Najuta kuoa mwanamke mlokole

Too much of anything is harmful, hta dini. "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
 

hivi ulitaka stress kama hii haimalizie wap kama si jf? Walokole malaya hadi wazazi washakuwa chizi itakuwaje mke atelekeze mtoto mdogo ivo kisa kanisani? Sote tunampenda mungu kama aliona mme wake sio hawataendana ilibidi aolewe na walokole wenzake.

Ebu amchalaze. Tena ulisahau kabla hajamchalaza ilibidi achepuke siku mbili alale ukoooo mke atikoka kanisani akute mme hayupo tuone. Loh shameless woman
 

Huu ushauri ni mzuri saana..


We jamaa uuzingatie huu
 
Haya yote ni kwa sababu unamuwaza Rachel

Ndoa unajua maana yake wewe?
 
Huyo kashajifunza ilo si kosa hata ingawa alilifanya adi likaonekana ni kosa usimwache huyo ndo mkeo. na uko alipokua amegundua alpokua anakosea kwaiyo kama kaja muulize tu swali moja je ameona mapungufu? kama ameona mrudishe home make ni heri huyo ambae umemjua kuliko ambae utaanza kutaka kumjua.
 
Ukioa tena unafanya dhambi ya kuzini kwa mujibu wa bible,lakini pia usi "generalize"wapo wadada wengi walokole wanaojua wajibu wao na ambao wana hekima ya maisha tena mikono yao ni salama kuliko wale wa misri
 
Kwanza umenifurahisha ulipomjumlisha na shemeji kwenye kichapo.good huo ndio uanaume.

Harafu muache akaolewe na kanisa maana Hanna namna.
 
Mkuu matatizo yako na wife ni makubwa lakini siwezi ungana na wewe mkono katika swala zima la kumpiga mwanamke, nashangaa watu hawaiongelei hili, Hivi we mtu mzima kweli unampiga mke wako hadi anazimia? Chunga sana utaletewa kesi ya mauaji siku moja, unamgusa kidogo tu mwanamke wa watu anakufa moja kwa moja.

Kwanza achana na kumpiga mke wako unaonekana mgomvi sana, mimi lawama zangu zinaenda kwako na si kwa mke wako, sababu umeshindwa kumcontrol, hakuna kitu rahisi kama kumcontrol mwanamke sijui watu hua mnashindwa vipi, jaribu kucheza na psychology yake tu, kupunguza frequency za kwenda kanisani its very possible na ni kitu rahisi sana, tatizo tabia yako inaonekana ya kigomvi sana, kumbadilisha akili mwanamke kama huyo itakutoa jasho
 
Sredi zingine unajikuta unacheka badala ya kusikitika.

Stoo......kutenguliwa mbavu... Oooh Rachel.

Lol
 
Maisha twenyewe tufupi utu; usikubali kabisa mtu akuties stress. Hatujaletwa duniani kupata tabu bana. Usimrudie, itakugharimu sana. Akirudi atapambana akubadilishe. Nawe unaonekana nunda, hautabadilika. Utampiga tena akufie bure; maskini hautaweza hata kupost hapa maana utakua unanyea debe segerea huko. Mwaambie aende tu...aongeze maombi atapata mwenzake anayependa hiyo ratiba na wakaishi kwa furaha milele yao yote.
 
ukweli lazima usemwe, kuna mmoja nilikutana naye tulipishana kama hatujuani, alivaa soksi imembana hatari wakati mwanzo alikuwa anazipiga vvita na kupondea, shame on them walokole!

Kuna mlokole nilisoma nae chuo tukiwa hostel tunatoka anavaa kimini na kanga,
Tukifika kwenye usafiri anaficha kanga,
Ila akiingia darasani ni mwendo wa charanga na Magauni..
Kiukweli nilikua namuambia tu aache unafiki maanake ulokole si kumridhisha binaadamu Bali Mungu pekee!
 
Vioja haviishi. Yaan kiukwel hapo huna mke. Anamwachisha mtoto na miez sita na wazazi wanamuunga mkono? Too bad! Hajitambui na hayuko tayari kibadilika kwasabababu kwanza anaburuzwa na ndg zake. Maandiko yanasema mke na mume wataambatana na kuwa kitu kimoja. Sasa huyo kakuachia housegerl akulelee mtoto maanake anataka huyohuyo housegerl akupe unyumba alafu mwisho wa siku atalalamika. Jaman wanaopata bahati za kuolewa wanazichezea.
 

wanawake katika kutetea upumbavu wao
 
Kweli mwanamke mpumbavu huvunja nyumba kwa mikono yake menyewe. Achn na huyo mama kwani hakufai na pia adabu hana, m'mke mwenye hekima, heshima na busara kwa mumewe anapoambiwa jambo fulan acha bas anapaswa kuacha hrka.. Na km hujaridhika na amri yake ukiwa faragha mueleweshe taratibu kwa upole kuwa unaomba jambo fulan uendelee kulifanya na km mpk hapo imeshindikana basi ni uliache kabsa.Ila kutaka kujifanya kweny nyumba eti vichwa vimelingana bas utaumia wew utamuacha yeye. Be obedient to your man
 

Mkuu kwanza nakushukuru kwa kujitokeza na kuomba msaada wa mawazo. Inaonesha ni jinsi gani ulivyo muungwana.
Nakupa pole kwa yaliyotokea. Kwa kiasi kikubwa kuna makosa ya kimaarifa ambayo mkeo anaonekana kuyakosa. Kushinda kanisani sio kujua neno la Mungu. Sitaki kuwashutumu wala kuwatukana ila kuna tatizo la kimsingi la ukosefu wa maarifa ya neno la Mungu hususani kwa mkeo. Milipo highlight humo na kubold nataka ni kushauri umsamehe mkeo na kumkubalia arudi nyumbani isipokuwa kwa masharti ya msingi kabisa. Kwanza, we ni muungwana sana kwa jinsi unavyoonekana uko tayari walau kumpa fursa ya siku kadha wa kadha za kwenda kanisani. Kaa nae na umweleze kinagaubaga kuwa akitaka kurudi awe tayari kufuata ratiba mpya utakayompa. Pili awe tayari kuachana na ushauri wa wazazi wake linapokuja suala la ndoa yenu.
Biblia yenyewe iko makini inaposema mke na mume wataambatana na kuwa kitu kimoja. Wakwe zako wanafanya kosa kubwa sana kuingilia sheria za nyumba yako. Kingine cha msingi awe tayari kuwaambia wazazi wake kuwa hataki kuingiliwa kwenye ndoa yenu. Hebu tuanzie hapo kwanza halafu urudi unipe mlishonyuma kwa sababu nna mengi ya kunena nawe
 

Yeye mleta mada hana akili angekuwa na akili wala asingetumia nguvu. Mwanamke ni kiumbe rahisi sana kukibadilisha nashangaa mleta mada anampiga zaidi ya nara moja na anaona habadiliki bado anampiga wala hajiulizi shida ni nini na kipigo habadiliki yaani hii dunia ni heri unyimwe mali lakini upewe akili.
 
Nakupongeza sana kwa maamuzi uliyochukua ya kuwachapa wote wawili. Haya mambo mengine ni kupeana stress tu. Aende kanisani kwa kiasi na isiwe too much. Hakuna mtu ambaye hapendi kuabudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…