Najuta kuoa mwanamke mlokole

Mkuu pole kwa masahibu.
Ningependa nishauri ila kabla sijafanya hivyo, nataka kujaua anaabudu Kanisa gani na wapi? Ni TAG, EAGT, KKKT,..n.k na kanisa lake ni wapi e.g Kariakoo, Mbagala,...?
 
Heri shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua.
 
Duu hawa watu wanaojiita wameokoka ni mashwetani,ninao dada zangu karibia ya wote wameingia huko yani ni shida kuanzia kwa family zao hadi kwa wazazi.then wakisha kua walokole wanakua na roho mbaya na unafki wa kupitiliza..kikubwa fanya maamuz ya kiume ukicheka na nyani utavuna mabua mkuu.huyo ni mwanzo wa kuyumbisha maisha yako na familia kwa jumla.mungu kakutoa tongo tongo kugundua hlo ukibaki unamng'ang'ania utajajuta.Yani wanakuweka had ndani then unacheka nao aisee!.Kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Malipo hapa hapa duniani, kama ulivyomtenda recho ndivyo yanavyokukuta wewe
 
Shida ya kuish na ukweni jirani kibongo bongo amri zinakuwa zinatoka Vatican
Walokole wanapumbaza waumini sana
Kuna shangaz yangu sasa vitu vyote amemalizia kwa kakobe, mwishoni mwa mwaka jana alipanga kuuza gari lake!
Duuh ukristo siku hizi ni kudai hela tu, michango michango michango daily.
Pole ndugu
 
Unasema utadhani sisi tunaishi nje ya Dunia
Makanisa yamezidi michango, wachungaji wengi ni wezi, wanawalaghai waumini kwa mistari ya kuwaletea hofu kisha watolea kila kitu na wao wabaki kuish kwa imani tu.
Sisi wenyew ni waumini na tuna ndugu wamefilisika.
 
Ulikosea kutofikiria mbele zaidi.. yaani maisha baada ya ndoa.

Naamini hizo ratiba alikuwa nazo pengine kabla ya kukutana na wewe, lkn pia ktkt uchumba wenu bado zilikuwepo kwa namna moja au nyingine ukapuuza. Na hayo ndio matokeo yake.

Cha msingi mpige ban ya maana hadi akili ikae vizuri, ajue kutofautisha maisha ya ndoa na maisha ya kanisani, kwani kila kitu kina muda wake na umpe chance nyingine endapo hatojirekebisha mrudie tu Rachel wako kama bado hajaolewa
 
.
Hapo kwenye rangi....

Kuna ulokole unaowaziba akili baadhi ya watu kiasi cha kuwafanya mabwege. Natoa mfano. Mlokole anagombana na mwanandoa mwenza au bosi wake ofisini; kisha anakwenda Kanisani na kumwambia Mchungani "niombee, nyumbani/ofisini kuna moja, mbili, tatu." Mchungaji anamwombea, kisha mchungaji huyo anapelekea taarifa hizo kwa wachungaji wenzake au kwa Bosi wa Bosi. Hapa bosi wa bosi au mchungaji wa mchungaji wanamrukia bosi au mume. Ni majungu juu ya majungu. Hivyo ndivyo Makanisa ya kikachero yaliyoanzishwa siku hizi yanavyofanya kazi. Ni vurugu tupu. Hivyo, sio kanuni ya jumla kwamba, "kuokoka kutamfanya [kila mwanamke] kuwa mtii kwa mme wake." Ulokole mwingine ni chanzo cha migogoro ya kijamii na kiofisi. Ni ulokole wa kijinga tu.
 
Hii Dunia ina maajabu mengi sana,waweza muoa Kahaba na akatulia lkn mlokole mkashindwa kuelewana!
 
Achana na chakula ya kanisa,kam wewe sio mlokole huwezi kuwa na mlokole,ndege wafananao huruka pamoja.
 
Naunga mkono hoja yako. Hawa walokole wanakuja sera za kif@l@ sana. Wanapotea kwa kutokujua maandiko wanamwamini mchungaji kuliko kitabu/Biblia. Hovyo sana
 
uko sahihi news 100. ila kama karud anataka muongee msikilize na akikubali afuate mashart na namkae mpange mpango kaz wa shirika wa maisha. na kama tatizo ni hilo tu hana jingine kaa nae usikubali kuoa mke mwi gine utaingia choo cha kike
 
Sijasoma mpaka mwisho maana nimeshindwa kuvumilia unyama wako, pumbaf* saana wewe, hata mwanamke akosee vipi huwezi kumpiga kiasi hicho
 
Enyi wake watiini waumezenu.
Enyi kina baba ishini na wakezenu kwa akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…