Najuta Kusoma hadi chuo Kikuu

Najuta Kusoma hadi chuo Kikuu

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
655
Habari zenu ndugu,

Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.

Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma HR ambazo hazina ukweli wowote.

Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.

Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?

Kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupoteza pesa na muda wangu.

Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.

Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.
 
Baadhi ya sifa za mtu mwenye stress, ni kujuta, kuwa na mtazamo hasi, na kuangalia mambo ya nyuma. Aliyekuambia ukifika University utapata kazi baada ya wiki moja ni nani? Unapotafuta kazi ya kwanza omba kazi yoyote, hata kuwasaidia watu wanaoreseat masomo uliyosoma shule, ili upate nauli za kuzungukia unapoendelea kutafuta kazi. Ukishapata kazi ya kushikiza, kisha uendelee kutafuta kazi nyingine. Jifunze pia kuwa mvumilivu, kukata tamaa sio sifa za mtu mwenye nia ya kuendelea!
 
Habari zenu ndugu,

Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.
Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.

Elimu yako imekufundisha nini kuhusu kubadilika kwa mujibu wa mazingira, kurekebisha makosa, kujiajiri na kujitegemea?

Umesomea nini?
 
Mtu kama huyu msubiri apate kazi...waja wa Allah ambao ni wanyonge kwake hua hawana thamani tena...Tatizo la Vijana wetu..wanafikiri ukimaliza chuo wewe ndo kila kitu....jaribu kutafuta kazi za kujitolea japo miezi mitatu na baadae unaweza kuingiza hizo kazi katika CV yako....hujasema umemaliza taaluma gani ili tukawza kukushauri vizuri
 
Baadhi ya sifa za mtu mwenye stress, ni kujuta, kuwa na mtazamo hasi, na kuangalia mambo ya nyuma. Aliyekuambia ukifika University utapata kazi baada ya wiki moja ni nani? Unapotafuta kazi ya kwanza omba kazi yoyote, hata kuwasaidia watu wanaoreseat masomo uliyosoma shule, ili upate nauli za kuzungukia unapoendelea kutafuta kazi. Ukishapata kazi ya kushikiza, kisha uendelee kutafuta kazi nyingine. Jifunze pia kuwa mvumilivu, kukata tamaa sio sifa za mtu mwenye nia ya kuendelea!
Ushauri uliokwenda shule..uzingatie utafika mbali
 
Usichoke na usijute Kwa kuipata hiyo elimu maana haikua Kwa ajili ya kukupa kazi nzuri na mshahara mkubwa tu,bali ilitakiwa kukupa ufahamu na uwezo wa kupambana na changamoto za maisha.Kwanza nakushauri uweke hadharani fani ulosomea,chuo na mahali unapoishi ili upate msaada Kwa wanajamii.Jipe ujasiri wa kuthubutu kufanya kazi za ujasiliamali hata Kwa mtaji mdogo nje ya taaluma yako na pia kua karibu na watu wenye fani kama yako ambao tayari wamefanikiwa.Naamini Mwenyezimungu ameandaa kitu kikubwa Kwa ajili yako kama utakua mvumilivu na Mwaminifu.
 
habari zenu ndugu,

ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi mungu tu kwakweli.
Eeeh mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.
unajuta mwenyewe kusoma chuo kikuu, mi sina kazi bado ila najivunia sana kufika chuo. Anyhow, hatukusoma mpaka chuo kikuu ili tukimaliza tukaajiriwe, suala la ajira baada ya kusoma ni moja tu ya faida ya kusoma.... "acha kujutia upuuzi wewe na kama majuto yako unayaona yana nguvu sana usingeandika hii mada bali ungeenda kuvichoma moto vyeti vya chuo kikuu"...
 
Cha msingi sio kujilaumu cha msingi ni kujiraumu kozi uliyosoma ndo haikuwa sahihi sema kozi gan umesoma watu wakusaidie unaweza kuanza kwa kujitolea kama casual labour kwa kuanzia
 
Tatizo mnasoma kozi kwa kufuata mkumbo bila kuangalia soko la ajira.Mara BBA,HR,Socilogy n.k.Ungesoma education ungejikuta sasa hivi unapiga mluzi tu.Somo zuri sana wengine wajifunze
 
Kwani lazima uajiriwe! Acha kulalamika jipange tu utatoka,
Na elimu ynyw ya siku hizi kazi kweli kweli! Waliomaofisini watathibisha hili, mtu anamaliza degree Akiandika CV ni kichekesho.
 
Habari zenu ndugu,

Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.
Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.

Pole sana Mbishi, usijutie kilicho pita hata kidogo, ila kinacho hitajika ni kujipanga kwa kutumia elimu yako uliyo ipata kuweza kufanya shuhuri yoyote upate kipato cha kujikim. Mfano mie nina elimu ya chuo kikuu kwa sasa nimejiajiri kwenye bodaboda ninapata pesa nzuri na ninaiheshim kazi yangu na nimejenga network na watu mbalimbali ambao wamevutiwa na style yangu na kuniahidi mengi na mafanikio nimeanza kuyaona. Usikate tamaaa. Kuwa mmbishi wa ukweli
 
Habari zenu ndugu,

Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.
Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.

na siku ukipata kazi ukumbuke kuja kusema hapa unavokula raha
 
Tatizo la ajira nchini ni kubwa ila mimi nitapingana na mawazo ya wadau kidogo,mimi nimebaahatika kuwafanyia usahili zaidi ya watanzania elfu mbili mpaka sasa na nimegundua kuwa kuna tatizo kubwa katika mifumo yetu ya elimu,unakuta mtu ana masters lakini ukimuuliza maswali rahisi tu yanayolenga kupima uwezo wake binafsi inasikitisha,wengine lugha ya kiingereza ambayo ni msingi kwa kampuni nyingi za binafsi ni matatizo
My take is ukikutana na mtu aliyeomba kazi sehemu zaidi ya tano bila kupata ana matatizo na wewe unaejuta unaweza kuwa mmoja wao.
Mtu kubali kuanza chini ujenge uzoefu na utagrow in three years katika level unayotaka nina mifano hai kabisa,kama huna habari makampuni yanatumia mamilioni ya shilingi kwenda nchi za nje kutafuta watanzania wanaosoma huko kuja kufanya kazi tanzania na eanachukua fresh graduates tusilalamike bila sababu
 
Tatizo mnasoma kozi kwa kufuata mkumbo bila kuangalia soko la ajira.Mara BBA,HR,Socilogy n.k.Ungesoma education ungejikuta sasa hivi unapiga mluzi tu.Somo zuri sana wengine wajifunze
Kwa hiyo unawashauri wote wasome BED? Kwanini hizo kozi ambazo umezisema hazina soko la ajira bado zafundishwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom