Kuna wakati huwa nakuwa sina office kwenye PC au natumia PC ya mtu nakuta nataka kuchapa kitu nakutana haina office. Option iliyopo ni kutumia Google Docs ambapo ntahitaji kusign in na vitu kama hivyo. Sasa just for fun nimeamua kuunda plugin ya chrome ambayo itakuwa inaweza kufanya basic tasks za word processing kupitia browser hata kama huna internet. Sema ninakumbana na changamoto ya kusave kwenye local storage napata tu error ndo napambana nayo.
Pia ninataka kuunda apk ambayo itakwua simple kwa ajii ya simple tasks za word na pdf reader ambayo itakuwa haina matangazo na iwe light kurun hata kwa simu za kawaida.
Mimi najifunza tu programming si programmer ambaye ni expert.