Mimtamu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 368
- 105
habari zenu wana MMU
Najuta kusema uongo na tamaa yangu ya mapenzi, mimi ni kijana wa kiume sijaoa nafanya kazi na kampuni fulani hapa rocky city. Mwezi januari nilihama sehemu niliyokuwa nimepanga nikapata chumba sehemu nyingine.
Nilipohamia mama mwenye nyumba anaishi na mdogo wake wa kike akaanza kuwa karibu na mimi sasa kidume nikarusha ndoano binti kakubari kutoa gegedo, baadaye dada mtu kainasa habari kuwa nakula mzigo kwa mdogo wake ikabidi amwambie mdogo wake anipe taarifa kuwa jion nimuone dada yake ana maongezi na mimi.
Maswali niliyokutana nayo katika kile kikao kati yangu na dada wa yule binti ni:
majibu niliyompa ni kwamba siwezi kujibu maswali yako haraka na mapema mno.
- mdogo wangu nimemuuliza akasema ukweli kwamba una mahusiano naye, je mpango wako ni upi sasa,unakula mzigo na kuacha au una malengo ya kuoa?
- Je huna mke au mpenzi mwingine?
Lakin kinachonifanya nijute ni kuwa mwezi June 2014 mpenzi wangu anakuja toka Dar kuja kuishi kwangu akiwa anafanya field na siwezi kuhama ile sehemu coz nimelipa kodi ya mwaka mzima na masharti ya mkataba wa pango ni kwamba mpangaji akihama kabla ya muda kuisha hela hairudishwi.
Kuepusha shari kati ya mama mwenye nyumba, mdogo wake(gegedo langu la sasa) na mpenzi wangu wa ukweli Nifanye? USHAURI WAKO NI MUHIMU NA SIYO MATUSI
Pole sana kaka yangu. Kwanza kabisa kama ulivyosema mwenyewe kuwa huyo binti ilikuwa tamaa tu na ni hakika kuwa hujawahi kumpenda.
Sasa kwa ushauri mzuri tu ili uuthibitishie moyo wako kuwa wewe ni real gent..weka kikao na huyo binti kisha mueleze ukweli then akidai kuwa kwanini ulimdanganya wewe mwambie kuwa hata yeye hukumuamini, ila mtayaongea zaidi baada ya huyo binti kumaliza field na kusepa.
Hapo atakuwa hana ujanja then maamuzi mengine utabaki nayo wewe.. ILA NA UKOME