Najipanga kwenda Canada kutafuta maisha

Omary zablon

New Member
Sep 1, 2021
4
14
Hello guys mambo vipi poleni na majukumu. Kwa majina Naitwa Omary naishi Nairobi ila elimu yangu ya Msingi mpaka Chuo nimepata Tanzania. Naamini hii ni platform kubwa sanaa ambayo imejaa watu wa kila aina hivyo basi nategemea once nitakavyo leta swala langu kwa ajiri ya ushauli ni furaha yangu ntapata comments za kujenga.

Kubwa kabisa mpaka naandika hii issue ni juu ya mimi kutaka kwenda nchini Canada kwa lengo la kutafuta maisha naamini mimi ni kijana ambaye bado nguvu ninazo na changamoto ni sehemu ya maisha.

Hivyo basi natamani kwenda Canada kwa ajiri ya kuangalia upande mwingine wa shillings then nirudi nchini kwetu kwa ajiri ya kusapotiana na vijana wenzangu, sio kwamba huku hakuna fursa lahasha zipo ila kwangu naona kama mungu hajanijaria hivyo nahitaji ku jaribu upande mwingini.

Ahsanteni na samahi kwa usumbufu
 
Kama unakwenda kujaribu hutafanikiwa. Tatizo la walio wengi ni kujaribu badala ya kufanya kweli. Kanada ni nchi nzuri sema ina mfumo wa kibaguzi kuliko hata Marekani. Ni tajiri sana ila kama siyo mweupe ni kazi kufaidi utajiri huu. Ina kila kitu ila ni vigumu kukipata kama mipangilio yako siyo mizuri.

Pia ni vigumu kuingia nchi hii yenye uzuri na ubaya wa aina yake. Huo ndiyo uzoefu nilio nao kuhusiana na nchi hii ambayo kusema ukweli inavutia kwa juu ila ndani si hivyo. Niliwahi kukaa kule kwa muda na kuamua kuondoka mwenyewe.
 
Habari Wakuuu nina plani ya kwenda Canada kama mungu akipenda kwa ajiri ya kwenda kujaribu bahati yangu kwa wenye kujua kuhusu hii nchi naombeni experience tafadhali, Mind you sina ndugu ndo naenda kujifatuta
Shehe Omary Hilo jina hupati viza kabisaa. Jaribu Saudia ama Oman. Unaweza kupata kazi za kulima tende au kusafishwa mitaro.
 
Mkuu Hizi nchi za Wazungu Mara nyingi sio Nzuri Kwenda bila kuwa na mwenyeji (kujaribu maisha)

Hata Ukiwa na mwenyeji kwa Mara ya kwanza Unaweza kubahatisha ukaenda lakini Mara nyingi lazima upitie Tabu kidogo

Wengi wamekuwa wakienda kwa kuungaunga mfano mtu anaenda Germany Basi Ataenda Belgium Kisha ndio aungeunge kuingia Germany kwa Treni au Bus pia na nchi nyingine nyingi kubwa Huwa hivyo hivyo mlolongo Wake ni mrefu

Nakushauri Kama umejipanga Nenda Meddle East Kama Dubai au Qatar Angalau Ufanye Kazi Huko hata kwa mwaka mmoja tu

Huko utapata connection ya kuingia huko kwa Wazungu

Bila Hivyo unaweza ishia Uwanja Wa ndege Ukabaki kujutia Gharama Zako

Alafu pia Kwenda Dubai ni rahisi kwasasa hata gharama sio kubwa pamoja na Visit Visa yake ya 30 days inapatikana kirahisi sana

Ukiwa na 2milion inaweza tosha kabisa kukufikisha Dubai na ukapata pesa ya kuishi Dubai bila kazi kati ya siku kumi mpaka 15 kama Ukiwa na mwenyeji

Dubai kazi Ni uhakika kwa 90% Labda uamue tu kuchagua na Pia mshahara Sio mdogo kiwango cha chini kabisa hucheza Kati ya laki 4 au 5 Ila mishahara mingi zaidi Ni kuanzia laki 7 na kuendelea na Hawakati Kodi yoyote unapokea pesa yako kamili..
 
Babu nenda na uende wala usiogope na asikutishe mtu hata kama anakaa huko au aliishi huko (virtually)

Kumbuka huko sio kwako lakini ukiamua na kujituma unaweza kubadilisha mawazo na ukapafanya ndio makao yako milele ili mradi kwa kisheria.

Usiwe sensitive sana kuona kila kitu unabaguliwa kwa rangi yako, mengine utakuwa unajihisi tu mwenyewe.

Kuwa mchapakazi na mcheshi, wewe utakuwa ni mgeni kwenye hii nchi, kwa hiyo lazima uwe na maongezi ya kicheshi na kuchangama kwa sana, utaeleweka vizuri badala kuwa boring na bubu.
 
Maskini hujui unachoongea. Huo unaoona kama ucheshi, kwa wenzio si chochote wala lolote. Nadhani kama utafanya utafiti mdogo, Kanada kwa sasa inapunguza idadi ya watu wanaoingia na kukaa mle. Kumbuka waswahili wengi walioko Marekani wanakimbilia Kanada hasa wakati wa msimu wa baridi.

Kusema nimeishi huko virtually ni kutojua maana ya neno utumialo. Kwani, ni heri lawama ya mwenye busara kuliko wimbo wa sifa wa mpumbavu. Mie nimetoka uzoefu wangu. Si vibaya kupingana nao au kukubaliana nao. Huo ndiyo ukweli hata kama haukukupendeza.
 
Mkuu Hizi nchi za Wazungu Mara nyingi sio Nzuri Kwenda bila kuwa na mwenyeji (kujaribu maisha)..

Hata Ukiwa na mwenyeji kwa Mara ya kwanza Unaweza kubahatisha ukaenda lakini Mara nyingi lazima upitie Tabu kidogo..

Wengi wamekuwa wakienda kwa kuungaunga mfano mtu anaenda Germany Basi Ataenda Belgium Kisha ndio aungeunge kuingia Germany kwa Treni au Bus pia na nchi nyingine nyingi kubwa Huwa hivyo hivyo mlolongo Wake Ni mrefu..

Nakushauri Kama umejipanga Nenda Meddle East Kama Dubai au Qatar Angalau Ufanye Kazi Huko hata kwa mwaka mmoja tu

Huko utapata connection ya kuingia huko kwa Wazungu

Bila Hivyo unaweza ishia Uwanja Wa ndege Ukabaki kujutia Gharama Zako..

Alafu pia Kwenda Dubai ni rahisi kwasasa hata gharama Sio kubwa pamoja na Visit Visa yake ya 30 days inapatikana kirahisi Sana..

Ukiwa na 2milion inaweza tosha kabisa kukufikisha Dubai na ukapata pesa ya kuishi Dubai bila kazi kati ya siku kumi mpaka 15 kama Ukiwa na mwenyeji...

Dubai kazi Ni uhakika kwa 90% Labda uamue tu kuchagua na Pia mshahara Sio mdogo kiwango Cha chini kabisa hucheza Kati ya laki 4 au 5 Ila mishahara mingi zaidi Ni kuanzia laki 7 na kuendelea...
Huo mshaara ni kwa mwezi au wiki?
 
Maskini hujui unachoongea. Huo unaoona kama ucheshi, kwa wenzio si chochote wala lolote. Nadhani kama utafanya utafiti mdogo, Kanada kwa sasa inapunguza idadi ya watu wanaoingia na kukaa mle. Kumbuka waswahili wengi walioko Marekani wanakimbilia Kanada hasa wakati wa msimu wa baridi.

Kusema nimeishi huko virtually ni kutojua maana ya neno utumialo. Kwani, ni heri lawama ya mwenye busara kuliko wimbo wa sifa wa mpumbavu. Mie nimetoka uzoefu wangu. Si vibaya kupingana nao au kukubaliana nao. Huo ndiyo ukweli hata kama haukukupendeza.
Nasikia Wahindi wapo wengi huko! Kwanini imekuwa rahisi kwao?
 
Nasikia Wahindi wapo wengi huko!,kwanini imekuwa rahisi kwao?..
Kipindi kile niko kule walikuwapo lakini hawakuwa wengi kama wazungu toka ulaya mashariki, wanigeria au wafilipino. Walikuwapo wakiendesha taxi mijini na kusota kama wengine ukiachia mbali wale ambao walipiga shule kama madaktari na wafamasia. Unajua wahindi siyo toka india tu bali karibu nchi nyingi za asia kama vile bangladesh, nepal, pakstan, afghanistan, na kwingineko.
 
Kama unakwenda kujaribu hutafanikiwa. Tatizo la walio wengi ni kujaribu badala ya kufanya kweli. Kanada ni nchi nzuri sema ina mfumo wa kibaguzi kuliko hata Marekani. Ni tajiri sana ila kama siyo mweupe ni kazi kufaidi utajiri huu. Ina kila kitu ila ni vigumu kukipata kama mipangilio yako siyo mizuri. Pia ni vigumu kuingia nchi hii yenye uzuri na ubaya wa aina yake. Huo ndiyo uzoefu nilio nao kuhusiana na nchi hii ambayo kusema ukweli inavutia kwa juu ila ndani si hivyo. Niliwahi kukaa kule kwa muda na kuamua kuondoka mwenyewe.
Umeeongea ukweli
 
Kuna kitu mimi nilijifunza nilipokwenda South Africa. Maisha ya kule ni shule tosha kama unataka kuishi nchi za ulaya.

Na kumbuka kama maisha yako ujajifunza kuwa smart au kuishi sehemu za kama Masaki, Ostabey au Mbezi Beach.

basi ukishindwa kuwa vile utakuja kuishi maisha ya mateso hata yule maskini wa kijijini ni tajiri.

utakuja lala madarajani, pembezoni mwa maduka, majumba mabovu, utaokota chakula kilichotupwa.

Utapoteza mda ambao ukija kurudi nchini uliowaacha wanamaendeleo.

Mimi na watu najuana nao sana wanakwambia miaka ya sasa sio kukimbilia nchi za ulaya wa huko nilipotoka.

Ni bora ukajikita na Tanzania yako tena kwenda kwenye mikoa ambayo sasa inaanza kukuwa kutafuta kama manispaa.

tTnzania fursa zipo nyingi sema asilimia kubwa watu wengi tumekalia Dar es Salaam ambapo kiwango cha mji huo kinataka kuwa na mitaji mikubwa.

kuna sehemu siwezi kukwambia kwa sasa ila wapo wachina,wakenya,warwanda,wazungu hata ukiongea nao wanakwambia ni rahisi kutoboa tanzania maana fursa zimelala.

nchi yetu tumelala kwa ajili ya mifumo mibovu ya serekali ndio maana inapelekea kuona nchi za ulaya ni rahisi kutoboa
 
Kama unakwenda kujaribu hutafanikiwa. Tatizo la walio wengi ni kujaribu badala ya kufanya kweli. Kanada ni nchi nzuri sema ina mfumo wa kibaguzi kuliko hata Marekani. Ni tajiri sana ila kama siyo mweupe ni kazi kufaidi utajiri huu. Ina kila kitu ila ni vigumu kukipata kama mipangilio yako siyo mizuri.

Pia ni vigumu kuingia nchi hii yenye uzuri na ubaya wa aina yake. Huo ndiyo uzoefu nilio nao kuhusiana na nchi hii ambayo kusema ukweli inavutia kwa juu ila ndani si hivyo. Niliwahi kukaa kule kwa muda na kuamua kuondoka mwenyewe.
Kupata visa ya canada ngumu sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Maskini hujui unachoongea. Huo unaoona kama ucheshi, kwa wenzio si chochote wala lolote. Nadhani kama utafanya utafiti mdogo, Kanada kwa sasa inapunguza idadi ya watu wanaoingia na kukaa mle. Kumbuka waswahili wengi walioko Marekani wanakimbilia Kanada hasa wakati wa msimu wa baridi.

Kusema nimeishi huko virtually ni kutojua maana ya neno utumialo. Kwani, ni heri lawama ya mwenye busara kuliko wimbo wa sifa wa mpumbavu. Mie nimetoka uzoefu wangu. Si vibaya kupingana nao au kukubaliana nao. Huo ndiyo ukweli hata kama haukukupendeza.

acha kukatisha watu tamaa kama wewe ulishindwa kuishi na kurudi mbagala kisa eti ubaguzi iyo kwetu sio ishu, wakati wengine wanaposhindwa wengine ndiyo fursa, nyie wa kishua mnadeka deka sana tatizo lenu? kama swala ni ubaguzi hata tz upo sana bongo kama wewe sio ccm utabaguliwa mpka ukome
 
Hello guys mambo vipi poleni na majukumu. Kwa majina Naitwa Omary naishi Nairobi ila elimu yangu ya Msingi mpaka Chuo nimepata Tanzania. Naamini hii ni platform kubwa sanaa ambayo imejaa watu wa kila aina hivyo basi nategemea once nitakavyo leta swala langu kwa ajiri ya ushauli ni furaha yangu ntapata comments za kujenga.

Kubwa kabisa mpaka naandika hii issue ni juu ya mimi kutaka kwenda nchini Canada kwa lengo la kutafuta maisha naamini mimi ni kijana ambaye bado nguvu ninazo na changamoto ni sehemu ya maisha.

Hivyo basi natamani kwenda Canada kwa ajiri ya kuangalia upande mwingine wa shillings then nirudi nchini kwetu kwa ajiri ya kusapotiana na vijana wenzangu, sio kwamba huku hakuna fursa lahasha zipo ila kwangu naona kama mungu hajanijaria hivyo nahitaji ku jaribu upande mwingini.

Ahsanteni na samahi kwa usumbufu
Kama Muislam kwa nn unashabikia nchi za Makafiri? Nenda Saudia upige pesa za Mahujaji deals kibao
 
Back
Top Bottom