Najuta kuoa mwanamke mlokole

Poleeee sana ndugu haya makanisa ya wachungaji kazi ni shida wanawajaribu akili watu
 
narudia tena mwanaume kamili na anayejiamini hpigi mke. mambo ya kupigana ni ya kinyama na hata wanyama hawapigi wanawake zao.huwezi kumrekebisha mtu kwakumpiga.unaonaje ukimpiga alafu ukamtia ulemavu.
kuna siku nilikuwa namwambia mtu pombe haifai.akasema hapana bwana inafaa ila usizidishe tu. nikamwambia tatizo la pombe ni pale ambapo unatakiwa kusema inatosha sasa.
mke sio mtu wa chini kiasi hicho. mbona wewe ukikosea hupigwi. huo ni mfumo kikurya ambao personally naudharau sana. wanaoongoza kwa mauza uza kwenye mahusiano mengi ni wanaume. wengi wanajisifia kufanya uzinzi ni uanaume na hata wanapofumania kuomba msamaha kwa mke wako unaona ni kujishusha. huo ni ujinga, upumbavu, ulimbukeni na ushenzi. mwanaume anayejitambua hawezi kuunda familia ya kupigana pigana. pia mambo ya kupigana sio ya kistaarabu wala kiungwana.
pia mke sio mtoto wa kuchapwa kiboko. mke ni patner. ana haki sawa kama wewe. watu wanaopenda kupiga ujue walikuwa abused wakati wa utoto wao.tabia ya kupiga ni tabia ya kinyama. ukishidwa kumrekebisha kwa vikao ujue umevamia ubavu wa mwenzakona sio wako huyo. sifa ya mchungaji mwema ni sauti yake kusikilizwa na kondoo wake. ukiona kondoo wako hasikilizi sauti yako ujue wewe sio mchungaji na hao au huyo sio kondoo wako
pia nakuona kama unahitaji msaada wakisaikolojia kwenye hili. am sure maafisa ustawi wa jamii wanaweza kusaidia na wanasaikolojia kama una hasira mbaya na tabia ya kupigamke. mtu anayemdharirisha mkewekwa kupiga ana chance kubwa pia kuwa huwa anabaka mkewe. hatuwezi kuunda taifa la wapigaji na wabakaji. lazima tabia hii ikome kabisa na ninasema ukweli nikikuta mtu anapiga mkewe barabarani lazima na yeye apigwe tu, maana hakuna namna nyingine na nasema apigwe tu apigaye mkewe
 
neno "MLOKOLE" ni neno TAKATIFU, mtu anaweza kujibebesha neno ulokole lakini yeye akawa siyo. ndivyo walokole weng wa miaka hii walivyo, wazee wengi wa zamani wamekuwa ni waadilifu na wapenda amani sana na sio kwamba wote walikuwa WALOKOLE, siku hizi mambo yapo kinyume xana huwez jua nini mwenzio anawaza juu yako. Mungu kwanza mambo mengne yafuate lakini neno linasema MWANAUME ampende mkewe na MKE amtii mumewe, kama kweli unampenda mke wako na yeye hakutii ww mumewe akumbuke kuwa BABA ni kichwa cha nyumba hata km kuna vitu kakuzidi hivyo inawezekana ww sio ubavu wake aliopangiwa na MUNGU, km ni ubavu wake na analeta ujuaji (bongo movie) basi na APIGWE TU!
 

Nashukuru umenena kwa busara ya hali ya juu.

Kwa maoni yangu hilo kanisa lina chembe chembe za cult. Cults huwa hazizingatii Biblia pamoja na kwamba zinaanza kana kwamba ni kanisa lenye msingi wa kiBiblia. Cult hizi huwa zinapindisha ukweli wa Mungu kidogo kidogo na hivyo kuwapotosha waumini taratibu, brainwashing. Mwishowe, muumini anakuwa hajitambui, haelewi na hataki kueleweshwa. Nia kuu ya waanzisha cults hizi ni kuwachomolea pesa, kuwadominate na to possess the members. Kibwetere ni mmojawapo alienzisha dini fake na kuishia kuwachomea kanisani waumini pamoja na kutoroka kusikojulikana na mali na fedha za hao marehemu. Pia Nkonyi nae wa huko huko Uganda, anaendesha vita na vitendo vya ukatili mkuu dhidi ya wananchi wa Uganda kwa kisingizio cha kuwa kiongozi wa The Lord's Resistance army. Anataka nchi iendeshwe kwa misingi ya amri kumi za Mungu ila at the same time anaua wasio na hatia pamoja na kubaka wanawake na watoto na kuwakata viungo.

Mwishowe, mtu alieokoka , kama alivyosema mkuu niliem quote, familia ni ya kujali maana 'asiewajali wa nyumbani mwake ameikana imani'.
 
Usije kuta mchungaji anakamua, maana dunia ya siku hizi imekuwa hovyo sana
 
Nadhani uende ukaongee na Baba Mchungaji kuna tatizo gani mke asahau majukumu ahudumu kanisa zaidi
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] da afu na Mimi Nina ndoto ya kuoa mlokole
 
Daaah!! Pengine unavua ulichokipanda kwa Rachel.

Ila ni kweli hata mimi nilishamshushia kipigo wife kwa ujinga huo.

Na hawa wanawake wa namna hii ndio hutufanya tuwe na michepuko aisee.
 
Kama amekuomba msamaha na kutaka kurudiana ina maana amegundua kosa lake na yuko tayari kubadilika. Nakushauri mkae chini muongee myamalize na umpe masharti yako. Siku zote kuna nafasi ya mkosaji kujirekebisha na wewe pia samehe mkeo. Kuoa mwingine naye atakuja na yake mwishowe utasema dunia imekupa kisogo. Mna mtoto tayari amka
 
Umenifurahisha uliposema "walipofika tu nikakamata wote wawili nikawapa kipigo kizito sana.."
 
Heri ukosee kushona suti, utashona nyingine kuliko ukosee mke au Mme...
 
" Waache wafu wazike wafu wenzao" njia iliyokuwa rahisi ni wewe kusoma sana maandiko ili uwe na uwezo wa kushirikiana naye na kumfafanulia baadhi ya mambo ikiwa na pamoja na kuwa na kiasi. Kumpiga ulikuwa hutatui bali ulikuwa unaendelea kumuongezea Muda wa kumlilia Mungu wake tena. Ulienda kanisa LA walokole ili upate mke mwenye hofu ya Mungu wakati wewe ukiwa huna Nuru hata punje hivyo haiwezekani Pepo akaenda kutembelea mbinguni hata siku moja hapo ilikuwa ni vita kati ya Nuru na Giza.
 
tupe mrejesho mkuu, kwa sasa imekuaje maana ni muda sasa umepita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…