Riot inaweza kuwa hata ya mtu mmoja au wawil, funguka. Watu wanasombwa na magari na wengine wametoka toka Mbeya na Iringa mjini halafu unasema kikukndi kidogo? hivi unayaandika haswa haya kwa nia safi kabisa na wala sio kwa kubishana mradi kubisha tu?
Ukatazwe kufanya mkutano, ukafanye kwa nguvu, uambiwe sambaratika ukatae na uanzishe fujo, ukitupiwa vibomu vya machozi na wewe unashambulia kwa mawe kwa dakika 30 halafu useme hiyo siyo riot? Isitoshe wakati huohuo atoke mmoja kwa kujiona yeye ni hodari sana akamvae mkuu wa kikosi? hiyo kama si suicide ni nini?
Ukweli unabaki kuwa ukweli hauchakachuliki!
Tazama picha, wameweka hata kitambaa kinachoonekama mita 200 kikiwataka watawanyike kwa amani na wakikadi serikali itatumia nguvu, hukukiona? sikuwepo lakini hiyo Ilani nimeiona humuhumu JF.
Sawa hawakutawanyika lakini kipigo alicho pata mwandishi wa habari kabla ya bomu ni dhahiri kulikuwa na mpango! Kwa nini hawakumkamata na kumpeleka kalandiga ila wakaamua kumpeleka kuzimu?
Ni wazi kabisa kulikuwa na mpango wa kusingizia cdm wameua mungu mkubwa waandishi wa habari wengine walikuwepo na kuchukua picha na inaonesha wazi kuwa idadi ya watu walio kuwepo hakukuitajika nguvu iliyo tumika!
Na alipomvaa mkuu wa kikosi? au tukuwekee picha hapa?
Zomba naomba nijibu hoja zangu za awali,alafu katika akili ya kawaida tena ya kiasi kidogo unadhani unaweza kumshawishi nani hata kama ni mtoto mdogo kua "polisi" saba walishindwa kumdhibiti mwandishi wa habari mmoja asiye hata na jiwe?hii ni nchi yetu sote,na vijana lazima tuwe na mitazamo chanya juu ya future ya taifa letu,mambo kama haya ni ya kuyakemea,na si ya kuyaletea porojo!
Na alipomvaa mkuu wa kikosi? au tukuwekee picha hapa?
Hawezi kilaza huyo anabwabwaja oh mwandish alikuwa na bomu oh alitaka kumpiga ngumi polisi oh watu walikuw....kungine utagongwa kichwa kwenye jiwe la akili