kholo
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 413
- 76
Habari za majukumu wana jf, kwa mara ya kwanza nimejikuta nikiingia katika jukwaa hili nikiwa muhanga na majeruhi wa kufa leo au kesho kwa sababu ya mapenzi, ni miaka 2 sasa imepita toka nimfahamu huyu binti anayeninyanyasa(tukiwa shule kipindi hicho) na katika kipindi cha mwaka mmoja tuliokuwa pamoja shule tuliishi vizuri ila sii kama wapenz, nilitokea kumpenda sana ila sikuthubutu kumwambia kutokana na kuhofia kuchanganya hali ya mambo japo baadaye aligundua. Na katika kipindi cha mwaka mzima tulipoachana baada ya kumaliza shule tuliendelea kuwasiliana japo kwa mara chache ila ugonjwa wangu haukuwa umetibika bado kwan kila nilipoisikia sauti yake mapigo ya moyo wangu yaliongeza kasi lakin pia sikumwambia kuwa nampenda. Zahama ilianza baada ya kumwambia ukweli kuwa nampenda mwezi 1 uliopita, alinikubalia na akaniambia hilo alilitambua toka mwanzo, cha ajabu kwangu imekuwa mateso kwan ninapoongea naye kwenye simu najisikia burudani sana ila simu iki katika tu na aman nayo inatoweka kwangu na hakuna ninachoweza kufanya kikawa sawa hata kula inakuwa shida, namuwaza yeye tuu. Natamani kusitisha uhusiano ila nafsi yangu inanambia ni afadhali mimi nife kuliko kusitisha uhusiano, nashindwa kuelewa kuwa nampenda au namtaman. Wanajamvi plz, ushauri wenu ni muhimu sana kwangu kwan najihisi kupungua uzito kwa kuwaza. Ahsanten