Naishi na njiwa

Naishi na njiwa

Hao njiwa tausi wakoje na ni bei Gani mbegu?
Ni njiwa wazuri sana, bei zake walivyoingia walikuwa Pair ni 600,000/= yaani mmoja ni laki 3 ila kuna mahali mimi nilinunua kwa laki 3 Pair, yaani Dume na Jike huko Arusha
 

Attachments

  • images (38).jpeg
    images (38).jpeg
    50.1 KB · Views: 12
  • images (36).jpeg
    images (36).jpeg
    31.9 KB · Views: 13
  • images (37).jpeg
    images (37).jpeg
    36.2 KB · Views: 13
Kwetu hata kunguru hatui, sijui tuna laana gani

Yaani Ukiacha kitu na shombo ni Mandushi yanajazana majike kwa maume mengine Chongo, mengine chiba Yaani tabu tupu
 
Nilikuwa na hamasa sana ya kuanza ufugaji wa wanyama mbalimbali kama kuku, sungura, mbwa, paka, njiwa, na bata. Kwa hiyo, kama sehemu ya mwanzo wa safari hiyo, niliamua kununua njiwa sita. Niliwaleta nyumbani kwangu nikiwa na nia ya kuwafuga kwa ajili ya urembo tu, si kwa biashara wala kwa chakula.

Hata hivyo, sikuwatengenezea mazingira rasmi ya banda au makazi yao maalum. Walikuwa wanashinda juu ya bati na kwenye dari. Mwanzoni, nilikuwa nawapa mtama kama chakula chao, lakini baada ya muda, niliachana na shughuli zote za ufugaji kwa sababu msimamizi wangu aliondoka. Nikaamua kuuza mifugo wote niliokuwa nao, isipokuwa njiwa. Kuwaondoa njiwa ilikuwa ngumu sana kwa sababu ni wepesi na walishazoea kuishi juu ya dari – kuwakamata ilikuwa haiwezekani.

Kilichonifanya niwaache ni kwa sababu hata siwapendi kwa ajili ya chakula; sijawahi kula njiwa hata mara moja. Nilikuwa tu na wazo la kuwaweka kama sehemu ya mandhari na urembo wa nyumba. Lakini tatizo kubwa lilikuja baadaye – wameendelea kuzaana. Sasa wameongezeka na kufikia karibu ishirini. Wanachafua sana mazingira ya nyumba, wanakojoa na kunya kila sehemu – ukutani, kwenye vitu – japokuwa cha kushangaza ni kwamba kinyesi chao hakitoi harufu kali. Wanachafua tu.

Nimejaribu njia mbalimbali ili wahame kama kutowapa chakula wala maji – lakini wamegoma kuhama. Nyumba yangu ipo mbali, imejitenga, kwa hiyo hawana sehemu nyingine ya kwenda. Kwa ratiba yangu ya maisha, natoka asubuhi na kurudi usiku, na naishi mwenyewe, hivo sina nafasi wala muda wa kuwashughulikia.

Nimeamua kuwaacha hivyo hivyo. Labda niwalete kama walinzi wa anga – maana hawasumbui zaidi ya uchafu tu.
fuga paka
 
Back
Top Bottom