Naisihi serikali itazame jambo la Kibiti kwa mtazamo mpana – Mhe. Zitto

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Baada ya usiku wa kuamkia leo Afisa Mtendaji kijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake wameuwawa kwa risasi katika kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti. Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameisihi itazame jambo hili kwa mtazamo mpana na wenye weledi.

zitto21.jpg


Mhe. Zitto ameyaanisha hayo leo katika ukurasa wake wa Facebook huku akisema kuwa wananchi wanahaki ya kujua nini kinaendelea huko.

"Mauaji mengine Kibiti! Usiku wa kuamkia leo Afisa Mtendaji kijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake wameuwawa kwa risasi na baadaye kuchoma moto nyumba.
Naisihi Serikali itazame jambo hili la MKIRU ( Mkuranga, Kibiti na Rufiji) Kwa mtazamo mpana na wenye weledi. Tambo za IGP na Amiri Jeshi Mkuu zinaonekana ni maneno matupu. Wananchi wana haki ya kujua nini kinaendelea MKIRU"
 
Waweke dau kubwa kwa atayetoa taarifa za kuwakamata hawa wauaji. Watasalitiana hao wenyewe kama muhusika sio mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom