Najuta kumpa Magufuli kura yangu

Najuta kumpa Magufuli kura yangu

Nairobian

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
873
Reaction score
2,283
Bila shaka vilio na kusaga meno vimetanda nchi nzima. Hasa kwa mashabiki wa UKaAWA waliokuwa na nafasi kubwa serikalini. Kwa mfano Rished Bade na wengine wengi. Kasi ya Magufuli ingawa ina mazuri yake, inayo pia mabaya yake mengi sana.

Vilio vimetanda kila kona ya Dar. Wadada zetu warembo waliokuwa wanatujazia barabara na magari aina ya Vitz, IST na Passo za kuhongwa wameanza kusaga meno kwa kiwango kikubwa. Hawana hela za Mafuta.

Nyumba nyingi zilizokuwa hazishikiki, zikipangwa kwa dola, zitakuwa ni kama mapango, kwani wengi hawataweza kumudu gharama za kuhonga kwa kulipia nyumba kwa dola, kusomesha watoto na kutunza familia zao.

Mazuri ya Magufuli ni kwamba, Ndoa zitaimarika, huku Waliokatwa na panga la Magufuli wakimrudia Mungu. Magufuli katurudishia heshima mtaani, mbembwe za wauza sembe na vichepuko vyao imekwisha. Hofu imetanda

Mimi najuta tu kwa sababu, niliipigia kura CCM nikitegemea, Magufuli angetusaidia sisi makada tuliopo serikalini. Najuta kwa sababu, matumizi yangu mengi na miradi ya kimaendeleo ilitegemea safari za nie, posho na dili Wizarani. Mambo sivyo, maisha yamekuwa magumu mno .

Makahaba wataongezeka kwa kiwango kikubwa tena wa bei ya kumwaga, majambazi nao wataongezeka zaidi. Maisha yanaelekea kuwa magumu mno.

Shule za English Medium, zaelekea kufa, Biashara za mama Lishe, wauza vifaa vya ujenzi, wenye mahoteli etc??Uchumi wetu unaelekea kubaya

Ha ha ha ha ha ha!!!!
Sauti ya Umeme@ NY
 
Pole sana. Sisi Tulimpigia kura Magufuli kwa kutaraji kuwa atatuletea mabadiliko ambayo ndiyo yanayoendelea sasa. Kama ulimpigia Magufuli kwa lengo la kulipwa fadhila basi umeula wa chuya
 
Ahahaaaaaa, so umekatwa?
Go Magufuli go, ulipo tupo.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana. Sisi Tulimpigia kura Magufuli kwa kutaraji kuwa atatuletea mabadiliko ambayo ndiyo yanayoendelea sasa. Kama ulimpigia Magufuli kwa lengo la kulipwa fadhila basi umeula wa chuya

Sikumpigia lakini kuwepo kwake na kutenda kwake ndiyo kitu nilichokuwa nina kililia. Nilitaka mabadiliko nchi ilioza/imeoza bila kujali mbadilishaji anatoka chama gani kama ana mudu namuunga mkono. Asante Magufuli.
 
Kwaiyo hata bodi ya muhimbili ilikua ukawa nayo kwakua imepigwa chini?
 
Kheeee! Sauti ya Umeme siku hizi ndio nairobian Matola? Anyway,inawezekana hujuti kweli ila kuna wanaojuta hata kupitisha jina lake:nono:
 
Last edited by a moderator:
ahahahaha ungempa fisadi lowassa au ujamsikia yule mzee mchaw kingunge alisema ccm imeishiwa pumzi
 
Na hasa sisi wapenzi wa michezo tulivyosikia Azam tukadhani itaishia huko sasa na mdhamini wetu Mbeya City tumeanza kujuta. Nasikia na dons wa smba na yanga nao wamewekewa kibano!
 
Unajuta nini sasa!, bado tunataka magufuli akaze uzi mpaka watu waone kufanya kazi wizarani(wizara mbalimbali) sio deal.Yaani alie wizarani awe na kipato sawasawa na wa mikoani, hiyo ndo Tanzania tunayoitaka.
 
Mjini lazima heshima irudi bila kazi utahesabu mabati tu 😀
 
Kheeee! Sauti ya Umeme siku hizi ndio nairobian Matola? Anyway,inawezekana hujuti kweli ila kuna wanaojuta hata kupitisha jina lake:nono:

Tutaheshimiana sasa.......
Kwa jeuri tu Kikwete majuzi alikuwa London akatua Johanesburg kwenye mkutano wa Marais ulioandaliwa na Rais wa China, huyu Mkwele bila kumtia jela kwa kulihujumu Taifa ataendelea kujisahau na kudhani yeye bado ni Rais wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom