Nakuchukia Baba yangu

Nakuchukia Baba yangu

Wakuu,

Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.

Baba yangu aliondoka nyumbani mwaka 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Najua baba yako haiwezi chukia 'manii' yake..!!
 
Kuna reality tv talk show, huyu mzee kamwita mwanae anamueleza sababu zilizofanya amtelekeze yeye na mama yake.
Alisema kipindi hicho alikuwa bado kijana mdogo, hana pesa wala hakuwa na kazi ndio maana aliamua kuondoka.
Kijana akamuuliza mzee, kwahiyo sasa hivi una pesa? Mzee akajibu hapana, ndio kijana akashangaa sasa umerudi umefuata nini?
 
Ulikuwa na wiki mbili ulijuaje kama kakimbia na mwanamke mwengine? Wazee miyeyisho wapo, ila nimejifunza kuwa makini sana tunapowatuhumu wazee wetu, wengi wamebeba siri nzito sana ambayo wakikuambia utajikana na utaishi maisha ya upweke sana.
Mpe dingi 👊 maisha yaendelee kwenye maisha kuna mambo mengi sana huenda dingi alipigwa msumari akawa hajitambui Bora hata wewe dingi bado yupo wengine wamekua wanakuja pata taarifa dingi alishaga kufa muda sana
 
Ulikuwa na wiki mbili ulijuaje kama kakimbia na mwanamke mwengine? Wazee miyeyisho wapo, ila nimejifunza kuwa makini sana tunapowatuhumu wazee wetu, wengi wamebeba siri nzito sana ambayo wakikuambia utajikana na utaishi maisha ya upweke sana.
.
 
Pole sana Mkuu dah kuna maumivu mengine ni ngumu sana kupona. Pambana wanao wasipitie hayo Mkuu na Mungu hatakuacha kisasi sio kizuri.
 
Ulitaka ukimchukia ndio atakufa.

Unamsamehe tu ila hapati kitu changu chochote........hii kubembelezana ni kulea ujinga.

Pesa zako unakula na mademu na pombe mimi za jasho langu uje kula bure tu? Huu ujinga mimi nilishaacha.

Sikufanyi kitu, wala sifatilii mambo yako ila changu cha jasho langu utakisikia kwenye redio. Maisha yanaendelea

Word.
 
Au vipi? Walikuwa wanatutusha eti kuna laana😅😅

Mtu anaye mtelekeza mtoto asiyeweza kujisaidia ni muuaji na wewe mtelekeze hakuna cha laana wala baraka utapata toka kwake. Wabongo waache kujazana upumbavu endelevu tu na kutetea hawa kenge.
 
Unamchukia kwakuwa bado yupo.

Ila akifariki ndio utajutia uamuzi wako.

Tafuta muda utengeneze nae.

Hakuna mtu muhimu kama baba, ingawa feminist wanasema nani kama mama ila nakuambia ndugu yangu Baba ni habari nyingine.

Hata kama hana hela. Ila akisema neno tu linatosha kabisa.
 
Unamchukia kwakuwa bado yupo.

Ila akifariki ndio utajutia uamuzi wako.

Tafuta muda utengeneze nae.

Hakuna mtu muhimu kama baba, ingawa feminist wanasema nani kama mama ila nakuambia ndugu yangu Baba ni habari nyingine.

Hata kama hana hela. Ila akisema neno tu linatosha kabisa.
ahsant sana mkuu
 
Unamchukia kwakuwa bado yupo.

Ila akifariki ndio utajutia uamuzi wako.

Tafuta muda utengeneze nae.

Hakuna mtu muhimu kama baba, ingawa feminist wanasema nani kama mama ila nakuambia ndugu yangu Baba ni habari nyingine.

Hata kama hana hela. Ila akisema neno tu linatosha kabisa.

Baba aliyekutelekeza wakati unamuhitaji ana muhimu gani sasa? Apeleke njaa yake hukohuko alikotumia pesa zake
 
Usimchukie bali jitenge naye na maisha aliyokupitisheni liwe funzo bora utakapojaaliwa kupata familia yako
Chuki kama hiyo huzaa kisasi.. Jitajidi uzao wako usirithi visasi
Kudhibiti hasira iliyotokana na maumivu makali ni ngumu mnoo, hiyo hasira ndiyo inayoleta chuki na kisasi.
 
Mimi dingi yangu aliwahi ninyima chakula siku kadhaa na wanakula hapo na mke wake (mama wa kambo). Wanakucheka!!

Niliwahi kuumwa kwa kuzidiwa kabisa nimelala karibu na uwani kwasababu nilikuwa natapika saaana (wakati mzee anatoka bafuni na mkewe ikabidi nimwombe angalau ela niende hosp kucheki maana hali ni mbaya) " kauli aliyoniambia ni kwamba we unayo?'" yaani hio ela nnayo omba mi nnayo?? Ikabidi niseme Sina.. nayeye akajibu Hana pia!!

Niliwahi fukuzwa home, sio mara moja!

All in all mzee wangu (dingi) namkubali sana pamoja na yote..

Nilishaapa sana kwamba haitakuja kutokea nimkubali!! Lakn ndo hivyo akiwa na shida akikucheki tu! Mtu upo tayri uazime ela sehem umtumie (I don't know hii Hali inakuwaje kuwaje)
Naendelea kujifunza kupitia wengine
 
Mimi nawapenda sana wanangu, ila kwa kitu mke wangu alinifanyia mwaka 2013 nikiwa na watoto wawili, ningeweza mtelekeza kama Baba yako alivyofanya ( Kama nisingekuwa na Imani katika Mungu)

Hawa Mama zenu sio malaika, wakati mwingine waache tu wateseke!

Mama yako anakupotezea mda tu, mfariji, ila tafuta Baba yako, atakusaidia sana na kukupa experience ya kiume ngumu aliyopitia kwa Mama yako, hawa wanawake waangalieni hivi hivi, shida sana!
Kwani hao wanawake hawaumizwi na waume zao na wakavumilia ? Mwenzio anasema siwezi acha wanangu wateseke, ila mwanaume mke kamuudhi tena wakati mwingine yeye ndiyo sababu, jibu lake anakimbia nyumbani
 
Back
Top Bottom