoja ya pili ya Halima Mdee, mwanasheria huyu, anasema akiba ya chakula imeshuka kutoka 406,846 ya mwaka 2015 mpaka 78,826 mwaka 2017. Na hii nayo ni Rubbish tu ila nitaijibu. Serikali haina mashamba bali hukusanya chakula hicho kutoka kwa wakulima wenyewe kwa kununua. Mkulima anahaki ya kutafuta bei anayoona inamaslahi makubwa kwake na wakati mwingine wakulima huchagua kuuza nje ya nchi chakula au kwa watu binafsi kutokana na bei. Ikumbukwe hao hao wapinzani ndio waliilazimisha serikali kuondoa zuio au katazo la kuuza nje ya nchi kwa wakulima na serikali kufanya hivyo jamba ambalo lilipelekea chakula kingi kuuzwa nje ya nchi ikiwemo *MALAWI, KENYA,BURUNDI NA SOUTH SUDAN*. Katika soko huria la namna hii ni kawaida sana kwa serikali kukosa chakula kwa ajili ya ghala na ikumbukwe serikali inanua na kuuza kwa bei elekezi. Hili nalo halihusiani na Economic equestion na wala halijawahi kuwa variable katika kupima UCHUMI wa nchi yoyote duniani. Tunapopima uchumi kuna viashiria vyake tunaangalia lakini sio hivi kama alivyovisema Halima Mdee.

Hoja ya tatu, Mdee anasema, Bei za vyakula kupanda ametolea mfano gunia la mahindi na mchele. Nayo hii ni rubbish. Price is determined with time and availability of commodity in the market. Wakati mwingine kupanuka kwa soko la biashara kunatoa fursa kwa mwenye bidhaa kuudha popote na hii inaongeza ushindani katika bei ya kununua. Kuruhusu uuzaji wa bidhaa ya chakula nje ya nchi kulichochea sana ongezeko la bei katika masoko yetu ya ndani.

Kwa mtazamo wa Halima mdee anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Uchumi wa Tanzania ulikuwa mkubwa miaka ya 2000 kuliko sasa jambo ambalo si kweli. Katika miaka ya 2000, Bei ya gunia la mahindi lilikuwa Tsh 25000 na kilo 1 ya unga iliuzwa Tshs 600 je ni kweli kipindi hicho uchumi ulikuwa mkubwa kuliko sasa? Jibu si kweli. Uchumi haupimwi kwa ulinganifu wa bei na muda, wakati mwingine mabadiliko ya bei bila kuathiri uwezo wa watu kununua ni ishara ya kukua kiuchumi na kukua kwa soko pia.

Hivyo Halima Mdee usikalilishwe maneno ambayo huyajui.

Najua ni agenda yenu kuwaondoa watanzania katika agenda ya kutetea rasilimali zetu kama inavyoendelea sasa. Wananchi tumejipanga katika umoja tukiiombea kamati teule ya RAIS inayotuwakilisha katika kikao cha madai ya fedha za nchi na kwa pamoja tunaunga mkono.

*Iwe kwa njaa au kwa kushiba agenda ya madini ndio Priority ya watanzania kwa sasa Mdee na wenzio hamna nafasi kwa sasa.*

Juma George Chikawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupotosheni tu lakini msisahau hoja mojawapo ya Mh. Halima ni pesa zilizokuwa allocated kwenye mikopo elimu ya juu zimepunguzwa wakati wanafunzi wanaoitaji mikopo wameongezeka! Benki pia zinapata hasara na zimekiri.
Tushawishini kwa hoja zinazoeleweka basi na sio kama ya yule daktari wa falsafa!
 
Umerudi kulekule kwa Msemaji wa Serikali na bora hata msemaji wa Serikali alitupatia takwimu ingawa hazikuwa sahihi kwenye majibu yake sio Mchumi ndio mana hakulaumiwa kosa lake ni kuja kujibu hoja asizokuwa na uwezo nazo,angewaachia wataalamu wa uchumi.

Katika andika lako umepinga hoja za Halima lakini hukumrudisha shule kama Mchumi ulivyomrudisha shule Kafulila,unaposema economic variables ni zipi tofauti na hizo alizosema Halima.

Tunapimaje kukua kwa uchumi,ni indicator zipi zinaangaliwa?Pia ukatusaidia na hali mbaya ya Uchumi inapimwaje katika hiyo So Called Economic Eqn.

Je ni kweli tuna hali nzuri kiuchumi?Purchasing Power Yetu ipoje?Inflation rate?Uwezo wa kukopesha wa Mabank Yetu? Uwezo wa kukopesheka? n.k

Hali ya Stock za Fedha za Kigeni?Trend ya GDP Yetu.

Trend ya Money circulation?

Stock ya Mazao?

Na nini application za hizo economic katika trend of economic growth katika miaka linganishi?

Then Fact kutoka BOT,WB,IMF n.k

Karibu Tujifunze.

Sent Using Sumsung S6 Edge
 
Kwasababu umeamua kujibu hoja kwa kutumia mfumo wa lugha chafu a.k.a matusi ngoja tukujibu kwa mtindo huohuo. Hao wanaokushikisha ukuta waliokutuma umjibu Mdee kipuuzi waambie mpaka sasa hatujaona nafuu yoyote hasa sisi wakulima. Pembejeo tunazipata kwa bei juu huku tukiuza kwa bei ya kulaliwa. Biashara zilizo nyingi zinafungwa au kulegalega sana. Na ushahidi ni pale utakapoenda kwenye taasisi za fedha kutaka mkopo ni ngumu kupata kulinganisha na huko nyuma. Hivyo wakati unanyonya mic za Me wenzio usimeze mpaka ule uji mzito wa kupatia mtoto a.k.a manii. Kisha leo wakati mnambandikia mzee maji ya kuoga baada ya kukupona mwambie kwenye uchumi mambo ni mabaya tunataka mabadiliko. Ukiweza jibu kwa heshima na hoja, lakini ukitumia disk mbovu tutakujibu kwa kuweka flash chafu.
 
nyie zungukeni lakini kipimo cha kukuwa kwa uchumi ni maisha halisi ya watanzania, maisha yamekuwa juu kwa kuchangiwa na vyakula kuwa juu na pesa zetu za ndani thamani inazidi kushuka siku hadi siku, zamani ilikuwa tunakula mlo mmoja sasa ivi hatujui kama tutakula siku inayofuata
 
Duh aisee hakuna alosoma anipe summary?'
kwamba, katika uchambuzi wake, mdee ametumia issues ambazo ni non- economic equetions na kuzifanya kuwa economic equestions, jambo ambalo kiuchumi si sahihi.
Anzia hapo sasa brother.
 
kwamba, katika uchambuzi wake, mdee ametumia issues ambazo ni non- economic equetions na kuzifanya kuwa economic equestions, jambo ambalo kiuchumi si sahihi.
Anzia hapo sasa brother.

Asante sana ubarikiwe
 
Duh aisee hakuna alosoma anipe summary?'
Jamaa ameandika upuuzi mtupu,ukisoma ni upotevu wa muda!Kanichosha kusema kupungua kwa ruzuku kutoka 78B mpaka 10B hakuna uhusiano wowote na uchumi wa nchi,ni uamuzi tu!!!!
Basi kwanini tusifanye uamuzi ikawa 200B ili wakulima ambao kimsingi ni asilimia 70+ ya watanzania wakanufaika!

Pia jamaa limeongeza kuwa mfumuko wa bei hauna uhusiano wowote na kuporomoka kwa uchumi,its a shame anajiita msomi!
 
Tupotosheni tu lakini msisahau hoja mojawapo ya Mh. Halima ni pesa zilizokuwa allocated kwenye mikopo elimu ya juu zimepunguzwa wakati wanafunzi wanaoitaji mikopo wameongezeka! Benki pia zinapata hasara na zimekiri.
Tushawishini kwa hoja zinazoeleweka basi na sio kama ya yule daktari wa falsafa!
Atajibu wanafunzi ni hewa!
 
Umerudi kulekule kwa Msemaji wa Serikali na bora hata msemaji wa Serikali alitupatia takwimu ingawa hazikuwa sahihi kwenye majibu yake sio Mchumi ndio mana hakulaumiwa kosa lake ni kuja kujibu hoja asizokuwa na uwezo nazo,angewaachia wataalamu wa uchumi.

Katika andika lako umepinga hoja za Halima lakini hukumrudisha shule kama Mchumi ulivyomrudisha shule Kafulila,unaposema economic variables ni zipi tofauti na hizo alizosema Halima.

Tunapimaje kukua kwa uchumi,ni indicator zipi zinaangaliwa?Pia ukatusaidia na hali mbaya ya Uchumi inapimwaje katika hiyo So Called Economic Eqn.

Je ni kweli tuna hali nzuri kiuchumi?Purchasing Power Yetu ipoje?Inflation rate?Uwezo wa kukopesha wa Mabank Yetu? Uwezo wa kukopesheka? n.k

Hali ya Stock za Fedha za Kigeni?Trend ya GDP Yetu.

Trend ya Money circulation?

Stock ya Mazao?

Na nini application za hizo economic katika trend of economic growth katika miaka linganishi?

Then Fact kutoka BOT,WB,IMF n.k

Karibu Tujifunze.

Sent Using Sumsung S6 Edge
Mkuu siongezi chochote hadi nione amekujibu ndio nimtolee uvivu
 
Nitakuchallenge kwa manufaa ys umma siyo kwa manufaa ya kichadema/kiccm..!

Vipi ndugu wewe uoni na ni RUBISH TWICE, kuibua projections zako bila reflectional statistics eti mahitaji ni 10 billions, afu unaondoka bila kutwambia inawezekanaje nchi ambayo 65% to 70 % ya watu wake depends on agriculture uje na simple projection isiyo ata na chembe ya analytical data

Tangu babu kuja baba sasa mimi tumelima, asiyejua hali ya pembejeo za kilimo nchini ni nani?? Labda awe siyo raia wa nchi hii..! Vile vile issue ya chakula inaweza isiwe issue sana ila mtambue siasa hazitakiwi kwenye UCHUMI hapa namba zinaongeo na kujibiwa na real situation ukisema uchumi unakuwa lazima variable statics zioneshe, taarifa ya mabenki inaongea kinyume sekta binafsi ambayo ndiyo ingine ya uchumi wa taifa lolote benki zinadai haikopesheki..!

Siyo mchumi wa makaratasi ila niko na elimu ya uchumi wa uzoefu na uchambuzi wa takwimu za kisekta.

Serikali haiwezi kujificha nyuma ya tuhuma za UFISADI eti kutuaminisha pembejeo za 10 billions zitoshe kwa nchi nzima ni uongo uliotukuka.
 
Nimekuelewa sn.ahsante kw uchambuzi mzuri.bank ya dunia wanasema uchumi wa tnznia unapanda kw kasi.lkn mwanasheria mdee anasema uchumi umepolomoka.MAKUBWA.lkn najua manyumbu na mapunda yaliyobebeshwa mzigo yatakutukana sn.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom