Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

View attachment 1126622

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE.
Nilimsimulia mama Karisa mkasa mzima, jinsi ambayo nilikutana na kashkash za polisi, jinsi ambayo safri yangu ya Dar es salaam ilikuwa nzuri na tayari ninalo gari na liko kwa mama mdogo, Nikamuelezea pia jinsi ambayo tulisoka out na mr lakini hakuna kilichoweza kurekebishika.
Simpendi tena baba Davis, simpendi… Nilimwambia Mama Karisa.
Hivi wee mama Davis una laana? Nani alikuwambia mume anaachwa? Usiache ndoa yako, wee danga tu lakini ndoa usiache,
Sisi tunadanga lakini hatuachi Ndoa, sasa unataka kuachana na mume unafikiri Fadhili atakuoa? Hakunaga mwanaume anao mke wa mtu,
Wewe unakaa kwenyendoa yako, ili mradi umepata mwanaume wa kukuridhisha,
Wewe unafikiri Baba Davis alishindwa kumuuoa Sarah?
Unafikiri mimi nimeshindwa kuachana na baba Karisa?
Diaaa ananipa kila kitu, lakini umeona nikiacha ndoa yangu? Una nini wewe?
Hembu rudi kwako acha ujinga,,
Mama Karisa aliniambia lakini bado nilikuwa nawaza nitarudije sasa?
Sikia,, unataka kuachika kweli? Aliniuliza,,
Ndio, sitaki tena kuishi na Baba Davis, wacha niishi peke yangu..
Ha ha ha ha,, haloo naona Fadhili sijui kakulambisha, nini.. Mungu wangu?! Wewe mama Davis serious?
Hembu ngoja kwanza,,,
Mama Karisa alichukua simu yake kisha akampigia Fadhili ,,,
Haloo.. wewe mwanaume balaa gani hili unalilleta?
Mama Karisa alikuwa anaongea na Fadhili.
Yani huku kimwana hataki kabisa ndoa,, umemfanyaje?
Sikusikia maneno aliyokuwa akijibu Fadhili lakini ni kama aliyekuwa akicheka na kufurahia tu.

Alikata simu na kuniambia,,, Sikia mama Davis, usimuache mume wako, usimuache kabisa, ila kwa vile umepata mwanaume , anayekupenda, anayekufikisha na kukpatia pesa mimi naona tulia kwenye ndoa yako tu mamii, Tulizana maisha yasonge.
Mama Karisa alinishauri sana,
Lakini nikawa nawaza narudije nyumbani?
Nilimkera sana baba Davis, narudije?
Lakini upande mwingine nilishatamani kuishi maisha yap eke yangu.

Ni saa kumi na mbili jioni bado tunaongea,
Nitalala wapi?
Itakuwaje? Nitaenda wapi?
Bado sijajua
Mama Karisa aliniambia, ngoja niongee na mume wako, ngoja niongee naye
Mh.. niliwaza jinsi ambavyo baba Davis asivyompenda Mama Karisa,,
Nikamwambia noo labda ongea na mdhamini wangu wa ndoa, hembu ongea na Tilda, maana nilikuwa naye labda mtaelewana,,
Nilimuomba mama Karisa aongee na Tilda,
Mh.. Yule mwanamke mimi sinaga mazoea naye, sipendi wanawake wanaojidai wanajua Mungu, ni wanafiki balaaa,
Mama Karisa alisema,, kwa hasira na dharau juuu..
Noo ongea naye tu, ongea naye hana shida,, hembu ongea naye..

Nikupe namba zake?
Ndio hembu nipe,, ila Yule mama anakuwaga na nyodo Fulani za kipuuzi , akinionyesha nyodo nitamtukana atajuta,,, Mama Karisa alisema akiwa kashalewa…
Nilimpa namba na akaipiga..
Hallooo.. Haloo Tilda aliitikia…
Bwana Yesu asifiwe,,, Mama Karisa aliisema hiyo Bwana Yesu asifiwe akiwa ananifinyia jicho kwa kejeli…
Amina mpendwa, Bwana Yesu asifiwe sana,,,, nani mwenzangu? Tilda aliuliza baada ya kuitikia salam kwa kurudisha kama alivyosalimiwa.
Unaongea na Conso, rafiki wa Mama Davis,,,
Ndio , nikusaidie nini? Aliuliza Tilda,,
Niko na mama Davis hapa, nilikuwa naomba tuongeee…
Enhe,, Tilda aliitika.
Mama Karisa alinitazama na kunionyeshea aongee nini? Baada ya Tilda kumwambia enhe…
Zilipita kama sekunda kumi na tano hivi..
Kisha Tilda akasema,, Haloooo, haloooo.
Haloooo,, Mama Karisa aliitikia, huku akiwa hajui aseme nini,, kisha akasema,, Unaweza kuja hapa tulipo? Mama Karisa aliongea…
Tilda alimjibu,, samahani dada, mimi sio mwanamke wa baaaa….
Mama Karisa alisonya na kusema, nyoooo.. nyie ndio wachawi,, huji maana yake nin,, ndio maana mnakufaga na ukimwi mkijiona watakatifu sana,,.. Mama Karisa alianza kubwatuka,, na nikampokonya simu ambayo bado ilikuwa hewani na nikaikata..
Unaona hizi ndizo shobo sizitakagi.. sasa atajuta,, huyu ni mpuuzi nini, eti sio mwanamke wa Baaa,, ..
Mama Karisa aliendelea kulalamika, nilisikitika sana na kujilaumu, lakini sikuwa na namna, nimeshaharibu.
Simu yangu ilikuwa inaita,,, niliitazama ni Tilda alikuwa anapiga,,
Nilisimama na kwenda kuongelea pembeni,
Mama Davis ni wewe? Ndio nilijibu,, umempa nani namba yangu? Mama Karisa,,
Nilimjibu,,
Umekosea sana, nikuombe tu usiwe unatoa namba zangu bila ridhaa yangu,, uko wapi? Tumekutafuta sana?
Aliongea Tilda,
Nipo,,, nilimjibu.
Upo salama? Ndio niko salama.
Yani Tilda aliongea na mimi kama hajatukanwa, nilishangaa sana.
Kuna hali Fulani moyoni iliniingia,, ya huruma na kutamani sasa kumsikiliza Tilda,
Yani Tilda akikubali kuongea na mimi sasa hivi nitamsikiliza, Mungu wangu.
Wakati naendelea kuongea na Tilda, huku nikimueleza mahali nilipo, Aliniomba sana kama naweza niende nyumbani kwake tukamaliza hili tatizo langu.
Sikia Mma Davis, naomba kama hutajali hembu uje nyumbani, tuweke haya mambo sawa, Baba Davis ameshapiga simu nyumbani kwenu nataka kabla kikao cha familia hakijakaa niweze kukuambia maneno machache, nitasafiri wiki ijayo kwenda Lethoto kikazi hivyo nitakuwa na mambo mengi sitapatikana na sitakuwa na muda hivyo fanya juu chi ni uje tuonane leo tuongee, kesho nasafiri kikazi Dar es salaam.
Tilda aliniambai kwa pole pole sana.
Dah,,
Nilikuwa tu nimesimama naongea na simu bila kujua kama nyuma yangu kuna mtu,
Nilishtuka sana kuona mtu ananikumbatia kwa nyuma..
Mungu wangu,, nilishtuka na kusema…
Uwiii ni Fadhili… niligeuka na kumkumbatia,, hii Diaaa
Mambo mamsup wangu… Fadhili alinisalimia.
Salama,,,
Pole na jana, pole sana mpenzi.. aliniambia.
Ni nani alinitukana jana? Ndio maana nikakuomba msamaha mpenzi, Fadhili aliniambia.
Kisha akanishika mkono na kuelekea alipokuwa amekaa Mama Karisa, na tukakaa ,
Sikuwa najali tena muda wala kitu, sijui roho gani imeniingia.
Tuliendelea kuongea na kuweka wazo langu mezani la kupatiwa nyumba na Fadhili
Tilda kashaniomba nikaongee naye na kesi imeshafika kwa wazazi, namfahamu mama yake baba Davis, ni mjeuri nahanipendi, najua tu sina ndoa hapa najua tu,
Niliwaza moyoni,
Sasa nisije nikakosa yote kwa pupa, wacha niongee an Fadhili nimalizane naye kabisa, nikienda kule liwalo na liwe,, nisije nikakosa bara na pwani buree.
Nilijisemea..
Unataka kuniambia Unatamani kabisa kuaanza maisha?
Ndio, ninatamani kuanza maisha,,, nilimjibu Fadhili.
Oky am ready mpenzi,, ninavyokupenda nakukataliaje?
Ila tu ni lazima tutawekeana mikakati, kwa sababu nina wivu hasa, sitataka kuona unarudiana na Hitla, maana nina mpango wa kukupendezesha hasaaa, sasa ukianza kung’ara alafu uje uniambie ooo mpenzi unajua, chapanda cha shuka sitakuelewa ujue ..
Fadhili aliongea kwa kumaanisha,
Na ujue nitatumia pesa zangu, muda wangu na mapenzi yangu kukufanya ujisikie mwanamke hasaaaa,
Sasa kabla sijafanya lolote nihakikishie kabisaaa kwamba unaachana na mumeo
Ndio wala sina haja naye, mateso niliyoyapata miaka yote yanatosha.
Okay mpenzi,
Basi hakuna shaka,
Ila kwa kipndi hichi nitaomba uwe makini kidogo mke wa mtu wewe,,
Tutakuwa tunakutana kwa siri sana, na pia hakuna kupigiana simu, kama nikikuhitaji nitakuwa nampigia Conso alafu anakupa ujumbe umesikia mpenzi?
Ndio nimesikia,
Sawa,,
Uwe na amani… take good care of urself..
Fadhili aliniambia hivyo,
Kisha akamuita mama Karisa akaongea naye pembeni na kuondoka,
Sijui hata alimuambia nini.
Lakini aliongea naye, sikupenda lakini nifanyeje.
Kasemaje? Nilimuuliza mama Karisa,, kasema anaenda mahali anarudi.
Mama Karisa alinijibu kilevi na akaondoka.
Sikuwa nimekunywa pombe kabisa, kwa sababu usiku wake nilikunywa pombe nyingi sana na nilijutia pombe nilizokunywa usiku ule.
Ambazo zilipelekea nikafanya maamuzi ya kufanya ngono bila ridhaa yangu.
Hivyo sikunywa kabisa pombe.
Watoto sijawaona, kazini sijaenda, kwangu sipo,, nilikuwa ninamambo mengi sana kichwani.
Niliwaza kumpigia Thea simu.
Lakini akiliingine ikaniambia acha kwanza, hembu nenda kwa Tilda. Niliangalia saa yangu ya mkononi ni saa tatu usiku.
Mh.. naendaje kwa watu usiku huu? Nitasema nimetok a wapi?
Ama niende boma kwa mama?
Niliwaza mambo mengi kwa wakati mmoja.
Ndio bora nirudi boma kwa mama,Watoto sijawaona, kazi je?
Potelea mbali, Fadhili yupo atanisaidia, ngoja nifuatilie swala moja kwanza,
Wacha niende kwa mama.

Mama Karisa aliniambie sema shooo,,unaenda kwa Mama mchungaji wako ama?
Maana mimi nikitoka hapa naenda nyumbani kulala,
Kama vipi twende kwangu.
Afadhali kumbe naweza kwenda kwa Mama Karisa eee,
Okay, good,,Sawa twende tu kwako nikapumzike.
Sawa,,
Tuliwasha gari na kuondoka, na kuelekea nyumbani kwa Mama Karisa,
Tulifika na tukafunguliwa geti na mdogo wa kiume wa mama Karisa, na tukamkuta mume wake amekaa sebuleni anaangalia Television, na mdogo wake mama Karisa wa kiume .( Yule ambaye aliyetufungulia geti)
Habari shemeji? Nilimsalimia,, Salama kabisa shemeji karibu.
Asante,, nilipita na kukaa kwenye kochi.
Kisha mama Karisa naye akamsalimia mumewe,
Baba Karisa mmeshindaje? Salama..
Yani gari leo imenisumbua hatari,, nilikuambia rejeta mbovu hukusikia,, mama Karisa alimlalamikia mume wake…
Nilikuwambia lakini ni ya kubadilisha ukasema unaondoka hivyo hivyo.. baba Karisa alijibu..
Wakati huo alikuwa akielekea chumbani.
Alikaa kidogo chumbani kisha akarudi na kumuita, Dadaaa.. dadaaa msichana wake wa kazi,, umepika nini?
Kabla dada hamtazama, akaniangalia akaniambia,, utakula ama uumeshiba?
Niiijibu tu nimeshiba.
Haya uje nikuonyeshe pa kulala.
Aliniingiza chumbani anakolala watoto na kunimmbia utalal hapa,,,
Daadaaa, sogea ulale na mama Davis,, sogea,, aliongea kilevi kisha nikatoka kumuaga baba Karisa usiku mwema na kuelekea kulala.
Nilijitupa tu kitandani na kwa sababu nilikuwa nimechoka sana, nilipata usingizi wa ghafla mzito sana.
Na nililala sana.
Nilishtuka saa kumi na moja asbh wakati dada wa kazi wa mama Karisa akiamka.
Msichana aliamka na kuanza kuwaandaa watoto shule na kufanya usafi,
Nilikuwa tu kitandani nimejiegemeza nawaza.
Nilichokuwa nakiwaza ni kitu kimoja tu,
KUPANGISHA NYUMBA YANGU NIANZE MAISHA MAPYA.
Kupatiwa biashara na Fadhili.
Niliisikia ile sauti ya Fadhili masikioni mwangu tena ikiongea.
“Na ujue nitatumia pesa zangu, muda wangu na mapenzi yangu kukufanya ujisikie mwanamke hasaaaa,”
Bahati haiji mara mbili… bahati haiji mara mbili.
Nilijikuta nikiwa na furaha moyoni.
Kama kaweza kuninunulia gari mpya, nzuri, kama ameweza kukaa na mimi hotelini, Ananipenda, na ninajua atanipa vitu vingi vizuri na kunitengenezea maisha,,
Najua. Sipotezi hii bahati, sipotezi,, siipoteziii. I LOVE YOU FADHILI.
Nilijisemea kimoyoni na kutabasamu.
Shoga umeamka salama? Mama Karisa alinisalimia.. ndio.
Haya oga basi,, sijajua ratiba zako, unaenda Boma kwa mama ama tunaenda dukani ama unaenda kwako ama unaenda wapi?
Hembu kuwa mtu wa maamuzi.
Aliongea hivyo mama Karisa bila hata kujali, mume wake alikuwa sebuleni nay eye wakati akiniambia hayo alikuwa akitafuta viatu vyake vya kuvaaaa…
Mama Davis sema basi,, umeamuaje?
Nilimjibu naenda Boma..
Okay sawa, basi jiandae nikurush stand.
Alimaliza kusema hivyo na akaondoka kwenda kujiandaa.
Mume wake aliniita na kunisalimia kisha akaondoka.
Baada ya kujiandaa tuliondoka na alinishusha stand na nikapanda basi la kuelekea Boma kwa mama.
Hata sikujua naenda huko kufanya nini.
Sikuwa na muongozo wowote ule.
Lakini nikaona tu wacha niende kwa mama ndipo penye usalama.
Ungeniuliza hata naenda kufanya nini sikuwa nina jua.

…. Nashindwa kukutetea, hupokei simu, hujibu msg,,, unacheza na kazi nini kimekupata?
Ni ujumbe wa simu kutoka kwa Thea…
““Na ujue nitatumia pesa zangu, muda wangu na mapenzi yangu kukufanya ujisikie mwanamke hasaaaa,””
Haya maneno yalijirudia tena , na kuisikia sauti ya Fadhili masikioni mwangu.
Wala sikujali,,
Hata kama Fadhili hatanipa pesa, nitauza hii gari nitaanzisha biashara, mbona biashara za kufanya nyingi tuuuu.. nilijisemea moyoni.

Nilishuka stand na huyo nikaelekea kwa mama

ITAENDELEA
Huyu mama dii huyu na kazi hakumbuki chaaaaa
 
Huyu mama dii huyu na kazi hakumbuki chaaaaa

Yaani ni janga huyo na alivyo hana chake cha kumuingizia pesa.. ni sijui yukoje.. eeeeh anatia aibu kuzidi kutegemea kudanga ndio apae.. badala ya kuchuma pesa sasa hivi akaanza kujiwekea anafikiria kuomba omba eeeeeeh

Fadhili kashampa yake.. Moses afie tu huko tusimsikie tena ha ha haaaa.. ila nani alimuona nae.. Moses atatumia ujanja kumpa Fadhili vidonge vya kumponda huyo mama d.. kazi ipo
 
Yaani ni janga huyo na alivyo hana chake cha kumuingizia pesa.. ni sijui yukoje.. eeeeh anatia aibu kuzidi kutegemea kudanga ndio apae.. badala ya kuchuma pesa sasa hivi akaanza kujiwekea anafikiria kuomba omba eeeeeeh

Fadhili kashampa yake.. Moses afie tu huko tusimsikie tena ha ha haaaa.. ila nani alimuona nae.. Moses atatumia ujanja kumpa Fadhili vidonge vya kumponda huyo mama d.. kazi ipo
Hana akili huyu mwanamke jamani
 
Thanks, tunajifunza mengi kupitia hii hadithi, ila mimi najiuliza mama dii ataishia wapi na Bwana mfadhili, ngoja tuone
Ninachokiona, ataachwa mda si mrefu maana ana hamu ya kujimilikisha Fadhili na kuisahau familia yake. Na lazima atajuta kuwa na mahusiano na Fadhili kiasi cha kutelekeza hadi familia yake, majuto ni mjukuu.
 
Namuhurumia sana Mama d, wanaume ni waongo sana,asifikiri fadhili atampangia nyumba atampiga danadana mwisho wa siku anambwaga mazima, uwiiiiiii.
 
Yule dogo nae....bora angejipigia tu siku ile.....kahaba marino lilishaingia line kabisa........angalia moses....changu limejipeleka akafanya yake kwisha.........ila inaonekana watakuja kumpiga MTUNGO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom