The Green Village
Senior Member
- Aug 30, 2013
- 170
- 73
wapi imeandikwa kuwa kila mwenye elimu ni lazima aajiriwe?Habari zenu ndugu,
Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.
Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.
Tatizo la ajira nchini ni kubwa ila mimi nitapingana na mawazo ya wadau kidogo,mimi nimebaahatika kuwafanyia usahili zaidi ya watanzania elfu mbili mpaka sasa na nimegundua kuwa kuna tatizo kubwa katika mifumo yetu ya elimu,unakuta mtu ana masters lakini ukimuuliza maswali rahisi tu yanayolenga kupima uwezo wake binafsi inasikitisha,wengine lugha ya kiingereza ambayo ni msingi kwa kampuni nyingi za binafsi ni matatizo
My take is ukikutana na mtu aliyeomba kazi sehemu zaidi ya tano bila kupata ana matatizo na wewe unaejuta unaweza kuwa mmoja wao.
Mtu kubali kuanza chini ujenge uzoefu na utagrow in three years katika level unayotaka nina mifano hai kabisa,kama huna habari makampuni yanatumia mamilioni ya shilingi kwenda nchi za nje kutafuta watanzania wanaosoma huko kuja kufanya kazi tanzania na eanachukua fresh graduates tusilalamike bila sababu
ua in my mind,,,,,because being deep into it will make u competent in a way u can employ your selfMimi huwa ninashangaa kidogo, hivi lengo halisi la kupata elimu(kusoma)huwa ni kuajiriwa?
Mtu anajuta kusoma hadi chuo kikuu kisa hajaajiriwa!!??
Eti mkuu, au mimi fikra zangu ndio zimepotoka, watu wa karibu yangu huwa wananishangaa sana nikisema kuwa nitasoma fani, sio kwa kuangalia kuwa fani husika ina soko, ila kwa sababu ninaipenda hiyo kitu, I want to be deep about it and I will do it regardless of payments.
Sikubaliani na wewe hata kidogo...kazi haipimwi kwa mtu kujua kiingereza na kama alikua hajui kiingereza alifikaje chuo...na kama kiingereza ndio kujua kazi wachina hawa wasingepata tenders na ajira nchi za kiafrika kwani asilimia 90 wanazungumza kichina, na pia ili suala halipingiki kazi ni kuhonga au kua na God Father hapa bongo au tuambie hao watu uliobahatika kuwafanyia interview hakuna wengine umeambiwa na mkubwa wako hawa wape kazi ingali hata kabla kukutana nao wewe, UONGOOO!??Tusidanganyane bwana wee mpe mtu moyo wa kuendelea kutafuta ila usimwambie lugha ya kiingereza ndio tatizo mie nakataa mara 800!!!
Eti mkuu, au mimi fikra zangu ndio zimepotoka, watu wa karibu yangu huwa wananishangaa sana nikisema kuwa nitasoma fani, sio kwa kuangalia kuwa fani husika ina soko, ila kwa sababu ninaipenda hiyo kitu, I want to be deep about it and I will do it regardless of payments.
Usijali kuwa mpole na mwamini Mungu nae atakuthibitisha kwa kazi itakayokushangaza itakayokufanya usahau machungu na kukata tamaa kwingi ulikopitia. Mungu na akufungulie mlango wake mrKukata tamaa ni vibaya sn mkuu,i understand ur situation..nilikuwa km ww nilipokaa kitaa miaka mitatu bila kazi,lkn sikukata tamaa,niliendelea kukomaa huku nikimuomba Mungu.
utakuja kupata kazi tu,mi nilipata kazi ambazo hata ndugu zangu wanashangaa nilipata vp.sikuwa na god faza wala nn ni msaada wa Mungu tu.mpk sasa nimefanya kazi km sehem tatu tofauti,mwanzo nilikuwa nataman kaz yoyote ile lkn sasa nacheck maslah.so nawe utapata tu mkuu,muamin Mungu,kama alikupa degree bas na kaz atakupa...
Tatizo mnasoma kozi kwa kufuata mkumbo bila kuangalia soko la ajira.Mara BBA,HR,Socilogy n.k.Ungesoma education ungejikuta sasa hivi unapiga mluzi tu.Somo zuri sana wengine wajifunze
Wewe umepita tu shule ila hujaelimika! Akili yako haina tofauti na Gari ya kwanza iliyotengenezwa na Henry Ford ambayo haikuwa na gear ya rivasi (reverse)!
Mimi huwa ninashangaa kidogo, hivi lengo halisi la kupata elimu(kusoma)huwa ni kuajiriwa?
Mtu anajuta kusoma hadi chuo kikuu kisa hajaajiriwa!!??
Eti mkuu, au mimi fikra zangu ndio zimepotoka, watu wa karibu yangu huwa wananishangaa sana nikisema kuwa nitasoma fani, sio kwa kuangalia kuwa fani husika ina soko, ila kwa sababu ninaipenda hiyo kitu, I want to be deep about it and I will do it regardless of payments.
Umenikumbusha wakati nataka kwenda chuo, niligombana sana na mzee wangu, alitaka nisome electrical engineering sababu inalipa, nikasema sisomi kitu ambacho sikipendi ng'o. Nikaenda kuibuka na kozi hata hawakuwa wanaelewa nitaajiriwa wapi, lakini ndio kitu nilikuwa napenda, sijawahi regret aisee.
Hakuna kitu kizuri kama kusoma kitu unachopenda, hata darasani huhangaiki sana na mambo yakiwa magumu hulaumu mtu, kiroho safi.
Teh teh teh!!!wewe umenena, eti mtu anapost humu kuuliza "nisomee kozi gani kwa matokeo haya?' yani yeye hana ambition yoyote anataka watu wa jf ndo wamchagulie, mi mwanangu wa miaka nane tayari anaijua ndoto yake, he wants to become a president... lol.
Husomei unachukua tu!!!?Siku hizi kuna kuchukua hakuna kusomea