Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
Salamu kwenu wote
Eid Mubarak
Leo sikukuu tena, hakuna kulala usiku/asubuhi hii nipo natoka Msondo Ngoma.

Inasumuliwa na Irene Mbowe. (Inaanzia sehemu ya kwanza na kuendelea, fatilia uhondo moto moto. Jadili hadi uchoke kumekucha.

********************************

FB_IMG_1559779778596.jpg


SHUHUDA NAIPENDA JUMAMOSI YANGU.
Shikamoo dada Irene.
Naomba na mimi nitoe shuhuda yangu juu ya Naipenda Jumamosi yangu.
Naitwa Marino. Ni mama na Mke. Nina watoto 3.
Niliolewa mwaka 2009. Nina ndoa ya miaka 10 sasa.
Nimeishi ndoa ya mateso na masumango sana kwa muda mrefu. Nimekuwa nikilia kwa takfibani miaka yote .Mpaka siku moja mwaka 2015 nilipoambiwa nikufollow. Nilianza kukufolow na sikuona kitu cha kunisaidia wakati huo. Nilikuwa nakusoma lakini sikuona kitu cha kumisaidia.
Nafikiri ni kwa sababu moyo wangu ulikuwa na uchungu na majeraha.
Irene Unaolewa ukiamini kabisa una mwenza wa ndoa ambaye atakuwa na wewe. Lakini ajabu ni kwamba unakuwa na Adui ndani ya nyumba.
Lakini hata hivyo unajipa moyo kwa ule usemi usemao ,
ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kuna teketea. Ni usemi ambao najifariji nao.
Lakini kuna uwezekano kwa we.zako ndiko kuna ungua kwako kunateketea. Ninawaza hayo.
Siku zinazidi kusonga bila mafanikio yoyote.
Kila unagejaribu kumwambia juu ya Ndoa yako na matatizo anakupa majibu.
Nakumbuka sasa nikaona aliyeniambia msome Irene Mbowe nimamuona hafai na nikaachana na kusoma.
Ni siku ya jumapili nakutana na Mama Karisa. Namuambia juu ya Ndoa yangu na Kuamwambia juu ya Kumsoma Irene Mbowe.
MamaKarisa anatabasamu kisha anaachia cheko refu na kusema Huyo Irene Mbowe yeye ndoa yake salama ama?
Anaongea kwa kumaanisha sana. Na Ili kunivunja moyo kabisa Akaniambia,Irene Mbowe mwenyewe ndoa imemshindaga kitambo ni mfamaji na Mume aliye naye sio mumewe ila alichukua mume wa mtu. Kalava baho. Bwana aliyenaye ni mume wa Mtu. Ama hujui makungwi wanaongoza kuachika?
mh...Nimahisi kama kweli. Maana mama Karisa anaongea kwa kumaanisha na kuonyesha Anachokiongea ni kweli.
Nikamuamini sana kutokana na kusisitiza kwake.
Lakini kweli.. Makungwi ni wanawake wa ndoa nyingi.
Lakini kweli, Makungwi wengi wanaachika na hawana ndoa.
Bila shaka huyu Irene naye ni Muhanga na ndio maana ndoa ikamshinda na.sasa ako na mume mwingine.
Sasa Naamini hili na halina ubishi. Naamua kuachana na Kinamkera Irene Mbowe.

Sasa nafanyaje?Namhoji Mama Karisa.
Anisaidie Kupata majibu ya Ndoa yangu.

Sikia mwanamke,Amka usingizini. Ndoa ili idumuazima ujiongeze. Kama mume anakunywa bia kunywa whyski. Kama anakunywa whyski kunywa bia.
Akicheua bia cheua wine,Lazima ndoa iwe nzurii
Mama Karisa anatabasamu na kunitazama.Huku anabana nywele zake vyema. Na Kuniambia mimi natoka.
Ni majira ya mchana kuelekea saa tisa. Namtazama akiwa anatembea kutoka nje . Nami nasimama kutoka nje kumfuata.
Nabakije ndani kwa mtu?
Dadaaaa... Mama Karisa Anaita, Mshefa akija mwambje na mimi ndo nimetoka. Yani muda Naoingia mwambie mmepishana na mama. Sawa?
Mama Karisa anamaliza kumpatia Maelezo Msichana wake wa kazi yani House geli.

Mama,Lakini Karisa Ana moto na Ana jipu mama.
Msichana anatoa maelezo.
Mama Karisa Bila Kujali anasema,Mpe panado moja akiamka.
Kisha ananiambia twende mama.

Namfuata nje na Anaongea na Simu nikiwa nasikia.
...Sema mpenzi... Ndio nakuja hivyo.
Mama karisa anaongea kimahaba.
Mh...Hapa anaongea tu na mwanamume.
Anakata simu na kuitisha Taksii.
Baada ya Muda Taksii inafika na Ananiambia, Nisindikize.
Kwa vile sikuwa napa kwenda naamua kumsindikiza.
Haooo mpaka tunafika Mjini . Anaelekezwa mahali pa kukutana. Tunachukua Taksii ingine haoo tunaanza safari kuelekea Sakina.
Tunafika sakina kituo cha mafuta tunashuka hapo na baada ya dakika chache Inakuja gari ya landcru
user zitumikazo kubebea watalii na ndani kuna mwanaume mmoja tunamsalimia kisha mwanaume huyo anamkumbatia mama Karisa na kumpiga kibao cha makalio kisha tunapanda haoo tunaondoka.
Tunaingia ndani ndani na kukuta Bar moja iko ucho joroni sana.
Tunakuta watu lakini sura ngeni. Ni Bar iliyo changamka sana.
Tunakaa hapo na kuanza kunywa.
Mimi sio mnywaji kabisa. huwa naonja tuu .
Nikaagiza Savanna yangu nikaanza kunywa.
Wakati nakunywa mama Karisa akaniambia wanakuja.
Nikabaki peke yangu. Ni saa kumi na mbili jioni.
Walikaa hasa. Sijui walipokuwa lakini nilijua tuu wako sehemu Wanadinyana. Waliporudi dalili zote za Kutoka kudinyana niliziona. Na walikuwa wamejiachia sana.
Nilikuwa natafakari mambo mengi.
Mama karisa anaonekana mwenye Raha sana. Mume wake namfahamu amezaana mwanamke mmoja. Lakini mama Karisa haonekani kusononeka japo anajua.
Ahaaaa... anapakuburudisha moyo wake.

Natafakari nikiwa pale. Kisha simu yangu inaita. Ni saa moja usiku. Ni Mr anapiga. Niliitazama nikasema uwiii,
Mama Karisa akiwa kalewa akamiambia uwii nini?Akanipokonya simu na Kuizima.Kisha akaniambia Tulia wacha kujitesa. Yeye kamaliza yake ndo anakutafuta?Kashamalizana na.wanawake zake hukoo ndo anakutafuta saaa hizi?Mchana wote mbona asikupigie kama anajali kweli?
Mama karisa alikuwa anaongea kilevi.
Nilikuwa naogopa sana. Sijazoea kukaa nje usiku.
Nikamuomba simu nipige.Akaniambia,Sikia,Kama vipi nikuitie Taxi.
Nilikuwa naogopa.
Sikuwa na amani Tena.

Diaa,Mama karisa alimtazama yule mwanaume na kumuita Diaa,Kisha akamwambiaNaomba tumrush huyu mwanafunzi Hapo aende maana ishakuwa msala.

Yule mwanaume akiwa kamkumbatia Mama karisa akamwambia, Diaa nina hamu sana na wewe. Wacha nimuombe Fadhili ampeleke.
Sawa. Mama Karisa aliitika.
Fadhili akaitwa kisha nimaondoka
kwa gari ile ya Utalii.
Ni saa tatu usiku .Niliwasha simu yangu na hapo hapo zikaingia msg nyingi sana. Ni za mr.Msg ya m
kwanza ilisema,
NITAKUUA LEO. MALAYA MKUBWA WEWE. BAKI HUKO HUKO.
Msg ingine, ikasema,
Wewe malaya unaniximia simu?
Kwangu leo usiingie
Utakuta mabegi yako nje.
Uko wapi wewe Mmbwa?
MUNGU WANGU! Nifanyeje?
Moyo ukanipasuka paaaa.
Dereva akaniangalia akasema,
Mamii mbona kama una mashaka sana?Aluliza..
Nilianza tuu kulia.
savanna 5 nilizokunywa zikayeyuka zoote.
Uwiiiii.
Nishushe hapa,Nishushe.Niliomba kushushwa.
Ni kama nusu km kutoka niliposhushwa mpaka nyumbani.
Nisijue Mr ananiona nikkshushwa.
Akajikausha misijue.
Nikawa nakazana ajabu kutembea. kama nahisi nipae.
Nikafika nyumbani. nikaingia ndani na kuchukua mswaki kwanza.

ITAENDELEA SEHEMU YA PILI. (Post #2)
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
FB_IMG_1559779817977.jpg


Nikiwa sina hili wala lile,Nilisbtuliza mlango wa chumbani unabamizwa kwa nguvu,Mungu wangu nilinisemea.
Baba Davis hakuwa na mswalie Mtume.
Moja kwa moja alinifuata bafuni na Kunivitia nje,Kabla sijakaa sawa nikiwa nashangaa alinirushia mabao ya mfululizo,Huku akionekana mwenye hasira sana.
Niambie kwa nini ulizima simu na kwa nini hukupokea simu yangu na ulikuwa wapi na ni nani alikuleta akakushusha njiani,
Ni maswali mengi kwa wakati mmoja.
Maswali yote nina majibu yake. Lakini naanzia wapi kumjibu,Utaniua Bana Davis,Utaniua mume wangu.
Ndio nitakuua... Umalaya umeanza lini?
Hapo alishachukua mkanda wa suruali na ananichapa nao.
Uwii nakufa,Unankumiza baba Davis.
Nalia kwa nguvu na Kafunga mlango wa chumbani. Nilikuwa napata maumivu sana.
Baba Davis nanipiga hivi,kweli?'Yeye akirudi saa tisa usiku nani anampiga?Yeye akilala nje nani anampiga?

Nilikuwa nimekaa chini sakafuni nikiwa nawaza nimjibu nini. Niambie aliyekuleta na kumushusha pale kona ni nani?
Sijaja na mtu,Nilikuwa nimepanda Toyo. Nilimjibu bila kujua aliniona. Nikamwambia nimepanda toyo.. Na nikaapa kabisa.
Mh... aliguna na kuniambia,bado sijakupiga. Utaniambia ukweli leo.
Sasa amua ,Unamtaja aliyekuleta ama Unaondoka?
Wacha niondoke,Wacha niondoke.
Alinyanyua mkanda kwa hasira akanichapa nao rwaachu.. bahati mbaya bakoli ikanivonga puani damu zikaanza kutoka.
Ndipo akaogopa na Kuniacha.
Akatoka nje akawasha gari huyoo.
Hapo ni saa sita usiku.
Nilijiangalia kwenye kiyooo nilivyovimba,animeumia na kuvilia damu hasaa. Nililia sana.
Wakati huo dada na Watoto wamejifungia woote chumbani wako kimya.
Nianzie wapi?Huyu akirudi anarudije?Si atanipiga zaidi?
Niliwaza haraka na nikasema wacha nifuate simu yangu ili nipige kwa Mamdogo wangu.
Nilifuata simu yangu na kuchukua kisha nikapiga kwa mamdogo kumwambia naenda kwake maana nimepigwa sana. Ama la basi aje.
Mamdogo alishtuka maana nilipiga picha madamu yalivyonitapakaaa.
Baada ya Lisaa limoja mamdogo alifika kwangu. Sijui alipata wapi usafiri lakini alitoka Bomang'ombe mpaka Kimandolu ndani ya Lisaa limoja tuuu.
Geti liligongwa na nilishangaa ni mama mdogo.
Mungu wangu,Mama Davis?Mbona umeumia hivyo?Nilikuwa nimevimba sana. Mwili mzima kwa alama za mikanda.
Mamdogo akanibeba na gari aliyokuja nayo hadi hospital. Kufika huko wakatukataa wakasema mpaka PF3,Ikabidi nikatae maana sikuwa nataka kesi. Mamdogo akasema noo. Lazima maana hutatibiwa. Mwisho nikakubali nikaandika maelezo tukapata PF3 Na kwenda kupata matibabu. Baada ya kutibiwa nikaambiwa lazima nilale hospital.
Nikalala na mamdogo.
Yule.dereva akalala guest.
Huku nyuma baba Davis alienda nyumbani akiwa kalewa sana na akalala. Binti wa kazi aliniambia.
Asbh sana Mr akiwa anaelekea kazini alimamatwa na mapolisi kwakosa la akunipiga.Akapelekwa lokapu akafungiwa huko.
Nikiwa hospital mama mkwe akaniandikia msg na akaniambia, "Umalaya wako ndio unasababisha mwanangu ateseke"
Nilishangaa sana mamaanakuwaje hivyo. Kwa nini atumie lugha hiyo mapema kiasi kile. Bila kunipa pole na kutaka kujua kilikoni
*******************
Mume alikamatwa na kuwekwa kituoni. Bado nilikuwa hospital. Saa tisa jioni nikaruhusiwa kutoka. Nikatoka Nikapita nyumbani kuchukua nguo na vitu vya muhimu. Kisha huyoo kwa mama mdogo. Wakati huo mume yuko polisi. Anashukiliwa huko. Alilala lokapu siku tatu bila huruma kabisa.
Mama yake ndiye aliyekuja na akawa akimhudumia. Na baada ya hapo ikabidi nirudi na kikao kikae ya kwamba tupatane. Tukapatakana. Lakini moyoni nina jeraha kubwa sana. Ni kama nina kidonda ambacho hakijapona kabisa. Maumivu niliyokuwa nayo hayakuwa ya kawaida.
Mama Karisa nilimuelezea kila kitu juu ya kipondo kile. Alisikitika sana. Na aliniambia nisijali kila kitu kitakwisha. Aliniambia nivumilie kwa muda mambo yatakuwa shwari.
Niliporudi safari hii Mama Karisa akawa rafiki mkubwa na wa karibu sana. Na akaniambia unashutumiwa kwa kosa ambalo hujafanya.
Mama Karisa aliniambia nakosa mapenzi na upendo.
Akaniambia wako wanaume wenye kujua kupenda na kubembeleza mwanamke. Si kama Baba Davis ambaye ana.roho ya kinyama. Nikaona ni kweli. Kwa sababu mama Karisa ninaahuhudia jinsi anavyopendwa na yule baba.
Mh... Nitapata wapi mpenzi?Nawaza. Baba Davis anajidai mjanja sana. Nitamnyoosha. Niliwaza akilini.
Anafikiri kuwa na mahusiano lazima kurudi usiku eeee. Hanijui. Sasa nitarudi saa kumi jioni na nitakuwa na mpenzi.
Nilianza kutamani kuwa na mpanzi. Kweli ukitembea na fisi unakuwa fisi.
Siku ile nilipotoka pale Bar Fadhili alinidrive mpaka kona. Alikuwa akiniambia ananipenda. mh.
Simjui vizuri lakini ni mwanaume ambaye nilitamani sasa kuwa naye.
Mama Karisa asijue nawaza nini akilini akaniambia,Hivi unajua Fadhili anakupenda sana?
Hivi unajua nilimwambia umepigwa kwa ajili yake akasikitika sana?Ni vile alisema hatakupigia simu anataka kukuona ana kwa ana.Unaonaje nikimwambia mkutane?
Sawa kabisa. Tena mwambie anipigie.
Nilijibu haraka sanaNa swntensi hiyo nikaisindikiza na maneno,
Ukiona wa nini wenzako wanasema tutakipata lini... Nilisema kwa hasira.
Mama Karisa akacheka, Ha ha ha... Ayeya... Asusa... Kisha akanigongea kunipa Tano.
Alipimaliza kucheka akapiga simu na kumwambia aliyempigia,
Kazi ni kwako,Ushindwe mwenyewe...Nikajua alikuwa akimpigia Fadhili.
Baada ya dakika mbili nilipigiwa simu. Mama Karisa akaitazama simu yangu akaniambia,Fadhili huyoo.
Pokea. Nilipokea,
Haloo Mwanamke unayeninyima usingizi...... Alisema Fadhili.
Maneno hayo yalipenya moyoni vaap... Nikasikia faraja na burudiko. Nikaachia tabasamu.
Sema.. Nikajibu huku Natabasamu.
Nakupenda sana wewe mwanamke. Nashukuru Mungu kukutana na wewe. Tangu nikuone ile siku mpaka leo Nateseka. Lakini nafurahia mateso haya kwa sababu ni ya Mapenzi. Tangu nimezaliwa nimegundua sijawahi kuteswa na mapenzi kiasi hiki. I love you mamiii. Nakuoenda. Wewe ni mtu mzima najua unaelewa nini maana ya Kupenda.

Dah... Maneno hayo yananifanya nakuwa kama mjinga kabisa.
Natabasamu kisha namwambia,
Na weweee....
Ndio mamii namaanisha. Na hivi leo nimesikia sauti yako ndio kabisaaaa... Sijui kama Nitalala. Ila napenda ninavyoteseka juu yako. Fadhili aliendelea.Kisha akaniambia tena kabla hajakata simu,
NAOMBA NIKUONE KAMA HUTAJALI. KISHA UNIJIBU KAMA UNANIPENDA AMA LA.
Alimaliza kuongea. Nikamtazama Mama Karisa ambaye naye alikuwa akinitazama.
Akaniambia enhee... Sema. Mwanaume ndo huyo. Namjua Fadhili. Anajua kupenda sana. Na ana care ile mbaya. Mwanaume hasaaa.
Kasemaje?Mama Karisa aliniuliza.
Mh... Niliguna... Mama Karisa akaniambia,Waacha weee....
Nikamwambia, Hivi Hana mke?
Mama Karisa akacheka sana.
Una nini wewe?Kwani Mke Ndo nini?Wewe Huna Mume kwani?
Unataka ndoa unataka mapenzi?Hata angakuwa nao kumi,What you need is Love. Full stop. Hembu kua bwana na wewe.
Mama karisa aliniambia.
Bado nilitamani kujua juu ya Fadhili.
Mama Karisa acha utani Bana. Fadhili hana Mke?
Mama Karisa alinitazama sasa hivi akiwa serious kidogo.
Mke anaye na watoto 2. Lakini haihusiani na Mapenzi yako na yeye. Unahitaji faraja ya moyo. Unahitaji Mapenzi. Full stop. Hata angekuwa na wake sita ni wakwake. Wewe pata mapenzi urudi ukaleee wanao. Ama unataka Ndoa?Mama Karisa akacheka tena.
Mh. Nikasema na kweli.
Wakati huo huo nikachukua simu yangu na kumpigia Fadhili.
Alipokea haraka sana na kuniambia Enhe,Sema kimwana.
Nikajiskia rahaa sana. Sina usemi. Nikajibu.
Akaniambia Nakupenda.
Nikamwambia Asante.Kisha akaniambia enhe... Poza moyo wangu basi. Niambie jambo nijiskie na mimi ni mwanaume.
Alisema kisha nikamwambia Nakupenda pia.
Asante sana. Natoka mazoezi sasa hivi. Naomba nikuambie mahali pa kukutana. Natamani kukuona mpenzi.
Fadhili aliniambia hivyo.
Uwii. Mama Karisa alinitazama akaniambia,Haya mwali. Kazi ni kwako. Mimi nikuache. Take care. Ushindwe mwenyeww. Bwana ndo huyo. Janaume la miraba sita, Ana kazi nzuri sana. Ana pesa na Anajua mapenzi. Ukikosa raha tena usinililie. Alafu tabia ya kila ukikutana na mimi unalia lia ooo ndoa ndoa,koma. Ukikutana na mimi nataka kusikia mambo ya malavi davi. Sawa bibi?Upo?Baiii... Take care.
Mama Karisa aliondoka akaniacha nimeduwaa.
Baada ya li saa Fadhili akanipigia simu na kunielekeza pa kumkuta. Akaniambia anamtuma na.dereva kabisa nitembee mpaka mahali kona kisha dereva wake atanichukua hapo.
Nilijivalisha nguo haraka huyooo. Nikaondoka.
Nilifika aliposema atatuma Dereva na kweli nikamkuta.Kisha Dereva huyo akaendesha gari mpaka kwenye Ile.ile Bar. Nikafika. Akanikumbatia kama mtu ambaye tulishaonana. Nilikuwa na.hofu sana. Akaniambia unaonekana unaogopa sana.
Tuhame hapa tuhamie ndani?Ndio. Nilijibu.
Wakati huo dakika chache simu yangu ikaita.Ni Mr alikuwa anapiga. Moyo ukapasuka paaa. Fadhili akanitazama na kuniambia maskini,Utakufa,Huyu mwanaume anakufanyaga nini?Hembu usipokee hiyo simu. Wacha iite mpaka izime. Usipokeee. Sitaki kabisa kuona unakosa raha.
Sikia Mamii, Ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona.
Hivi Diaa unajua na mimi nina mke ila kwako moyo wangu umefika?Si unaona simu yangu nimeweka kabisa silencer?Nataka kufaidi penzi lako. Sasa sikia, kama unataka tufaidiane hawa wenzetu wakae pembeni. Sawa?Ili sisi tufurahie mapenzi . Sawa eee. Usijali nitakufunindisha kila kitu usiogope.
Bado akili yangu ilikuwa kwenye Simu ya Mr.
Fadhili aliniambia Nakupenda Dia. Naona huyo Hitla wako anakukosesha Raha. Unaonaje nimuite Dereva akurudishe kwanza kisha tutaonana ukiwa umetulia?
Moyoni nikasema mh... Mara nimkose Fadhili itakuwaje?Nikajiambia liwalo na liwe. Wacha ni kubali tuu. Nikachukua simu nikaandika niko Salon.
Basi nikatuma msg.Fadhili akaniangalia akasema Asante kunipenda. Unadanganya kwa ajili yangu sitakuangusha. Nitakupa mapenzi kuonyesha najali na unaniheshimu. Jiandae kupendwa.
Dah. Ni kweli ni mama wa miaka 29 wakati huo .Sijawahi kukutana na aina hii ya mwanaume tangu. Nikishangaa sana. Akili yangu ikaniambia kweli penye wajenzi hakuna miti. Mke wake yuko wapi mume anachepuka?
Fadhili aliagiza chakula na Akanilisha. Kwa kunihurumia sana na majeraha yangu maana bado nilikuwa na makovu mwilini. Alisikitika sana kuona nilivyovilia damu.
Tulikula tukamaliza. Kisha akaniambia sitaki upigwe tena. Nenda mamii. Nakupenda. Akinikumbatia kwenye likifua lake la haja. Kama dakika tano hivi. Huku ananiambia ananipenda sana. Mimi ni mrembo sana na atahakikisha Thamani yangu ya kike inarejea.
Mamii,Nataka ujue wewe ni wa Thamani. Nitakupenda mpaka ujue thamani ya Kike maishani. Nataka nikupende ukiwa unatembea kila anayekuona ajue unapendeka. Nataka nikupende mpaka mumeo ajue Unapendwa ila asijue ni nani anakupenda.
Take care...Nakupenda. Nilijikuta nalia sana. Akanibembeleza na kuniambia Nyamaza. Am here for you Diaaa.Tukaagana. Nikawa nasimama kuondoka. Nikapiga hatua kama Tano hivi. Akaniita, Mamii,Mamii Nikageuka Akaniambia nisubiri. Akatembea haraka kunifikia. Akanikumbatia. Kulikuwa na walevi wengine hapo wanakunywa pombe zao wakatuona wakapiga kelele,Weweeee.. weee..Nikaogopa sana. Akaniambia usijali. Washkaji hawa. Kisha akaniambia naomba nikupe pesa. Naomba tuuu. Nikamwambia nooo...Akaniambia naomba nikupe. Akaingiza mkono kwa suruali. Akatoa walet yake. Akahesabu noti za elfu kumi kumi kama noti kumi na tatu. Akanipa. Akaniambia bai.
Nikamwambia Asante. Huyooo nikaenda Home.
Nukafika home saa Tisa mchana. Nikajisemea moyoni waooo. This is love.
Jamani mwanaume yule. uwiii.
Nikachukua Simu yangu nikampigia Kumuambia Nimefika home Salama.
Akaniambia Where is Hitla?Nikacheka. Nikamwambia hajafika bado. Akaniambia poa.Take good care of ur self.
Nikatamani kumsimulia mtu juu ya mapenzi niluyopata.Mapenzi ya maneno. Nikaona isiwe taabu. Nikampigia Mama Karisa. Akapokea. Nikasimulia kuanzia a to z. Akaniambia waoo. Bora shoga angu na.wewe upate raha. Maana dah. Ungekufa na kihoro. Huyo ndo Fadhili mamiii. Mwanaume yule hajawahi kupata mapenzi. Na anajua kupenda. Sasa zubaa uliwe. Na wewe Changamka. Mpende mpendane. All the best mamii. Kama una raha na mimi nina Raha. Ukifurahi ndo raha yangu.

ITAENDELEA SEHEMU YA TATU (post #6)
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
FB_IMG_1559779836804.jpg


Ndo siku ya kwanza naanza kujifunza uchepukaji. Swali langu ni je Mke wa Fadhili yuko wapi?Wanaishije?
Najihoji maswali mengi. Tangu niingie Ndoani kamwe sijawahi kuchepuka. Ama kwa hakika Ndoa huharibu tabia za wanawake. Hivi mume wangu angenipenda haya yangetoka wapi?Potelea mbali.
Atajijua. Na huu ni mwanzo tuu.Nilijikuta namkumbuka tena Fadhili. Na sasa nikampigia Simu kuongea naye. Akapokea na kucheka sana. Akaniuliza Jamaa yako hayuko hapo Karibu?Nikamjibu hayupo. Akaniambia sema mamii. Nikamwambia sina usemi nimekumiss tuu. Akaniambia Nakupenda. Kama vipi Kesho tuonane nikitoka mazoezi. Tuonane mapema.
Mh. Nikamwambia sawa kabisa.
Basi tukaagana. Baada ya muda Mr akaja. Mr nilimwambia nilienda salon. Aliporudi akanitazama na kuniambia mbona hujaenda salon na ulisema uko.salon?Nikamwambia nikiahirisha baada ya simu yako.
Akanitazama akaguna.
"Huo umalaya unaojifunzia uzeeni utakugharimu. Usisahau Condom usije Ukafa"
Mr akaniambia.
Dah. Nikasema ni nini hii lakini?Maneno gani haya?
Sikia Mama Davis. Unaonekana kabisa kuna tabia umeanza. Sitaki mada kesi. Hao mabwana zako kuwa nao makini. Nisije kata shingo yako ama ya mwanaume hapa mjini. Ohoooo... Haya.
Baba Davis aliongea kwa hasira lakini kwa vituo.
Sikujali japo nilikuwa naogopa nikihofia kipigo.
Hembu hiyo simu yako,Baba Davis alisema. Nilichukua simu na kumpatia. Wakati huo nilishafuta calls zoote za Fadhili. Akaangalia kisha akanirudishia simu.
Sikia,Mji wa Arusha mdogo sana. Kwa vile umeamua kufanya ufuska,nikuombe kuwq makini. Sitatamani kukuaibisha.
Alirudia tena.
Nilikuwa tu kimya. Nikajiuliza kukikoni?Amejua ama?Amehisi ama?
Mwisho nikasema potelea mbali. Aniache.
Nikaandaa chakula akasema hatakula. Na akahama chumbani. Akawa analala chumba cha wageni. Mh. Lakini nikasema sawa. Uamuxi ni wa kwake.

