Nakerwa sana na tabia hii kwa mafundi magari

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
999
Nampelekea fundi Kigari changu kikiwa kusafii ila baada ya yeye kumaliza kutengeneza kitu chochote unakuta imejaa gress kila eneo mpka kwenye Viti,kwahiyo naingia tena ghalama yaisafisha.

Lakini kingine ni pale anapotaka kuinua gari juu kwa kutumia jeck, wazungu wameweka sehemu Maalum za kuweka Jeck sio kila eneo ni kuweka tu mwishowe kuna sehemu kwenye ukingo wa chini zinabonyea, na hata kama Gari jipya lakini linaonekana la mwaka 47.

Zaidi sana ninapo Peleka Gari langu kwenye Garage fulani maana yake kuna fundi pale namwamini ila utakuta kuwapa wanafunzi wajifunzie kwenye hiyo gari na wanakata bolt nyingi sana kule chini.

Wewe kiongozi unakwelwa na nini kwa mafundi wetu unapo peleka Kigari chako?
 
Nakelwa napopeleka gari mafuta yakiwa nusu tank lakinj nakabidhiwa gari ikiwa na mafuta robo tank. Akishamaliza kutengeneza anaanza kupiga misele anayoijua yeye.mpaka ahakikishe gauge imeshuka. harafu anakuchaji hela ya ufundi.
 
Tutumie uzi huu kuwapasha habari mafundi wetu ili wajue kuna siku tutawalipisha kama sio kuosha gari kwa ghalama zake
 
Sio siri pumbavu sana hawa.

Kuna fundi namuamini sana lkn nimempelekea gari yangu kama mara 2 hv.
Kila napoenda kuichukua naikuta ndani kama tabata dampo.
Sijampelekea tena afe njaa tu pumbuwavu zake
 
Sio siri pumbavu sana hawa.

Kuna fundi namuamini sana lkn nimempelekea gari yangu kama mara 2 hv.
Kila napoenda kuichukua naikuta ndani kama tabata dampo.
Sijampelekea tena afe njaa tu pumbuwavu zake
Lakini pia ilipaswa kumwambia ulivyo chukia mkuu,maana kwa njia ya ku mwambia alivyo fanya kwa gari yako atajifunza kwa wengine
 
Hii tabia mwanzoni ilikua inanitesa sana nikawa na hama hama garage tuu ila nikakata shauri mi nikawa nawambiaga nayeye alikua ananipa shit ila sa hivi ameelewa saana tu maana tumezoeana pia...
(Ila JF hatari saana daah yani naweza nikawa nimeandika hivi halaf kumbe sina Hata gari wala nini) Thank u fake ID
 
Mafundi gari wanatabia mmoja ukiwa nae pale pale gari litatengenezwa kwa gharama nafuu... Ukimuachia gari ukaondoka utapigiwa simu na kutajiwa msururu wa spare za kubadilisha mpaka utashangaa...
 
Mafundi gari wanatabia mmoja ukiwa nae pale pale gari litatengenezwa kwa gharama nafuu... Ukimuachia gari ukaondoka utapigiwa simu na kutajiwa msururu wa spare za kubadilisha mpaka utashangaa...
Zote hizo nililipia kelo, ila sasa tujipange kuwalipisha ili kuibadilisha tabia ,haiwezekani gari inatengenezwa kitu one week kimekufa, ila kubwa kuliko yote swala la kuchafua gari hii mimi kwakweli inanikera sana Bandugu
 
Back
Top Bottom