Nakubali mahakama ya kadhi

Nakubali mahakama ya kadhi

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,320
Reaction score
18,599
Kama kichwa cha habari kilivyoonyesha hapo juu, mimi napenda kutoa ukweli wa moyo wangu leo.
Nakubali waislam waanzishe mahakama ya kadhi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa uwepo wa mahakama hiyo, uwepo wa mahakama ya kadhi utasaidia waislam kufuata sheria zinazoendana na imani yao.
Kila jambo linalowahusu waislam litafanywa bila kutatiza maadili yao.
Pamoja na hayo niliwaza uwepo wa mahakama hiyo bila kuwekwa kwenye katiba ili kuepusha:
1.mambo yanayoweza kuvuruga mshikamano wa raia, kwa kuleta dhana kwa kila mtu kwamba kumbe sisi tuko tofauti sana, hii itaongeza ubaguzi.

2.kuwafanya watu wasio waislam kufikiri kwamba serikali inafungamana na dini flani hapa nchini.

3.watu wasio waislam kufikiri kua mahakama hii ititatumia fedha zinazochangiwa hadi na watu wawasiokua waislamu

4. Watu wasio waislamu wanawaza kua uwepo wa mahakama ya kadhi kutaashiria kua uislam ni sehemu ya dora (serikali).
Kwa mtazamo wangu naomba iwepo ila isiingizwe kwenye katiba.
Wadau tafadhali haya ni mawazo yangu naomba nisiulizwe dini yangu, wala nisipewe matusi kwa sababu ni fikra zangu sio lazima kila mtu awaze kama mimi.
Naomba kuwasilisha.
 
Ni muhimu ikatambulika kikatiba ,ili iwe ya kudumu ndani ya nchi.
 
Mkuu kama umesoma vizuri nimeeleza baadhi ya mambo ninayodhani ni madhara/mitazamo inayoweza kuleta madhara endapo itaingizwa kwenye katiba, sasa ikiwa utaanza kunipa somo la katiba kuitambua jua hayo nayafahamu ila naona upande hasi wa hii kitu kua kwenye katiba.
 
Mimi dhana yangu ni tofauti sana kwani mahakama si itahukumu waislam kwa baadhi ya mambo yakiwemo mirathi,ndoa,wakfu. Haki ni kuiweka kwenye katiba. Ila kutoiweka ni kuendeleza ile dhana ya mfumo kristo na hata wapingao ni wakisto
 
Kwani Tanzania inadini? Tanzania haina dini, ila watanzania wana dini zao, katiba inabadilika ila dini hazibadiliki, kwa hiyo kila dini ijifanyie mambo yake yenyewe na pamoja na waislam.
 
Mimi dhana yangu ni tofauti sana kwani mahakama si itahukumu waislam kwa baadhi ya mambo yakiwemo mirathi,ndoa,wakfu. Haki ni kuiweka kwenye katiba. Ila kutoiweka ni kuendeleza ile dhana ya mfumo kristo na hata wapingao ni wakisto

Mkuu ukinzani uliopo baina ya wakiristo na waislam upo siku zote, mimi nimetoa maoni yangu kama mwananchi sio mkiristo wala sio muislam wala sio mpagani, toa hoja zako kwanini unataka iwepo, faida zake na madhara yake usikimbilie kusema wakiristo wanaipinga.
Karibu tujadili kwa hoja.
 
Ni vizuri serikali ikaiweka ndani ya Katiba then ikaweza kusimamiwa na dola, lakini iwapo Waislamu wenyewe wataianzisha, serikali itakosa uhalali na nguvu ya kuisimamia na Badala ya mambo hayo manne, ya ndoa, mirathi, wakfu na talaka Waislamu wanaweza kuongeza na mambo mengine kwa kusema kuwa hiyo ni sehemu ya Ibada yao na KATIBA INATOA UHURU WA KUABUDU!!!! Je ikifikia hatua hiyo si itakuwa mgogoro mkubwa katika nchi?
 
Nakubaliana na wewe ila kitendo cha katiba kua na mahakama ya kadhi na serikali kuanza kuisimamia kuangalia inafanya nini hiyo itakua ni picha tosha kwamba serikali inafungamana na dini, kumbuka serikali yetu haina dini, hii ni kuepusha migogoro ya kidini na ubaguzi wa kidini.
 
Kama kichwa cha habari kilivyoonyesha hapo juu, mimi napenda kutoa ukweli wa moyo wangu leo.
Nakubali waislam waanzishe mahakama ya kadhi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa uwepo wa mahakama hiyo, uwepo wa mahakama ya kadhi utasaidia waislam kufuata sheria zinazoendana na imani yao.
Kila jambo linalowahusu waislam litafanywa bila kutatiza maadili yao.
Pamoja na hayo niliwaza uwepo wa mahakama hiyo bila kuwekwa kwenye katiba ili kuepusha:
1.mambo yanayoweza kuvuruga mshikamano wa raia, kwa kuleta dhana kwa kila mtu kwamba kumbe sisi tuko tofauti sana, hii itaongeza ubaguzi.

2.kuwafanya watu wasio waislam kufikiri kwamba serikali inafungamana na dini flani hapa nchini.

3.watu wasio waislam kufikiri kua mahakama hii ititatumia fedha zinazochangiwa hadi na watu wawasiokua waislamu

4. Watu wasio waislamu wanawaza kua uwepo wa mahakama ya kadhi kutaashiria kua uislam ni sehemu ya dora (serikali).
Kwa mtazamo wangu naomba iwepo ila isiingizwe kwenye katiba.
Wadau tafadhali haya ni mawazo yangu naomba nisiulizwe dini yangu, wala nisipewe matusi kwa sababu ni fikra zangu sio lazima kila mtu awaze kama mimi.
Naomba kuwasilisha.

mawazo yako ni mazuri.
lalikini kuwekwa kwenye katoba ndio utakua imetekelezwa. ivi jiulize hata chama cha mpira kinatambulika kwenye katiba . wasaniii wana katiba inayowalinda na angalia sintofaham za wana micheZo kuvunja sheria jee wakiwachiwa tuseme katitbu awwe simba na naibu awe yanga tutaeajie nin?
angalia wasanii kila siku wanavyoyumbisha wakat pia wamo kwenye katiba.
overview angalia Watanganyika ni watu wanaojichukulia sheria zao mikononi mwao zidi ya maadui zao na sheria zipo na katiba zipo na bado mauwaji. unyanyasaji uporaji vyote vimeshamiri na hivi tuseme kungekua hakuna chombo cha jatiba na sheria ingekuaje?
 
Mimi dhana yangu ni tofauti sana kwani mahakama si itahukumu waislam kwa baadhi ya mambo yakiwemo mirathi,ndoa,wakfu. Haki ni kuiweka kwenye katiba. Ila kutoiweka ni kuendeleza ile dhana ya mfumo kristo na hata wapingao ni wakisto
Ulitegemea upingwe na nani?Maana hakuna siku ambayo Ukristo utakubaliana na mambo ya Uislamu.Kusema ni mfumo Kristo Je kuna mahakama ya Kristo ndani ya Katiba ya Sasa?Maana kungangana iingizwe kwenye katiba mahakama ya kadhi ni kusema kuwa Waislamu hawajiwezi mpaka wapewe msaada na Katiba,maana yake kutumia dola.Kinachoniacha mdomo wazi ni kuwa pamoja na kufundishwa toka wakiwa wadogo na kukataa kwenda shule ile wasome elimu ya dini bado wanahitaji msaada wa Vyombo vya dola kuwezesha dini kuwepo.Hata ikiruhusiwa kuwepo kwenye katiba mwisho wa siku ni kukaribisha vurugu na shida.Yesu anasema Njooni kwangu nami nitawapumzisha.Itajulikana kuwa YESU ni Mungu au la.
 
[h=2] Nakubali mahakama ya kadhi[/h]
Kama kichwa cha habari kilivyoonyesha hapo juu, mimi napenda kutoa ukweli wa moyo wangu leo.
Nakubali waislam waanzishe mahakama ya kadhi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa uwepo wa mahakama hiyo, uwepo wa mahakama ya kadhi utasaidia waislam kufuata sheria zinazoendana na imani yao.
Kila jambo linalowahusu waislam litafanywa bila kutatiza maadili yao.
Pamoja na hayo niliwaza uwepo wa mahakama hiyo bila kuwekwa kwenye katiba ili kuepusha:
1.mambo yanayoweza kuvuruga mshikamano wa raia, kwa kuleta dhana kwa kila mtu kwamba kumbe sisi tuko tofauti sana, hii itaongeza ubaguzi.

2.kuwafanya watu wasio waislam kufikiri kwamba serikali inafungamana na dini flani hapa nchini.

3.watu wasio waislam kufikiri kua mahakama hii ititatumia fedha zinazochangiwa hadi na watu wawasiokua waislamu

4. Watu wasio waislamu wanawaza kua uwepo wa mahakama ya kadhi kutaashiria kua uislam ni sehemu ya dora (serikali).
Kwa mtazamo wangu naomba iwepo ila isiingizwe kwenye katiba.
Wadau tafadhali haya ni mawazo yangu naomba nisiulizwe dini yangu, wala nisipewe matusi kwa sababu ni fikra zangu sio lazima kila mtu awaze kama mimi.
Naomba kuwasilisha.

Watanzania wenzangu kila kitu kina uhalisia wake.Duniani kote wanadamu wanazo tofauti za kila aina ,lakini pia kuna mambo wanayofanana .Pamoja na hayo yote munaweza kufanana katika jambo fulani na mukakosan kwenye jingine.huu ndio uhalisia wa viumbe wote tulivyoumbwa na Muumba wetu.
Mfano.wa mafanano yetu makuu ni haya.
1.kundi lakiumbe mtu wote tunafanana kama binadamu.
2.Kula,kunywa,na kuenda haja,kulala,furaha na huzuni nk tunafanan.
3.Hisia wete tuna hisia bili tunatofautiana tuu.
4.Kupena au kuchukia na mengi ya kiutu tunafanana
Lakini ukiingia ndani zaidi ya hapo utaona tunatofautiana kimaumbile,sura,utashi,na hata imani zetu za kidini pamoja na kuwa tunaweza tukawa na imani moja kwa kundi fulani mfani Waislamu,lakini kwa undani kila mtu ana upeo wa uamini wake tofauti na mwengine.
Hivi kweli sisi ni wamoja ?
Swali hili linahitaji uangalifu sana,kulijibu,lakini kwa haraka haraka sisi si wamoja.
Wewe ni mkiristo hawa ni waislamu.
Wewe ni mtanganyika na hawa ni wazanzibari.
wewe ni mnywa pombe na mla nguruwe na wale ni wala nyama za watu na vibudu na wengine Vegeterians.
Kwa hiyo basi Taifa linapoandika katiba inayohitajiwa na watu wenye mchanganyiko kama huu,ni lazima iangalie mmambo yanayo tuunganisha wote,na kisha iangalie makundi makubwa, halafu izilinde haki za makundi madogo madogo bila ya kuathiri uhuru wa mtu mmoja mmoja.

KWA MSINGI HUU NDIPO INAPOKUJA HOJA YA MAHKAMA KAMA ZA BIASHARA,ARDHI,KAZI NA ILE YA KADHI ambazo zitayahusu makundi husika tuu.Kufanya hivi ni kurahisihsa utawala na kuwafikia watu wote kwenye makundi yao.
Mbona sijawahipo kusikia kuwa Mahakama za Biashara zikipingwa wakati Kundi la wafanya biashara Tanzania ni dogo tu.
wafanaya kazi nao mahakama yao inagharamiwa na watanzania wote ilhali wengine hata hizo kazi hawana?
Mahakama ya Ardhi ni kwa wale wanaomiliki ardhi tu . nk
ZINDUKA MSOMI MWENZANGU, HIVI KARIBUNI KUTAKUWA NA MAHAKAMA YA WANAWAKE NA WATOTO UNAJUWA HILO.
JEE WATANZANIA WOTE NI WANAWAKE?

lakini kimsingi sisi ni Watanzania kwa umoja wetu ila tunazo tofauti zetu kubwa tuu za kimakundi.hapa umoja wetu ni wa Kiutaifa tuu si wa kidini,wala kikabila.Ndio maana makabila mengi hapa Tanzania yana umoja wao wa kimaendeleo,misiba na majanga.Haina maana wanavunja umoja wa kitaifa bali naamini ndio wanauimarisha,.

Umoja wa kitaifa unaoutaka wewe hauwezekani kwani kharama yake ni kubwa mno kwa kuzikandamiza haki za Imani za dini yenye kundi kubwa nchini.

Mimi dhana yangu ni tofauti sana kwani mahakama si itahukumu waislam kwa baadhi ya mambo yakiwemo mirathi,ndoa,wakfu. Haki ni kuiweka kwenye katiba. Ila kutoiweka ni kuendeleza ile dhana ya mfumo kristo na hata wapingao ni wakisto

Mbona mnamalalamiko ya kike kike wanawake wanadai haki wakisema mfumo dume nyie nanyi mfumo Kristo mh hii mpya ila jua kwamba kichwa ni kichwa tu wala katu hawezi kuwa mkia Teh Teh Teh!.
 
Kwenye nchi isiyofungamana na dini yoyote, kwenye nchi ambayo wananchi wake wana dini tofauti, haki yenye kutoa usuluhishi sawa usiofungamana na dini yoyote ni ile tu ya mahakama ya serikali isiyochagua dini wala kabila. Mahakama hii ndio pekee itakayotenda haki kwa usawa.
 
[h=2] Nakubali mahakama ya kadhi[/h]
Kama kichwa cha habari kilivyoonyesha hapo juu, mimi napenda kutoa ukweli wa moyo wangu leo.
Nakubali waislam waanzishe mahakama ya kadhi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa uwepo wa mahakama hiyo, uwepo wa mahakama ya kadhi utasaidia waislam kufuata sheria zinazoendana na imani yao.
Kila jambo linalowahusu waislam litafanywa bila kutatiza maadili yao.
Pamoja na hayo niliwaza uwepo wa mahakama hiyo bila kuwekwa kwenye katiba ili kuepusha:
1.mambo yanayoweza kuvuruga mshikamano wa raia, kwa kuleta dhana kwa kila mtu kwamba kumbe sisi tuko tofauti sana, hii itaongeza ubaguzi.

2.kuwafanya watu wasio waislam kufikiri kwamba serikali inafungamana na dini flani hapa nchini.

3.watu wasio waislam kufikiri kua mahakama hii ititatumia fedha zinazochangiwa hadi na watu wawasiokua waislamu

4. Watu wasio waislamu wanawaza kua uwepo wa mahakama ya kadhi kutaashiria kua uislam ni sehemu ya dora (serikali).
Kwa mtazamo wangu naomba iwepo ila isiingizwe kwenye katiba.
Wadau tafadhali haya ni mawazo yangu naomba nisiulizwe dini yangu, wala nisipewe matusi kwa sababu ni fikra zangu sio lazima kila mtu awaze kama mimi.
Naomba kuwasilisha.

Watanzania wenzangu kila kitu kina uhalisia wake.Duniani kote wanadamu wanazo tofauti za kila aina ,lakini pia kuna mambo wanayofanana .Pamoja na hayo yote munaweza kufanana katika jambo fulani na mukakosan kwenye jingine.huu ndio uhalisia wa viumbe wote tulivyoumbwa na Muumba wetu.
Mfano.wa mafanano yetu makuu ni haya.
1.kundi lakiumbe mtu wote tunafanana kama binadamu.
2.Kula,kunywa,na kuenda haja,kulala,furaha na huzuni nk tunafanan.
3.Hisia wete tuna hisia bili tunatofautiana tuu.
4.Kupena au kuchukia na mengi ya kiutu tunafanana
Lakini ukiingia ndani zaidi ya hapo utaona tunatofautiana kimaumbile,sura,utashi,na hata imani zetu za kidini pamoja na kuwa tunaweza tukawa na imani moja kwa kundi fulani mfani Waislamu,lakini kwa undani kila mtu ana upeo wa uamini wake tofauti na mwengine.
Hivi kweli sisi ni wamoja ?
Swali hili linahitaji uangalifu sana,kulijibu,lakini kwa haraka haraka sisi si wamoja.
Wewe ni mkiristo hawa ni waislamu.
Wewe ni mtanganyika na hawa ni wazanzibari.
wewe ni mnywa pombe na mla nguruwe na wale ni wala nyama za watu na vibudu na wengine Vegeterians.
Kwa hiyo basi Taifa linapoandika katiba inayohitajiwa na watu wenye mchanganyiko kama huu,ni lazima iangalie mmambo yanayo tuunganisha wote,na kisha iangalie makundi makubwa, halafu izilinde haki za makundi madogo madogo bila ya kuathiri uhuru wa mtu mmoja mmoja.

KWA MSINGI HUU NDIPO INAPOKUJA HOJA YA MAHKAMA KAMA ZA BIASHARA,ARDHI,KAZI NA ILE YA KADHI ambazo zitayahusu makundi husika tuu.Kufanya hivi ni kurahisihsa utawala na kuwafikia watu wote kwenye makundi yao.
Mbona sijawahipo kusikia kuwa Mahakama za Biashara zikipingwa wakati Kundi la wafanya biashara Tanzania ni dogo tu.
wafanaya kazi nao mahakama yao inagharamiwa na watanzania wote ilhali wengine hata hizo kazi hawana?
Mahakama ya Ardhi ni kwa wale wanaomiliki ardhi tu . nk
ZINDUKA MSOMI MWENZANGU, HIVI KARIBUNI KUTAKUWA NA MAHAKAMA YA WANAWAKE NA WATOTO UNAJUWA HILO.
JEE WATANZANIA WOTE NI WANAWAKE?

lakini kimsingi sisi ni Watanzania kwa umoja wetu ila tunazo tofauti zetu kubwa tuu za kimakundi.hapa umoja wetu ni wa Kiutaifa tuu si wa kidini,wala kikabila.Ndio maana makabila mengi hapa Tanzania yana umoja wao wa kimaendeleo,misiba na majanga.Haina maana wanavunja umoja wa kitaifa bali naamini ndio wanauimarisha,.

Umoja wa kitaifa unaoutaka wewe hauwezekani kwani kharama yake ni kubwa mno kwa kuzikandamiza haki za Imani za dini yenye kundi kubwa nchini.

Usilinganishe mahakama za aldhi,biashara na kazi na mahakama ya kadhi. Dini,rangi,kabila ni vitu tofauti na hizo sekta nilizotaja hapo juu!
 
Mimi dhana yangu ni tofauti sana kwani mahakama si itahukumu waislam kwa baadhi ya mambo yakiwemo mirathi,ndoa,wakfu. Haki ni kuiweka kwenye katiba. Ila kutoiweka ni kuendeleza ile dhana ya mfumo kristo na hata wapingao ni wakisto

hivi mnadhani sisi wahindu hatuna taratibu zetu kwenye hinduism?tukitaka tuziweke kwenye katiba itakuwa vipi?sisi wapagani je?mnadhani hatuna taratibu zetu?tukitaka zionekane kwenye katiba je?sisi moonists,sunists,pegans,traditionalists,etc etc .tukitaka kila dini ionekane kwenye katiba tutafika kweli?MFUMO KRISTU UKO WAPI?BADALA YA WATU WAACHE KWENDA SHULE KUSOMA ILI WAPATE NAFASI YA KUAJIRIWA WANASOMA MADRASA.WASIPOAJIRIWA ETI MFUMO KRISTU.WAKRISTU WANAAJIRIWA WENGI KULIKO WAISLAMU.DOES THIS BRING SENSE????????????
 
Battawi unanishangaza sana kwa upeo wako unaokutuma kulinganisha shughuli za kibiashara, kilimo na imani za watu.
Hivi ni sahihi kwamba jambo la imani linaweza kua sawa na shughuli za kiuchumi?
Kama ziko sawa basi naomba nipewe takwimu za uzalishaji wa kila mwaka katika sekta za kidini kama tunavyopokea takwimu za kilimo na biashara, pia tunaomba wafanya biashara na wakulima waachwe bila sheria kuwaangalia tuone uchumi wetu utakuaje?
Jambo la imani ya mtu liwepo tu ila si vyema liwe kwenye katiba yetu kwa sababu hiyo katiba ni mali ya watu wote sio mali ya dini fulani kama watu wataelewa maana ya ''serikali yetu haina dini'' basi hata madai mengine kama ya mahakama ya kadhi tutayaacha na kufanya mambo ya maana
 
Angalia mifano hai ya mahakama ya kadhi. Tuangalie baadhi ya hukumu zake za "haki" kwa wananchi kisha tujiulize kama tuiruhusu ak la. Angalia hapa.

LiveLeak-dot-com-4eb_1407196993-3_14071971871.jpg.resized1.jpg
 
Imefika wakati na sisi tuwe na mahakama zinazoendeshwa na wachungaji. Hakuna namna nyingine, mahakama za misikitini kulipiwa mishahara na serikali!!!! Watoto wanakaa chini, madawati hakuna, vitabu hakuna, waalimu hawalipwa stahili zao hivi ccm inataka kutupeleka wapi???? Hakika ccm ni Ebola.
 
Back
Top Bottom