VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kwa nchini kwetu Tanzania, kuwa mtumishi wa umma ni kuonesha uzalendo mkubwa. Hii ni kwakuwa, watumishi wa umma Tanzania wanalipwa mishahara kidogo kulinganisha na watumishi wa sekta binafsi.
Watumishi wa umma ni wazalendo kwelikweli. Hawarudishwi nyuma na mishahara na marupurupu yao kiduchu. Wanaendelea kujenga Taifa lao kupitia utumishi wao. Siyo siri, watumishi wa umma huishi kwa posho na mafunzo.
Watumishi wa umma huwa na amani moyoni wanapokuwa na 'viposho' vya hapa na pale. Hii ni kwakuwa, mishahara yao humezwa na mikopo,kodi za Serikali, michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii,michango ya afya, michango ya vyama vya wafanyakazi na kadhalika.
Mtumishi anapopata 'kasafari' ka mafunzo ndani au nje ya Tanzania, huyasahau maumivu yake na kusonga mbele kuelekea kwenye kilele cha mafanikio yake. Kufutafuta kila posho au mafunzo kwa mtumishi wa umma ni kumuumiza maumivu yasiyoweza kupozwa.
Posho na mafunzo (visafarisafari) humpa chachu ya utendaji mtumishi wa umma. Mtumishi wa umma hastahili kuishi kama 'shetani'!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam