Naisikitikia Kinondoni kurudi mikononi mwa CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nina masikitiko makubwa kuhusu Kinondoni. Tangu niamke leo,hata kazini nimechelewa kwenda,nimekuwa nikilia kwa uchungu kuiona Manispaa ya Kinondoni ikirudi mikononi mwa CCM.

Sijalia kwa jinsi CCM ilivyotwaa Umeya na Unaibu Meya wa Kinondoni. Najua mchuano wa kimahakama utafuata. Nimelia kwa masikitiko kuona Kinondoni ikirejea kwenye mkwamo wa kimaendeleo.

Tangu kuanza kwa vyama vingi,Dar ilikuwa chini ya CCM,ikiwemo Kinondoni. Mambo yalifanyika kwa mazoea. Kodi ilikusanywa kwa mazoea. Miundombinu ilijengwa kwa mazoea. Mazoea yanarudi. Kulindana na kukwepana.

Walipoingia UKAWA chini ya Meya Boniface Jacob pale Kinondoni,mambo yalibadilika. Makusanyo ya kodi yaliongezeka. Bajeti za miradi na wafadhili vilinona. Hakukuwa,kwenye kukusanya kodi,na upendeleo wowote.

Kwaheri Kinondoni yenye kwenda mbele,karibu Kinondoni ya mazoea. Wapenda mteremko na kupendelewa kwa kulindwa wanashangilia. Mimi nalia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Wakati mwingine siasa ni afadhari kuachana nayo,maana ni kero tupu,huyo Beni sitta wanampa umeya wa kinondoni wakati kata ya msasani imemshinda? Alitoa ahadi kedekede wakati wa kampeni ila alipopata tu udiwani hakuna chochote alichofanya wala anachokusudia kufanya,na jamaa lengo lake ilikuwa ni umeya hii ipo wazi,daaah naisikitikia kinondoni
 
Umechelewa kazini! hivi na wewe kuna ofisi imekuamini hadi ikakupa kazi! Kwani wewe ni nani hadi utulilie wanakinondoni,! Kwa utashi wetu tukiamini chama cha mapinduzi na tumekipa dhamana ya kutuongoza huna haja ya kutulilia hilo ni chaguo letu tunajua tumechagua maendeleo na siyo maandamano.
 
Kwanza naomba mlio karibu na BENJAMIN SITTA mwambieni kabla hajaapishwa kuwa meya wa kinondoni atuletee msasani mpya,maana alisema ataleta Msasani mpya,na atimize ahadi zifuatazo maana aliahidi
1:Afya,alisema atajenga zahanati ya kata
2:Ajira na ujasiriamali,alisema ataunda chombo maalumu cha kutafuta misaada ya vikundi vya ujasiriamali.
Hizo ni baadhi tu ila zipo nyingi sana aliahidi...na awashukuru ukawa,maana walijivuruga wenyewe kati ya mgombea wa cuf na chadema ,na.hivo kura ziligawanyika ndipo akapita kirahisi
 
Hivi nn kimetokea mpk uchaguzi kurudiwa?
Mbina sielewi?

Kweli sikuhizi nipo nyuma
 
Umechelewa kazini! hivi na wewe kuna ofisi imekuamini hadi ikakupa kazi! Kwani wewe ni nani hadi utulilie wanakinondoni,! Kwa utashi wetu tukiamini chama cha mapinduzi na tumekipa dhamana ya kutuongoza huna haja ya kutulilia hilo ni chaguo letu tunajua tumechagua maendeleo na siyo maandamano.
ccm wezi wa kura....
 
Back
Top Bottom