Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 30,165
- 41,906
DuhView attachment 2603749
Mwaka jana niliazisha uhusiano na binti fulani, ambaye kwa kweli nilimpenda na kuvutiwa naye sana. Aliniambia ana mtoto mmoja wa kiume, 6 yrs. Kwa asili mimi sio mtu wa kuhukumu watu kwa kufuata tu hisia za wengine, imani au dhana. Mf muda mrefu nimekuwa nikisikia kuwa single mother ni mke wa mtu, lakini binafsi mama yangu mzazi alikuwa single mother, na wameishi na mzee wangu hadi kuzeeshana na ndoa yenye amani sana, so nikajipa imani, kutokana na imani yangu kuwa, watu huwa ni waovu/wema wao wenyewe wala sio kutokana na kundi lao, nikasema acha niingie kwenye mahusiano. Na nilikuwa na plan ndefu sana na yule mwanamke. Mzee wangu nilimshirikisha, jibu lake likawa; kuwa makini na wanawake waliozaa na wanaume wao bado wako hai, wanawake aina ya mama yako ni wachache sana, pia hii generation yenu ni tofauti na yetu. Basi, nikaamua kujilipua.
Miezi miwili ya mwanzo ilikuwa mizuri sana. Kwangu mimi mapenzi ni imani, imani huleta uhuru na amani kwenye mapenzi na kunifanya nifanye chochote kwa mwanamke wangu. Baada ya muda nikaanza ona mapicha picha mengi sana. Mzazi mwenzake ikawa ni kero na kikwazo. Na mambo mengi mwanamke anayakingia kifua.
Last straw:
Mwanamke akaniambia wako kwenye kikao cha kutengenishwa na mzazi mwenzie kwa dada yake (Shemeji yangu), shemeji kumpigia akasema ni kweli, kuwa na amani shemeji, nataka niwaondolee kikwazo. Nikawa na maswali mengi haya make sense. Basu, hiyo ilikuwa ni mida ya saa 10. Kufika saa 1 nampigia simu kuwa niko sehemu fulani, ukitoka nikute tupate msosi wa jioni pamoja. Akasema poa. Mida ya saa 2 hadi saa 4 nampigia simpati. Kwa kweli, nilipata mawazo na uchungu sana. Basi, nikaenda piga mtungi, hadi saa 8 nikarudi lala. Mwanamke anakuja nitafuta saa 5 asubuhi kuwa baada ya kikao, wakaenda kulala na kupata kinywaji, sasa akalewa sana. Sikumjibu msg. Maana nilikuwa nina hasira. Basi mida jioni nikampigia simu ikaita, bila majibu. Usiku haipatikani. Kwa wiki nzima ikawa simu ikipigwa mida haipatikani, mida inapatikana. Mkionana ni kwa tabu. Ili ndio wiki ngumu zaidi niliyowahi ipitia kwenye mapenzi. Baada ya hapo mwanamke akawa panctual na mimi.
Nikafanya upelelezi wangu, nikagundua mzazi mwenzie alikuwepo mjini. Taa nyekundu, ikasema huyu tutakuwa Polyandry. Kilichokuja niumiza zaidi, niligundua kuna hela aliniomba ili aweze kucover gap kazini, kumbe alikuwa amemkopea huyo jamaa yake. Nikaona, bora niumie sasa kumuacha ila sio kuishi maisha ya kipuuzi.. Eva alinifanya niamini mwanamke aliyezaa, sio wa kuoa.
Siku hizi ni mchepuko tu. Nikiwa na hamu zangu namtafuta, basi.
Aiseee