Najmunisa

regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
51
Naombeni msaada wadau. Ninasafiri kwenda dodoma nimepanda gari ya Najmunisa inayoelekea Mwanza. Kwa kweli dereva anaendesha basi vibaya. Tumejaribu kumkemea lakini hasikii. Naombeni namba ya polisi niko jirani na chalinze
 
Siku hizi polisi wamebandika namba zao kwenye mlango wa dharura wa kila basi. Jaribu kuangalia.
 
we unaenda karibu kwa hiyo ungepanda zako shabiby kuliko kupanda basi linaloenda mbali asipofanya hivyo watafika mwanza kesho we sali tu msiishie njiani..
 
Unaposema anaendesha vibaya una maana gani? Anaenda mwendo mdogo? Anaenda mwendo kasi? au anaendesha pembeni mwa barabara??
 
Hilo basi jina la mtaani linaitwa super majini ya musa!!!! Ngoja nikupe namba mie mnoko nakupa ya kamanda mpinge 0754360046 huyo ndiye mkubwa wa matrafiki bongo mwendee hewani moja kwamoja
 
Buji buji mie huwa napenda masihara yako, tayari umeshambadilishia mantiki yake!! kuendesha vibaya ni kutofuata misingi na taratibu za driving, iwe kwenda pembeni, mwendo kasi, mwendo mdogo,kuyumbayumba, nk haya yote ni makosa inategemeana na upo wapi, akiwa kwenye oneway akaendesha spidi 10 ni kosa!
 
Tatizo la Najmunisa ni kupasuka mataili, halafu mara nyingi yanapasuka lakini basi halianguki, hivyo jiandae kulala njiani.
 
ha ha ha ha ha.....hapo kwenye buluuu nimecheka sana, yote maswali ya msingi sana
Unaposema anaendesha vibaya una maana gani? Anaenda mwendo mdogo? Anaenda mwendo kasi? au anaendesha pembeni mwa barabara??
 
Back
Top Bottom