Najivunia kuwa brazamen

Kubali kataa kuwa bishoo ni hela kama huna hela huwezi kuwa brazamen miaka mia8 pili watu wamekariri kuwa brazamen ni lazima upake poda hizo ni akili za kijinga kuwa brazamen ni kuwa msafi na kujijali huku ukipiga kazi ili ueendelee kushine ukiwa mchafu mchafu uko hovyo hovyo hung'oi mtoto mkali hata siku moja
 
Nachojivunia kwanza Nina jicho la nguo huwa sibaatishi Mzee baba,rangi pia naangalia jinsi ya kumechisha,pia navaa kutokana na sehemu nayoenda na aina ya watu ninaenda kukutana nao, nikivaa suti imoo,nikavaa kanzu ipo,t-shirts na jeans vitu vinakaa!full usafi hadi inzi wananiona kwenye TV,Viatu pea kama zote!siwezi kunuka kijasho mtoto wa town kama Mimi!
vipi unaoga mara ngapi kwa siku
 
Navaa pamba kali na najua haswa kuvaa vitu vikali.

Napenda usafi wa mwili wangu mpaka mazingira yanayonizunguka.

Nnanukia perfume nzuri Gucci, Creed au Uomo.

Napenda kutumia vitu vyenye quality na standards za juu. Najali sana viwango kwenye kila kitu changu.

Kibongobongo wananiita brazameni na silichukii ilo jina.

Ubrazameni ni damu unazaliwa nao, wengi wanapenda swaga za kibrazameni ila ndio hivyo wanajikuta hawawezi sababu uwezi jifunza kuwa brazameni utachemsha tu.

Wenye hasira na sisi wanaishia kutuita majina mabaya kutuchafulia CVs. Wanatuita wauza sura, wanaume wa dar, wapaka poda na kutuchafua kwa mademu eti hatuna pesa lakini cha ajabu mademu awaambiwi awasikii kwetu wanatukubali ile mbaya.

Siwezi enda kwenda board room kufanya presentation ya mradi wangu uku nanuka kijasho cha saa saba eti ndio uanaume lazima nichukuliwe poa, lazima nijali muonekano wangu uniuze na kuepuka harufu za kibinadamu.

Navinjali sehemu zenye watu classic ata kama inanigharimu lakini napata connection zenye akili. Bia ya Maison ni gharama ila inanilipa kuliko bia ya buku mbili ya La Chaz.

Najivunia kuwa brazameni na kwa mabrazameni wenzangu msijisikie vibaya kuitwa mabrazameni.
Mkuu basi Mimi tuna swaga moja na wewe,,ila mimi wananiita check Bob,,,mtaani,,, sasa sijuwi kuna tofauti hapo,,,,ila napita mule mule,,,chini Nike ,,,belt brown au black pure leather,,, saa diesel,,miwani ray band...wallet diesel,,hakuna mambo ya kuweka pesa kwenye soksi,,,.

Perfumes xs Paco rabanne ,,, ANTHONIO BENDAS au Essie miyake,,au joop...mkuu zote napiga mix ,,2 drops each perfume,, mkuu demu simpigii simu,,namwita kwa harufu tu..nikipita barazani kwao mwenyewe anatafuta nilipokuwa...anapata salamu..
 
Back
Top Bottom