Nimekuwa nikiumwa tumbo sana sielewi tatizo ninini.Nimetumia tiba mbalimbali kama dawa za minyoo na za typhoid lakini sijapona hapa mwananyamala naona wananisumbua au wanabahatisha tu.Nimekuwa nikiharisha mara chache sana ila tumbo limekuwa likiunguruma.Naombeni ushauri wakuu maana naona nakufa.
nenda ospitali ya maana sio mw'ala. Usibanie pesa utakufa. Pole lakini. Kunywa maji mengi hasa asubui kabla hujala chochote. Google watertherapy utapata info. Kama unakunywa vya jioni acha kwa sasa
Unahitaji kumuona daktari wa upasuaji (surgeon)...afya yako kwanza, halafu pesa baadae! Sidharau madaktari wa M'mala, lakini kila daktari ana upeo wake wa ujuzi, na ndio maana kuna madaktari bingwa.
Kaka inaweza kuwa h-pyroli namaanisha ni bacteria wanaopelekea vidonda vya tumbo.ukipimwa wakaonekana mapema unapewa dozi ya mwezi mmoja.ukimaliza unakuwa umepona kaka kama umeiwahi.
pole sana ndugu nenda hosp. kama vipi chemshwa mwarobaini ongeza na majani fulani yanapandwa kama maua ila hayachanui, ukipata hiyo dozi kwa siku tatu wewe mzima kama zamani - samahani dr. riwa hii nayo ni tiba mbadala.