Naipenda sana CCM, hutaki acha

Naipenda sana CCM, hutaki acha

Ushawahi ona mvuta sigara akaiponda, hata aambiwe vipi madhara yake bado ataisifu na kuienzi.
Hiki ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wanyonge.maskini na walalahoi. Nawashauri Watanzania mliodanganyika na wapinzani, muondoke huko.

Hao ni walaghai na mabaka uchumi.

CCM daima
 
Hiki ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wanyonge.maskini na walalahoi. Nawashauri Watanzania mliodanganyika na wapinzani, muondoke huko.

Hao ni walaghai na mabaka uchumi.

CCM daima

Mkuu umeandika maneno machache lakini ya busara mno. Mungu akuzidishie hekima na busara.
 
Yaliyosemwa yanatosha kwa kweli ila siwezi pita hivihivi, posho imeongezeka siku hizi?
 
Imekuwa ccm tena na sio act? hahahahahahahaaaa.
 
hiki ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wanyonge.maskini na walalahoi. Nawashauri watanzania mliodanganyika na wapinzani, muondoke huko.

Hao ni walaghai na mabaka uchumi.

Ccm daima

.mimi siipendi ccm kama nishivyompenda shetani na nilisha aacha zamani sana...!
 
naipenda ccm.hakuna asiyofadhiliwa na ccm .zaidi yanayokuja ni ulaghai tu.mmesoma mejenga mnajidai.Neema zinawasumbuwa.kuchamba kwingi kushika mavi.
 
Hahahahhah eti kaa kimya uheshimiwe....mbona ulivyoandika pumba zako juu ya kukipenda chama chamatumbo huku kaa kimya?
 
CCM imeingiwa hofu, Magufuli kuwa shughuli

KUNA hofu imetanda ndani ya CCM; hofu ambayo inajaribu kufichwa mapema kwani kama mambo hayatobadilika ndani ya miezi hii mitatu hivi iliyobakia kabla ya Uchaguzi Mkuu basi chama hiki kikongwe zaidi nchini kinaweza kujikuta kikipumzishwa kutoka madarakani kwa nguvu. Dalili ya hofu hii imeonekana baada ya kutangazwa kwa mgombea wao wa kiti cha Urais Dk. John Pombe Magufuli.

Mojawapo ya mambo ambayo yametokea baada ya Magufuli kutangazwa ni kauli za kuwa yeye “anakubalika na anachagulika”. CCM imetaka kuliaminisha taifa kuwa Magufuli siyo tu anajulikana kwa utendaji kazi wake, na kuwa wananchi wengi wanampenda na wanaweza kumchagua. Kiasi kwamba wametaka watu waamini kuwa Magufuli ni Rais anayesubiria (President in waiting). Kwamba, upinzani hauna nafasi hata kidogo ya kumnyang’anya uwezekano huo.

Ukweli ni kuwa matendo ya CCM hayaoneshi kujiamini huku. Kama kweli CCM inaamini Magufuli anajulikana na kazi zake zinakubalika nchi nzima kwa nini juhudi kubwa sana inajaribu kufanywa ya “kumtambulisha”. Unamtambulisha vipi mtu ambaye tayari unaamini anajulikana, kufahamika na kukubalika? Ukiangalia utaona kuwa CCM inataka kumtumia Magufuli kukibeba chama; tatizo ni kuwa Magufuli mwenyewe – ukiondoa kukariri kwake takwimu mbalimbali – utendaji kazi wake una shaka. Tayari wizara ambayo amekalia imeshagubikwa na kashfa lukuki na hili peke yake lingetosha hata kumchafua. Akija mgombea mzuri kutoka upinzani na akajizibu hizi takwimu za Magufuli, basi Magufuli na CCM iko matatani. Yote haya yanatosha kufanya watu wajiulize mara mbili kama kweli Magufuli hatokuwa shughuli kweli kweli.

CCM imepasuka, rekodi yake mbovu, na upinzani ukimsimamisha mgombea makini, Magufuli ataweza vipi kushinda? Njia pekee ya kushinda katika mazingira ya namna hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu, vyombo vya dola na hata kuliingiza jeshi katika siasa kama walivyofanya chini ya Jenerali Shimbo mwaka 2010. Vyovyote vile ilivyo hata hivyo kuna hofu imetanda kwa CCM; hofu kama vile wingu zito la mvua lenye dalili ya radi na ngurumo. CCM hawajui sasa wafanye nini zaidi ya kuombea Magufuli aweze kuwaokoa. Akishindwa je Hili ndilo swali la kuogopesha zaidi kwa kila mwana CCM

Chanzo: Raia Mwema (22, July 2015)
 
Haya CCM tuambieni utamtamhulishaje mtu anayejulikana???
 
Back
Top Bottom