Naitaji mkopo kugaramia Arusi yangu.

Mambo ya ki-SENGE-rema usituleteee humu!
 
Acha ufala na usiishi maisha ya kukrem kama huna hela kafunge ndoa ya serikalini alika ndugu wa pande mbili tu hata laki haizidi unakuwa umeoa
 
Duh aisee we mtu wa maajabu kweli...yaani unataka ukope ili ufunge ndoa mi ningekushauri neno moja JIPANGE..nyie ndo mnakuja kuoa halafu unakuja kulalamika hapa mke wangu kanitoroka kisa ukata home..aahhh JIPANGE
 
Mbona kwenye taasisi za kifedha unakopesheka kabisa mkuu?? Tatizo ni hapo kwenye riba. Kama utachelewa kurudisha utapata hasara mkuu
 
Sure mkuu,nimefunga harusi juzi juzi tu mkesha wa mwaka mpya gharama zilikuwa hivi
1.Suti yangu 80000/= hii naendelea kuivaa
2.Nguo ya Wife 80000/=
3.wasimamizi 30000/=
4.Saloon wife na msimamizi 40000/=
5.Usafiri 30000/=
sikufanya sherehe yeyote na sijamsumbua hata mtu mmoja kumchangisha na hapa nilipo sijakopa na sina deni hata mia,ila nashukuru Mungu ndugu wamenizawadia vizawadi mpaka nimebakiwa na balance na nimefungia hapa mjini Dar Ubungo Msewe
 
Mimi naweza kukukopesha hiyo hela hata kesho ila utamwacha mke wako rehani hadi utakapo maliza deni lote. Na mke namchukua baada ya sherehe ya harusi kuisha kama dhamana. Vp upo tayari ?

Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh..... Hii kali
 
Mtolee mahali ishi nae halafu ndoa utafunga baadaee sio lazimaa sasa hivii
Jikune mkono unapofikaa
 
Haya sasa makubwa,wenzio wanakopa wafanyie biashara,we unakopa kwa ajili ya harusi hahaaaa!pole na harusi njema
 
ndg zangu huyu mwenzenu anashida 2napaswa kumsaidi, mimi decemba nilifunga haruc ,cikuwa na chochote na nafanya kz kwa mshahara wa laki 28o nikapata mkopo wa million 2.5 kwa kurejesha elf90 kila mwez na nikitoa hz hela kwenye mshahar wangu bado naendelea kusafaiv na wife nae anafanya kazi kipato chake hicho hicho na maisha yanaenda usikate tamaa we kopa ila angali cehemu ambao auna riba kubwa
 
Funga ndoa ya kimila hizo za wazungu kama huwezi waachie wenyewe.
 
Pole sana kama unafikra kama hizo, jaribu ndoa bila mahari
Utaona inavyokuwa tamu na imara kama simba.
Maisha yamebadilika sana ndugu.
Amka.
 
Ndugu wananichukia kwa kupinga sherehe, kwangu kila kitu kimya kimya si graduation wala harusi
 
Hapa tunapata picha kuwa swala la ndoa linakabiliwa na changamoto ya kipesa pia,japo kupata mchumba ni tatizo pia
 

Ina maana hajawahi kuchangia harusi yoyote? Ukipata watu 40 wakatoa 50,000 utapata 2,000,000/=. Watu 80 @ 25,000/=.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…