barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Uamuzi uliofikiwa Na waziri katika ofisi ya Rais, tawala za mikoa Na serikali za mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kulikabidhi soko la Machinga Complex kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana mdogo Paul Makonda, ni uamuzi uliozingatia maslahi ya kisiasa kwa Chama cha mapinduzi CCM, Na uamuzi huo hautoleta tija yoyote Ile kwa wafanyabiashara wa soko hilo kwani mkuu wa mkoa sio muhusika wa moja kwa moja wa shughuli za maendeleo katika halmashauri.
Uamuzi huo ulifuata baada ya kuivunja bodi ya soko hilo, kwa madai kuwa halmashauri ya jiji la Dar es salaam imeshindwa kutekeleza malengo ya uanzishwaji wa soko hilo.
Viongozi wa CCM wamekuwa ni wanafiki kila kukicha, Na unafiki wao umekomaa kwani hapo awali kabla ya kuingia katika zoezi la Uchaguzi mkuu wa 2015, halmashauhalmashauri ya jiji la dar es salaam ilikuwa ikiongozwa Na Meya Na naibu meya kutokea CCM, pia wabunge Na madiwani wengi walitokana Na CCM, hivyo maamuzi yote yalikuwa yanafanywa Na wao CCM wenyewe. Kwa hiyo CCM wao ndiyo walioharibu au walioshindwa kulisimamia soko lile Na kutatua kero zote Na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara hata kuwapelekea kushindwa kulitumia soko lile.
Sababu za kufikia uamuzi huo nivkwasababu hivi sasa halmashauri ya jiji inaongozwa Na Chama cha Demokrasia Na maendeleo CHADEMA/UKAWA, hivyo kuna mawili yanakwepwa hapo kama sio matatu:
#Mosi: Ufisadi Na ubadhilifu uliofanywa hapo tangu kujengwa kwa jengo hilo 2010 unakwenda kufichwa, Na upo ukweli kuwa vizimba (vibanda vya biashara) vinamilvinamilikiwa Na baadhi ya viongozi hao hao watokanao Na CCM Na kisha kuwakodishia wananchi kwa kodi kubwa zaidi, nk. Hayo pamoja Na ubadhilifu wote, CCM wanajaribu kukwepa kivuli Chao.
#Pili, soko la Machinga complex ni moja ya kero kubwa kwa wakazi wa dar es salaam, Halmashauri mpya ya sasa inayoongoza jiji la dar es salaam ikiwa imejipanga kimkakati kuwaondolea wakazi wa jiji la dar es salaam changamoto hiyo kubwa ya kimaendeleo, CCM hawana PA kufichia nyuso zao kwa kuhofia wananchi watafahamu sababu iliyokuwa ikiwakwamisha kimaendeleo, hivyo kuamua kuliondoa soko hilo chini ya halmashauri Na kumkabidhi mkuu wa mkoa ambaye ni kada wa CCM, Na mkuu wa mkoa hapitishi bajeti ya halmashauri japo Ana majukumu yake tofauti Na hayo ya kimaendeleo.
Halmashauri ya jiji la DSM ina majukumu ya kuratibu Na kusimamia shughuli za uendelezaji wa jiji katika halmashauri za manispaa zote tatu, temeke, kinondoni Na Ilala. Majukumu hayo ni kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa (mamlaka za miji) Na.8 ya 1982 kifungu 69A, pamoja Na majukumu mengine, pia ni:
Muandaa mpangi mkakati kuhakikisha panakuwepo maendeleo endelevu ya jiji,ambapo kuliondoa soko hilo kwa halmashauri, ni kuliondoa katika mipango hii ya kimaendeleo kwasababu tu ya siasa.
Pamoja Na Rais kuahidi kushirikiana Na wote bila kujali itikadi, serikali ya CCM imekuwa mstari wa mbele kulinda maslahi yake ya kisiasa na matokeo yake kuwachelewesha wananchi kuoiga hatua kimaendeleo.
Simbachawene Na huyu dogo Makonda wanapaswa kufahamu kuwa, wananchi wanahitaji maendeleo kwa wakati, hivyo siasa zisizo Na tija katika masuala ya maendeleo zitalirudisha nyuma jiji ka DSM, ilhali hivi sasa halmashauri inaongozwa Na uongozi makini CHADEMA/UKAWA.
Soko hili ni moja ya "majipu" makubwa katuka jiji la Dsm ambapo Halmashauri ya Jiji na ile ya Wilaya ya Ilala ilihusika moja kwa moja katika kuufanikisha.Kuliweka mikononi mwa mkuu wa Mkoa wakati kuna uongozi mpya ambao ulijiandaa kufukua na kuuonyesha umma namna wananchi wa Jiji la Dsm waliibiwa na watawala waliokuwepo ni ukiukwaji wa dhamira ya kweli ya kuwaletea wananchi maendeleo.Nyuma ya Machinga Complex na sarakasi ya vizimba kuna ubadhirifu wa kutisha