Najipanga kuchukua likizo ' Maalum ' ya kuwatafakari akina Mange Kimambi na Cyprian Musiba kwani naona kuna ' yaliyojificha ' mengi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Kwa yanayoendelea kwa sasa nchini Tanzania huku na hawa Wanaharakati wawili mmoja wa Upinzani na mwingine wa Serikali akina Mange Kimambi na Cyprian Musiba nahisi wamebakisha muda mchache mno wa kunifanya GENTAMYCINE niwe Taahira kabisa kutokana na wanayoaandika na kuyazungumza.

Kuna lililojificha na ' bomu ' kubwa linakuja nchini Tanzania kama hawa wote hawatasikilizwa na Wahusika kuyafanyia Kazi huku Watanzania kwa ujumla wetu tukikubali kuwa kuna mahala kama Taifa tumekosea kisha wote tuombane radhi / msamaha na tukubaliane kuanza upya kwa maslahi mapana ya Mama Tanzania yetu.

Nisiwaficheni sasa naanza ' Kuogopa ' juu ya mambo yanavyokwenda na naanza kuamini kuwa Mange Kimambi huwa yupo sahihi 100% na hata huyu Cyprian Musiba ne yupo sahihi kwa 100% kutokana na kwamba Wawili wote hawa ' taarifa ' zao zote huwa wanazitoa kule kule Makao Makuu ya ' Unyeti na Uzandiki ' nchini Tanzania hivyo hawabahatishi.

Mwenyezi Mungu nakuomba ingilia kati haraka kwani kwa dalili ninazoziona sasa kama ' Malaika ' wako pamoja na Wewe hamtoingilia kati ile Tanzania ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere, ya Mzee Mwinyi, ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete inakwenda kupotelea kama siyo hata Kuangukia kwa Baba Dkt. Magufuli.

Leo GENTAMYCINE nina OMBI muhimu Kwenu hebu naomba Watanzania wote bila kujali tofauti zetu za Kivyama au Kidini au Kijiografia basi tushikane mikono popote pale na tuombane ' Misamaha ' kwa yote yaliyopita na naomba kila Mtu kwa Imani yake akienda ' Ibadani ' aiombee Tanzania yetu Uvumulivu, Upendo na Amani.

Narudia tena kusema ' Ninaogopa ' mno na kuna dalili fulani ya ' hatari ' naiona kwa mbali sana inakuja. Tujitafakari haraka sana!

Nawasilisha.
 
Kwa yanayoendelea kwa sasa nchini Tanzania huku na hawa Wanaharakati wawili mmoja wa Upinzani na mwingine wa Serikali akina Mange Kimambi na Cyprian Musiba nahisi wamebakisha muda mchache mno wa kunifanya GENTAMYCINE niwe Taahira kabisa.

Kuna lililojificha na ' bomu ' kubwa linakuja Tanzania.
Huu sio muandiko ako
 
Popoma lililotukuka hebu weka nyama kidogo maana kuna codes nyingi hapa kwenye mada yako
 
Nilisema hapa juzi(mada ilifutwa) kuwa Musiba ana copy ya blacklist iliyopo Magogoni kwa mkulu.

Blacklist hiyo inaundwa na watu walioko upinzani, ndani ya CCM,nje ya CCM na walioko serikalini ambao ni tishio kwa mkulu.

Inawezekana kabisa Mkulu ndio anamtumia Musiba kuwashambulia anaowaona ni tishio kwake.

Mkulu, kwa tabia zake, ameshajitengeneza maadui wengu hata ndani ya chama chake kwahiyo ana hofu ya kuhujumiwa na watu wa ndani ya chama chake kwa kushirikiana na walioko nje ya chama chake.Hajiamini!

Hatari iliyopo na ambayo naiona ni mkulu kutumia power yake kushughulikia baadhi ya hawa watu hatua, inayoweza kuvuruga kabisa hata chama chake.
 
HUU UANDISHI SIJAUZOEA KABISA MKUU KUTOKA KWAKO NSHAZOEA MAANDISHI YALE MADUNCHU DUNCHU IS THERE ANYBODY STOLE YOUR PHONE?

Nilikuwa bado namalizia kuuweka sawa na nadhani sasa upo kama ambavyo umezoea na ulivyokuwa unataka. Ila narudia tena kusema kuwa GENTAMYCINE ' ninaogopa ' na naomba Watanzania tushikane mikono, tukubali makosa kama yanatuhusu na tuombane ' misamaha ' kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Hii siyo dalili njema / nzuri kama ukiitafakari kwa Kina kabisa.

Cc: kunta93 , My Son drink water
 
Genta, hivi ni nani anatakiwa kwa mujibu wa sheria za asili (natural laws ) amwombe mwenzake msamaha? Namaanisha mkosewa na mkosaji! Nani anatakiwa kumwomba mwenzake msamaha?
 
Genta, hivi ni nani anatakiwa kwa mujibu wa sheria za asili (natural laws ) amwombe mwenzake msamaha? Namaanisha mkosewa na mkosaji! Nani anatakiwa kumwomba mwenzake msamaha?

Hivi niliposema kuwa naomba Watanzania wote kwa hali hii ilivyo sasa wote kwa ujumla bila kujali aliyetenda au aliyeumia tuombane ' misamaha ' ulinielewa? Mbona kama vile na Wewe unaonekana hutaki amani na unapendelea hii hali iliyopo sasa ya ' taharuki ya Kisiasa na Kidemokrasia ' na ' sintofahamu ' iendelee kuwepo? Kama ukitulia na ukayapima ya Mange Kimambi na ya Cyprian Musiba moja kwa moja utaona ' anguko ' la amani na utulivu wa Watanzania linakuja na siku si nyingi kama hatutoshtuka, jitafakari na kujisahihisha haraka.

Nasema tena Kwako kuwa sasa naanza ' Kuogopa ' kabisa na nimemaanisha Mkuu.
 
Sote hatujui kesho yetu ila imani tuliyonayo haipo kwa mange Wala musiba.imani yetu tumeamua kuiacha kwa Mungu Jehovah,yesu mwalimu na ndugu Magufuli kwa mbali Basi..hao wengine me hata siwaelewi kabisa na sitaki kuwaelewa
 
Tatizo la Musiba ni kama la RC wa Dar, mkuu kabisa anawa-entertain watu wa aina hii. Anashindwa kuwa Baba kwa maana ya mtenda haki kwa wote. Anaishia kuchukua upande fulani wa jamii.

Mange anayo mema na pia anayo mabaya yake. Sio mjinga hata kidogo.
 
Nilisema hapa juzi(mada ilifutwa) kuwa Musiba ana copy ya blacklist iliyopo Magogoni kwa mkulu.

Blacklist hiyo inaundwa na watu walioko upinzani, ndani ya CCM,nje ya CCM na walioko serikalini ambao ni tishio kwa mkulu.

Mkulu ndio anamtumia Musiba kuwashambulia anaowaona ni tishio kwake.

Naanza sasa ' Kushawishika ' kukubaliana nawe Mkuu na ndiyo maana nimesema na nitaendelea kusema kuwa naanza sasa ' Kuogopa ' jinsi hali ilivyo na mambo yanavyoendelea nchini Tanzania. Kunahitajika maombi ya nguvu kuiombea nchi, maridhiano na upatanisho wa Kisiasa na Kidemokrasia lakini kufanyike mijadala huru na ya wazi kabisa ya kuweza Kuijadili Tanzania kwa marefu na mapana yake na Wahusika ( wenye dhamana ) Kimamlaka na Kiutawala wasikie, wabadilike na Tanzania iwe moja siyo kama ilivyo sasa ambapo huhitaji kuwa na Certificate au Diploma au Degree au Masters au PhD kujua ya kwamba imeshagawanyika na imejaa chuki na fitna kila mahala.

Mwenyezi Mungu aisaidie Tanzania yetu!
 
Kwa yanayoendelea kwa sasa nchini Tanzania huku na hawa Wanaharakati wawili mmoja wa Upinzani na mwingine wa Serikali akina Mange Kimambi na Cyprian Musiba nahisi wamebakisha muda mchache mno wa kunifanya GENTAMYCINE niwe Taahira kabisa kutokana na wanayoaandika na kuyazungumza.

Kuna lililojificha na ' bomu ' kubwa linakuja nchini Tanzania kama hawa wote hawatasikilizwa na Wahusika kuyafanyia Kazi huku Watanzania kwa ujumla wetu tukikubali kuwa kuna mahala kama Taifa tumekosea kisha wote tuombane radhi / msamaha na tukubaliane kuanza upya kwa maslahi mapana ya Mama Tanzania yetu.

Nisiwaficheni sasa naanza ' Kuogopa ' juu ya mambo yanavyokwenda na naanza kuamini kuwa Mange Kimambi huwa yupo sahihi 100% na hata huyu Cyprian Musiba ne yupo sahihi kwa 100% kutokana na kwamba Wawili wote hawa ' taarifa ' zao zote huwa wanazitoa kule kule Makao Makuu ya ' Unyeti na Uzandiki ' nchini Tanzania hivyo hawabahatishi.

Mwenyezi Mungu nakuomba ingilia kati haraka kwani kwa dalili ninazoziona sasa kama ' Malaika ' wako pamoja na Wewe hamtoingilia kati ile Tanzania ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere, ya Mzee Mwinyi, ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete inakwenda kupotelea kama siyo hata Kuangukia kwa Baba Dkt. Magufuli.

Leo GENTAMYCINE nina OMBI muhimu Kwenu hebu naomba Watanzania wote bila kujali tofauti zetu za Kivyama au Kidini au Kijiografia basi tushikane mikono popote pale na tuombane ' Misamaha ' kwa yote yaliyopita na naomba kila Mtu kwa Imani yake akienda ' Ibadani ' aiombee Tanzania yetu Uvumulivu, Upendo na Amani.

Narudia tena kusema ' Ninaogopa ' mno na kuna dalili fulani ya ' hatari ' naiona kwa mbali sana inakuja. Tujitafakari haraka sana!

Nawasilisha.
Mkuu mbona unajiingiza kujadili hao non -issues.
They have never neen, will never be, driving forces in Tanzania politics.
They demand no serious thought, and doing so reduces your Great Thinking to nought,

Hao ni vibonzo, Pwagiu na Pwaguzi wa kisiasa
 
Genta, mbona ni kama unauogopa uoga wako mwenyewe? Huku nilipo sina fununu yoyote juu ya hao watu uliowataja. Kama hutojali funguka kidogo nikusome na wengine wafaidi. Uoga huo uko wapi na umesababishwa na nani au nini?
 
Kuna Kauli moja ya Kiingereza naipenda sana Mkuu inasema " Even a Fool has something to say / comment " hivyo naomba hapo katika ' Fool ' uniweke Mimi GENTAMYCINE tafadhali. Ukiona mpaka naanza kuwa na wasiwasi au hofu juu ya Jambo fulani amini 100% kuwa kuna ' problem somewhere ' japo kuna Watu wengine labda kwa Kujiamini au Kujidanganya Kwenu kwakuwa pengine mpo ' Jikoni ' mnadhani kwamba ' everything is okay '. Namalizia tena kusema kuwa naanza ' Kuogopa ' kwa hali inavyokwenda sasa nchini Tanzania na ukiwatumia hawa Watu wawili akina Mange Kimambi ( Mtetezi na Mwanaharakati ) wa Upinzani nchini Tanzania na Cyprian Musiba ( Mtetezi na Mwanaharakati ) wa Serikali ya Tanzania kama ' Kioo ' chako cha hali nzima ya Ustawi wa Tanzania yetu utagundua kuwa kuna ama bomu kubwa linasubiri Kulipuka au kuna tatizo kubwa na la msingi kwa sasa nchini Tanzania na bado halijatafutiwa ufumbuzi wake.
 
Genta, mbona ni kama unauogopa uoga wako mwenyewe? Huku nilipo sina fununu yoyote juu ya hao watu uliowataja. Kama hutojali funguka kidogo nikusome na wengine wafaidi. Uoga huo uko wapi na umesababishwa na nani au nini?

Mkuu leo hapo ' Kitengoni ' jirani na Kanisa la Mtakatifu Petro Wewe ndiyo umepewa ' Special Assignment ' ya Kumchokonoa GENTAMYCINE ili upate mengi zaidi ili baadae uyaandikie ripoti nzuri na uiwasilishe kwa Bosi wako Mkuu Mluguru sijui huyo Mpogoro? Halafu siku hizi naona hata mbinu zenu pia za kutafuta ' info ' kwa Watu zimekuwa ' very outdated ' kiasi kwamba mmekuwa rahisi mno Kujulikana tofauti na wale waliowatangulieni hapo ' Kitengo ' na ambao kwa bahati mbaya wengine sasa ni Marehemu na wengine wameshastaafu japo Kustaafu Kwao kutahitimishwa pale wakishafukiwa Makaburini wakiaga rasmi dunia.
 
Wazee wa Coded Language tumeshakuelewa kaka kabisa ila huyo wa Madini yetu inasemakana ni mnoko tuu ila Shangazi anapata info kutoka pande zote mbili halafu Shangazi pia ana support kutoka kulee kwa kaka wa mataifa inahitajika neema ya Mungu tuu
 
Back
Top Bottom