*************************************
Mume wangu ni mbabe sana, na siku zote za maisha yetu, tumekuwa ni watu ambao hautuwezi kukaa pamoja na kujadili jambo. Yani akiamua ameamua, hakupi uhuru wa kuchangia mada wala kkutoa wazo. Ninamfahamu. Hivyo hata hapa namuulizaje juu ya kuhama chumba?
Niliamua kumuacha tu. Nakumbuka siku za nyuma sana, aliwahi kuwa na mahusiano na msichana mmoja ambaye alikuwa ni mwanachuo, alikuwa anasoma chuo cha uhasibu. Niliumia sana kipindi hicho, nilipojaribu kumuuliza kulikoni baada ya kuona ticketi mbili xa ndege za kusafiria yakweke na ya huyo dada anaitwa Herieth, nilipomuuliza alinigombeza sana na kunitukana sana, na aliniambia sitamuona nyumbani kwa sababu ana mdomo, mpaka siku nikiacha mdomo ndipo nimuambie aje nyumbani.
Kweli alihama nyumbani kama miezxi miwili hivi, nikajua kabisa anaishina huyo msichana, Mpaka badae Yule msichana alipomaliza chuo na kuondoka ndipo mahusiano yao yakafa, hata hivyo nilipoona kahama nilianza kujibaraguza na kumuambia sitamsemesha tena arudi tu tena anisamehe.
Hivyo nimekuwa nikiteseka sana ndoani hata kumuonya sikuwa nathubutu. Maisha yakawa hivyo.
Sasa leo naanzaje kujadili mada ya kuhama chumba? Yamkini ana mwanamke wake ndio maana kahama.
Lakini na mimi nikasema potelea mbali, maadamu na mimi niko na Fadhili basi wacha ngoma iwe droo. Akidhani kanisusia mimi nakusanya nguvu na mapenzi ya Fadhili. Na sasa nikaamua kabisa wiki hii ni mapenzi moto moto na Fadhili. Na hivi Mama Karisa kashaniambia Niache uzoba, basin a mimi nikasema liwalo na liwe.
Asbh nilijiandaa na kwenda kazini. Nilifika kazini na kufanya kazi haraka haraka, ama kweli Penzi kitovu cha uzembe. Nikasema kwa nini nisiombe ruhusa naenda hata hospital ili nikaonane na Fadhili? Ni mida ya saa nne asbh. Nilianza kuongea na wenzangu kwamba najisikia vibaya, na hivi karibu staff nzxima walikwua wanajua nimepigwa walinihurumia na kuniambia nenda tu mamii. Nilichukua pochi yangu, nikaondoka na kuelekea kwenye mgahawa ambapo nilikaa hapo na kuanza kupiga simu.
Nilipiga simu ya Fadhili na haikupokelewa, niliipiga sana kama dakika kumi hivi bila majibu.
Nikaamua kuagiza supu nikawa nakunywa. Badae Nilisikia simu inaita, niliitoa kwenye pochi na kuitazama, ni Fadhili anapiga, nilitabasamu kwanza kabla ya kuipokea, kisha nikapokea.
Haloo .. … haloo diaaa upande wa pili uliita.
Ni Fadhili aliyekuwa anaonga.
Sijambo, wewe mzima? Nilimuuliza.
Ndio mimi mzima kabisa, alinijibu. Kisha akaniambia , samahani sikuona simu yako, nilikuwa busy na shughuli za hapa na pale.
Pole sana, nilmjibu. Asante akaitika.
Niambie mamsapu… aliniambia.
Nilimwambia nimekumiss tu, niko nimekaa mahali nikaona nikupigie.
… Ha ha ha… Alicheka na kuniambia wewe mwanamke unataka kuniua eeee.. niko kazini, kunashughuli nazifanya hapa, kisha nitatoka saa nane, alafu baada ya hapo nitapitia mazoezini nitatoka saa 12. Ulikuwa unasemaje mamii?
Mh… niliona ratiba yake ilivyokuwa imejaa. Sijui hata anafanya kazi wapi. Kazi ya kutoka saa nane ni kazi gani hiyo? Nilijihoji kisha nikakosa jibu nikanyamaza.
Nilikuwa nimekumiss tu, nimepata nafasi kazini nikasema nikupigie nikidhani uko na muda ili tuonane.
Dah… alisema, kisha akawa kama anataka kusema kitu kwa sekunde kadhaa.. ammmmm… ammm… ngoja kidogo subiri hapo hapo nikujibu.
Fadhili alikuwa anaongea na mtu mwingine na nikawa nasikia…
Imrani hembu niambie ile oda ya Mr Makambi imeshashughulikiwa?
Aliongea hivyo, kisha nikasikia tena akisema, Od azote za jana na juzi zimekamilika, Invoice ziko tayari.
Alipokuwa anaongea hivyo alinirudia na kuniambia, Mamii.. naomba tukutane saa saba, nitamtuma dereva aje akuchukue, unielekeze utakapokuwa. Nilimwambia nitakuwa salon nikitengeneza kucha.
Alimaliza kisha na mimi nikapumua,kwa sababu ukweli nilihitaji faraja na sikutaka kujali inatoka wapi kikubwa ni faraja. Na leo nilipanga nitakuwa na maongezi na Fadhili ya kina, maongezi ambayo yatanipa kumjua yeye vyema, historia yake na familia yake, lakini pia swala la afya yake.
Nilipomaliza kunywa mtori, sikuona sababu ya kurudi kazini kwa sababu nilishaaga, na niliamua kuelekea salon.
Nilifika salon na kuamua kutengeneza kucha za mikononi na miguuni.
Saa saba kamili on dot, Fadhili alinipigia simu na kuniambia, Mamii, Dogo (akimaanisha Dereva) Atakuja kukuchukua hapo salon, Sawa niliitika.
Na baada ya dakika chache sana Dogo alifika, na kunichukua.
Alinisalimia, Dogo ni dereva wake, ni kijana mwenye lafudhi ya Kisambaa, bila shaka ni msambaa huyu. Kijana mweusi na mfupi. Alinisalimia shikamoo Sister, niliitika kisha nikapanda kwenye gari na kuelekea alipoambiwa annipeleke. Nilijua ni kule kule kwa siku zote. Lakini sasa sio huko , niliona kabisa Dogo akiendesha kuelekea sehemu ingine kabisa. Ni nje kidogo ya mji, nilishangaaa.. Tuliendesha kwa dakika kama 30 hivi, ni zaidi ya km 20 kama sio 30.
Aliendelea kuendesha, na sehemu hiyo ilikuwa ni sehemu ambayo hakuna makazi mengi ya watu, nilikuwa nikiona nyumba mbali mbali sana. Na baada ya dakika chache sana tukawa tumefikaa.
Ni eneo zuri na llina jengo jipya sana. Dogo aliniambia hapa ni kwenye mradi wa Bro. Ni hotel anajenga. Hii ni hotel.
Ni sehemu nzuri sana, na Jengo lake kubwa sana, lakini bado halijamalizika. Tulikuwa walinzi na wafanyakazi wengine wakiwa wanajenga na kufanya usafi na kuotesha miti na maua.
Nilipelekwa moja kwa moja kwenye moja ya nyumba ndogo iliyopo ndani ya eneo hilo hilo. Nyumba hii ilikuwa imemalizka vizuri kabisa. Ni nyumba ambayo inazo mpaka na feniture.
Dogo aliniambia nakuacha hapa, Bro anakuja sasa hivi. Nilikuwa naogopa,, hapana Dogo, usiniache peke yangu, ngoja mpaka Fadhili aje. Niliogopa kwa sababu ni sehemu ambayo ni ngeni kwangu, lakini pia ni mbali sana. Niliogopa. Usiogope sister.. Wakati tunaendelea kujadili mara geti kubwa na honi zilikuwa zikipigwa sana, na Dogo akaniambia Broo huyo. Dogo alitoka kwenda kumpokea Bro, na kuniacha ndani.
Fadhili alifika na akawa anazunguka hku na huko kama nusu saa hivi huku akitoa maelekezo na alikuwa kama akilipa watu pesa, na baada ya hapo, alikuja.
Pole mamsapu.. alinikumbatia na kunibusu, Na kuniambia pole nimechelewa,, umeogopa eeee….
Aliuliza… ndio, nimbali sana huku,,, Alitabasamu.. akasema yes. Panafaa sana kupumzika huko , nimejenga hapa kwa ajili ya mapumziko, Ni lodge hii. Imenila sana pesa, na kunisumbua sana akili. Iishe tu.
Alisema Fadhili. Alionekana kweli kama ambaye amechoshwa na jambo.
Hapa kitakachonisumbua ni Umeme, ninapata taabu sana na Umeme, yani nikipata umeme hapa nitafungua hii lodge rasmi mwaka kesho. Ninataka kuifungua mwakani. Lakini umeme utanichelewesha.. Naomba nikuzungushe uone Lodge ya mpenzi wako… Alisema h ivyo kisha akanikumbatia na kunibusu na kuzungusha mkono wake kiunoni na kuchukua wangu na kuuxungusha kiunoni mwake na kuniambia usiogope… mimi ndiye mpenzi wako, Mwanaume wako niliiyeumbwa kwa ajili yako. Usiogope.
Alinishhika kwa ujasiri sana, nikajiuliza jamani huyu kaka ana mapenzi sana, Sijawahi kupendwa hivyo muda mrefu sana.
Mwanaume ambaye ni handsome, ambaye anautunza mwili wake kwa mazoezi, anaonekana mwenye pesa, anaonekana mwenye mapenzi, dah.. kuna wanawake wana bahati duniani sana. Nilitamani kumjua mke wake sa.a
Tulitoka nje na kuanza kutembea, na kuanza kunielekeza na kuniambia kila eneo ni sehemu ya nini na nini. Ni jingo la gorofa 4. Kila floor ina room 8. Room nzuri sana ambazo zimeshamalizika bado finishing kidogo sana.
Baada ya hapo akaniambia hapa ni ukumbi mdogo wa mikutano, utachukua watu 100 mpaka 15 tu.
Na lodge yetu (akasema lodge yetu as if nahusika sanaa, wanaume jamani, Na mimi likichwa linafura kabisa.) Lodge yetu itachukua wateja wa kulala 60 tu kama itakakuwa imejaa, Nataka ya wateja wachache ili wapate huduma amaizing.
Ahaaa… utaitaje? Nilimuuliza,,, Alitabasamu, akaniambia niambie mpenzi niipe jina gani? Nilicheka na kumwambia sina jina mbona, akaniangalia akaniambia nitaiita BEMBEA LODGE . Ama ulitaka niiiteje mamii? Hapana, jina zuri sana.
Aliniambia na hapa ndipo nitajenga swimming pool , na wataanza wiki ijayo kuijenga.
Kisha baada ya hapo akanipeleka kwenye jingo kubwa ambalo ni kama stoor, aliita, Amiri… Amiri alikuja akiwa anakimbia na akafika na funguo, Alifungua mlango na tukaingia ndani. Dah… nilishangaa kuona feniture nzuri sana na nyingi mnoooo, na mabox ya tv, akaniambia mamii, si unaona, hivi vyoote ni vifaa na feniture za lodge yetu, nilishanunua kila kitu, ila kufunga tu sasa ndiyo bado kwa sababu umeme ndio tatizo.
Tulimaliza na kuzunguka kila eneo na tukarudi kwenye ile nyumba nzuri sana ambao ina room 3 za kulala, sebule, dining hall, jikoni na stoor.
Nilikaa Sebuleni ambapo kulikuwa na feniture zoote. Aliniambia mamii nikupikie? Nilicheka, alifungua friji na kutoa sausage pakiti nxzima, na kuzichemsha kwenye jiko la gesi.
Kisha akatoa box la juice kwenye friji, akaleta na glass mbili na kuweka mezani. Na kutoa chupa ya maji ya Kilimanjaro akaweka mezani pia. Tukaanza kula alinikaribisha.
Dah, nilishangaa sana ,
Fadhili, samahani, ninaweza kukuuliza swali? Ndio mamii niulize tu, Aliniambia akionyesha kuwa na shauku ya kutaka kujua namuulixa nini.

ITAENDELEA SEHEMU YA NNE (post #7)
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
FB_IMG_1559779857905.jpg


Nilitamani sana kumjua vyema Fadhili. Ni mwanaume kijana,kama anazidi miaka 35 ni bahati. Lakini anawezaje kumiliki lodge kubwa kiasi hiki?Lakini mke wake yupo wapi?mbona hii nyumba nzuri hivi haiishi mtu?Tena nilipokuwa nakagua haraka haraka sioni kama ni nyumba ambayo mwanamke anaweza kuwepo hapo. Si pachafu lakini hapana usafi wa kuonyesha mwanamke yupo hapo. Nilimtazama Fadhili usoni nikamwambia, Navutiwa na wewe sana.
Aliniambia Karibu. Kisha akanishika mkono na Kunitembez taratibu hadi kqenye balcon kwa nnje. Hapo kuna viti viwili tukakaa. Na meza nzuri tuu. Akaniambia You know what mamii,Hii ni maneja house. Hapa atakaa meneja wa lodge.yetu.
Ahaaa,Nikajibu.
Aliniambia nina hamu sana na unachotaka kuniuliza, enhe.. endelea mama yangu
Aliniambia kisha nikakohoa kidogo kama ninayetengeneza sauti. Kisha nikamwambia,
Kama nitakuwa navuka mipaka nisamehe,Ila natamani sana kujua juu ya Familia yako.
Akinitazama na kuniambia unataka kujua nini hasa mama yangu?Aliongea kwa upole sana.kisha akaniambia,Unafikiri nikikuambia huajiskia vibaya?
Hapana,Sitajiskia vibaya,Niambie tuu.
Okay. Alichukua simu yake na baada ya hapo akaifungua na kunipatia. Akaniambia angalia hizi picha hapa. Nakuja.
Alisimama na kuelekea ndani.
Kisha akarudi na glasi mkono wa kushoto na mkono wa kulia kashikilia chupa ya pombe kali.NiJackdaniel hiyo. Nikumiminie kidogo mama?
Ops.. sorry unatumia dawa bado eee...
Ngoja nije just a moment,Wacha nikuletee vitu laini kama wewe.
Aliondoka na kurudi tena na chupa ya soda ya fanta na glass. Kisha akanimimini na kunipatia Na sasa hivi hakukaa kwenye kiti bali alikaa chini kabisa na kukunja miguu yake kama anayekula pilau la idi.
Kisha akanitazama. Akaniambia umeona hizo picha eee.
Huyo ni mke wangu na hao ni watoto wetu. Nina watoto 4. Na Huyo ndo mke wangu.
Enhe,Kingine mama?
Aliniuliza.
Sikuwa na haraka. Niliona picha nzuri sana za mwabamke mrembo sana. Yani mwanamke mzuri. Mimi ni mwnamke na.tumezoea mwanaume akichepuka ana mke hohe hahe. Lakini sio kwa mwanamke huyo niliyemuona kwa simu. Ni mrembo hasa. Na watoto wazuri wenye furaha.
Kidogo nikama napoteza pozi. Maana mke mke hasa. Sasa kakosa nini huyu mwanaumw jamani?Akili kama zinarudi fulani hivi.
Mamii mbona kama hujaniuliz kitu. Kingine ni nini mama?
Hapana. Asante. Una mke mzuri sana.
Nilimwambia.
Asante. Ila hakufikii hata kodogo. Wewe mzuri sana. Napenda umbo lako,rangi yako,sura yako na sasa nina raha kwa sababu nategemea na Penzi lako nilipende.Fadhili aliniambia. Na kisha akasimama na kuniambia mamii muda muda. Nikitazama simu yangu ni saa kumi na.nusu jioni.
Akaniambia dah.. Yani wewe mwanamke ninavyopenda mazoezi lakini naacha kwa ajili yako. Dah. Nakupenda sana. Aliniambia enhe... Niambie lini utakuwa na nafasi ya siku nzima. Nataka kukaa na.wewe siku nxima. Unipikie,Unilishe,uniogeshe Niambie lini mamiii.
Nilitabasamu nikamwambia hata kesho.
Akacheka. Akaniambia serious?
Yes. I mean it. Nilimkahkikishia ninachokisema nakimaanisha.
Basi sawa kabisa.
Basi naomba nikuwahishe mama yangu. Alafu kesho saa nne tukutane hapa kwa raha zetu. Akitabasamu na kuninyanyua. Kisha tukatoka kuelekea kwenye gari.
Akaniambia niendeshe mpaka pale njia panda kisha Dogo aje kukupick pale.
Sijui kuendesha gari. Nilimjibu.
What?Yes. Sijui kuendesha gari.
Nilirudia tena.
Aiseee.. Mwanamke mzuri hivi hujui kuendesha gari?why?
Nilitabasamu na kusema wacha nichomekeeee. Nikamwambia Mwalimu natoa wapi pesa ya gari?
Akanitazama akatabasamu. Kisha akasema hembu ngoja .Akashika simu yake akabonyeza bonyeza na kuniambia Nikikupa gari utasemaje kwa Hitla wako?
Nilinyamaza dakika moja tu na kumwambia nitamwambia nimekopa. Uwii. Nitafurahi sana sana.Akaniambia basi anza shule,Ila noooo. ..Nitakufundisha mwenyewe. Nitakufundisha peke yangu. Nakupenda sana wewe mwanamke. Nilikuwa nakung'atia tu meno.
Tulifika njia panda. Dogo alinichukua na kunipeleka mpaka anaponishusha siku zoote.Nilishuka na kutembea na mguu hadi nyumbani.
Nilifika nyumbani Mr alikuwa hajafika bado.
Niliandaa chakula na baadae nikala na watoto na kwenda kitandani.
Nilikuwa nogopa sana kupiga simu kwa Fadhili kwani nikiogopa mke wake lakini pia niliogopa Baba Davis asije akafumania msg ataniua.
Hivyo sikuwa na tabia ya kuandika msg. Lakini nikaona wacha nimsimulie mama Karisa .Saa nne nikaanza kuongea na mama Karisa nikampa umbea woote. Akacheka sana na kuniambia bado. Utafurahi sana. Namjua Fadhili ni Alwatani wa mapenzi. Pale umefika mamii. shida ya ndoa yako imeisha. Na ndio sasa usiache kumjali mumeo. Mimi nimeishi na Mpenzi wangu mwaka wa saba huu na mr hajui kabisa. kazi ni kwako. Sawa mamiii. Sawa mrs Fadhili... Kisha akaachia cheko, ha ha ha.... Hongera nyonda.
Alisema hivyo na tukaagana.
Dah. Kupendwa raha sana.
Saa nane mr hajafika. Saa tisa, Mara asbh hii hapa.
Hajafika.
Nikachukia sana. Nikajiandaa na kuelekea kazini. Lakini lengo ni ifike saa nne tukakutane na Fadhili.
Tukikubaliana saa nne. Nilimpigia simu nikaanza kulia nikimuelezea juu ya Mr kutorudi kwake nyumbani.
Sikia mamii,Usiwe unaniambia mambo ya huyo bedui kabisa. Ninaweza kumfanya kitu mbaya. Please sitaki kusikia anakutesa kabisa. Pole. Ndio maana nipo mimi kuhakisha usalama wako. Na ni kwa vile naogopa tuu kukuambia Uachane naye maana sijajua unamaagano gani na yeye,ila sio mwanaume huyo. Sio kabisa.
Aliniambia naomba nije kukuchukua.
Sawa niliitikia. Hapo nilikuwa nalia sana. Moyo umejaa uchungu na hasira za hali ya juu. Saa nne aliniambia nimkute mahali. Nilifika na atukaondoka. Akinihurumia sana na akaniambia,
Nakuonya mpenzi wangu. Sitaki kusikia juu ya huyo mwanaume akikufanyia unyanyasaji. Sawa mama. Nataka ukikutana na mimi tuongee maisha ya Raha tuuuu. Ufurahie maisha sawa mama. Usilie kabisa. Uko na Real man. Sawa mpenzi. Nyamaza. Nilijifuta machozi. Nikasema jamani mwanaume ndio huyu sasa. Aliniambia nataka tuongie supermarket tununue chakula. Enhe mamsapu,Nitume sasa. Niambie chakula gani unataka nikanunue. Samaki,kuku na kingine?
Nilitabasamu nikamwambia sawa kabisa na beef filet usisahau.
Aliingia supermarket akatoka na mazaga zaga kibao.
Haoo tukaanza safari ya kuelekea BEMBEA LODGE. Bado ninatafakari,Huyo mke ana kasoro gani jamani?Huyo mke mbona haonekani kuwa karibu na huyu mwanaume?
Any way. Atajijua. Hata mimi nimekwapuliwa wangu. Atajijua. Wacha nivute raha zangu.Haoo tuliendesha mpaka tukafika. Tukaingia ndani ya mjengo.
Alitoa mfuko ambao ulikuwa na nguo. Akaniambia mami najua unahofu. Huo mfuko una khanga,na nguo zingine nimekununulia zawadi. Nilitabasamu. Mh.. Nikaguna. Nilichukua na kuangalia. Kulikuwa na nguo blauzi mbili nzuri na Khanga mpya pair 2.
Na nguo za ndani.
Huyu mwanaume ni wa aina gani?Huyu baba jamani katoka wapi?Nilitafakari haraka. Mbona upendo uliokithiri huuu jamani?Dah.
Aliniambia you can change mamii. Chumba hicho hapo. Jiskie huru kabisa.
Na yeye alingia ndani na kuvua nguo alizokuwa kavalia na shati la kadeti ambalo lilikuwa ni uniform ya kazini. Na kuvaa singland na kaptula. Sasa nikaqeza kuona mwili wake barabara ukivyogawanyika.
Akaniambia Go and change,jiskie huru mama yangu. Nami nikaingia ndani na kubadilisha nguo. Khanga moja mamii.. kazi kweli kweli.. Akijisemea. Nilitabasamu na kutoka nami nimebadilisha nguo. E waaaa... sasa Unaonekana mwanamke wa Fadhili sasa. look at you mamii.
Mwanamke hasa. Hivi wanaume wengine wakoje?Mwanamke kama wewe ni adimu sana kuparikana duniani humu dah. Aisee umeumbika hasaa mama.
Ingia jikoni sasa mhudumie mume wako. Kisha nina wageni wangu watakuja kula lunch sawa mamii.
Moyo ukafanya paaaa... Wageni tena?
Ndio. Usiigope. Uko kwenye mikono salama. Usiogope kabisa. Nitakulinda. Nataka penzi letu lidumu milele.
Usiogope kabisa.
Nilijiuliza ni wageni gani? Nikiingia jikoni na kuanza kupika. Nilipika wali na samaki na njegere. Kisha tukatengeneza juice.
Baadaa ya hapo nikaandaa mezani. Akaniambia kaaa hapa mamii upumzike. Sema nikupatie kinywaji gani,Nikamwambia nitakunywa juice.Ok... Yeye akachukua tena pombe yake na kujimiminia na kuanza kunywa.
Muda mwingi alikuwa akiwasiliana na simu za kazini. Akitoa maelekezo kwa wafanyakazi.
Lakini sikuona wala kusikia hata simu moja akiwasilina na mke wake.
Kuna mwanaume natamani sana akuone na mimi. Najua hataamini na aliniapia siwezi kukupata. sasa nataka aje aone kabisa uko na mimi.
Akicheka akagonga na mimi. Kisha akaniambia hao wanakuja,Nilimuuliza ni kina nani na hakusema. Dah. Nilikuwa dirishani nachungulia wakati yeye katoka kwenda kuwapokea. Nilicheka kuona ni Mama Karisa na Mchepuko wake. Nilicheka sana.
Wliingia nikasalimiana nao. Na story zikaanza na tukala.
Japo mama Karisa akionekana hana raha kabisa. Sasa sijui shida ilikuwa wapi. Lakini akionekana sio yule. Nilimuuliza na akaniambia hana neno kabisa.

*************************
Tulikula, Wakunywa wakanywa. Wakulala wakalala. Na baada ya kupumzika Tuliamka na kujiandaa kuondoka . Mungu wangu,Nimezini kwa mara ya kwanza tangu niolewe. Niliwaza sana akilini. Sikuwa na furaha hata kidogo. Moyoni nilisikia majuto. Lakini najikaza tuuu. Fadhili aliniona sina raha. Nina uhakika alijua kabisa nimepata hofu. Lakini pia aliniambia Nisiogope ni mwanzo. Nitazoea tuu. Uwiii. Sikuamini kabisa kama inawezekana mimi siku moja kuzini. Nilipata mawazo sana. Utazoe,Usiogope Mamii. Fadhili alisisitiza.
Nimezini bila kupima afya, Lakini Fadhili he ia health. Ilikuwaje hata nikakubali mimi sijui. Mbwembwe zake ndizo zilinifanya nikajikuta nakubaliana naye tena kwa hiyari kabisa bila kulazimishwa.
Baada ya hapo Tuliondoka. Na sasa nikiondoka na Mama Karisa haoo mpaka nyumbani kwangu. Njiani tuliongea mambo mengi sana ya maisha na ya ndoa. Na aliniashusha nyumbani kisha akaondoka zake akaniacha.
Niliingia ndani ni saa mbili kasoro . Na mr hajarudi. Na hatuwasiliani kabisa na simu.Nilisema na mimi sitampigia. Moyo wangu ukawa unaniuma sana. Hivi kumbe hata ukipata mchepuko bado mume akikosea unaumia ee. Nilijiambia. Nimepata mwanaume,Anayenipenda sana, anayenipa pesa na mapenzi,lakini mbona bado naumia Juu ya mume wangu?Huyu baba Davis jamani mbona harudi nyumbani?'Nilikuwa najiuliza alipo. Niliumia sana nikajikaza tuu.
Asbh niliamka na kujiandaa kwenda kazini. Siku mbili sijaenda kazini. Nilifika kazini nikafanya kazi zangu lakini akili ikiwa inazunguka. Upande huu unawaza penzi jipya. Upande huu inawaza kutendwa na mume. Niliumia sana nikiwa ofcn.Fadhili sio mwanaume wa msg wala kupiga simu kama hutampigia.
Na makubaliano yetu ilikuwa ni kukutana tu kwenye Mjengo wake,BEMBEA LODGE.
nikajiuliza mbona mke wakw haji,nikajua lazima atakuwa aiza ni mwanamke ambaye ni mzembe ama la mume anaweza kuwa hataki mke ajue vitu vyake. Lakini kwenye picha mwanamke anaonekana ni mjanja na mshapu. Any way... Watajijua.
Nikikumbuka Fadhili aliniahidi gari. Nikasema hivi kweli alimaanisha ama ni feki feki tuu?
Nitamkumbusha.
Nimeshaanza kumzoea,natamani hata nionane naye tena. Ni mwanaume wa kunifaaa. Jioni inafika na Sijaongea na Fadhili wala kuonana naye.
Niliamua kumpigia simu.
Nilipiga mara kwa kwanza ikakatwa, nikapiga tena ikakatwa,Nikapiga tena ikakatwa. Badae akaniambia am home honey.... pleasw dont call.
Nikaelewa. Ila nili mmisi. Nikatamani hata angenisalimia.
Baada ya nusu saa nikaona ya nini niteseke,Nikamuandikia msg kwamba ninampenda na nina mmisi. Hakujibu msg.
Na nikaamua kupiga simu. Nilipiga simu yake na alikata na akazima kabisa.
Niliumia sana kwa nini anizimie simu. Nilitamani pakuche ili niongee naye.
Siku zikasonga,sijaonana naye.Nikimuuliza mama Karisa ananiambia he ia busy. Mbona hajaniambia?
Mama Karisa akaniambia mwanamke naona unataka ndoa wewe, Huyo mume wa mtu mama. Tulizana.
Nilikuwa nammisi hasa.Baada ya siku kama nne hivi Akapiga simu na Kuniambia tukutane Bembea Lodge kama kawaida. Yani ilikuwa ni siku ya jumapili wala sikujali. Na mr alikuwepo lakini sikujali. Nilivyo mmiss Fadhili naachaje kwenda. Mr alikuwepo nikamwambia naenda Salon. Akanijibu dry,Sikujali. Huyooo nikaking'oa hadi mahali Pa kukutania.
Nikafika tukakutana na Fadhili nikapanda gari haooo mpaka maskani. Tukikunywa,tukala,tukalala tukaamka.
Nilikunywa sana pombe kwa sababu nilikuwa na.stress za kutosha. Mpaka saa moja ndio nashtuka ,Nakurupuka na kuanza kujiandaaa. Niliangalia simu ya Mr ina missed call kama 20 hivi. Kapiga mpka kashaa. Anajua salon ambayo huwa naenda kila siku. Bila shaka alienda hapo. Maana Dada wa Salon aliniandikia msg na Kusema Mr wako kaja hapa tumjibuje maana atarudi. Akiandika kama msg 10 lakini sikuona. Maana nilikuwa chumbani na Fadhili.
Niliogopa.sana.
Fadhili alikuwa kalewa sana. Alikunywa sana hii siku. Nikamuomba anipeleke akaniambia nimuite Dogo. Dogo akaniambia yuko mbali sana. Hatafika kwa wakati. Nilijiskia kulia. Fadhili alikuwa kweli kachoka sanaa. Nilichukua simu nikampigia mtu wa taksii. Nikamuelekeza na baada ya dakika kama 50 hivi akafika.
Nilichukia sana lakini sikuwa na namna.
Nilipofika home Mr alikuwa ndani. Akanitazama na kuniambia,Mama Davis unanitafutia Mada. Umetoka wapi?Kwa vile nilikuwa na woga nikasingizia vikoba. Anajua napenda vikoba.
Aliniambia bahati yako. Leo nimelala vizuri. Ila naomba tabia za kuja kwangu usiku sitaki kabisa.
Sawa mume wangu. Niliitikia.
Kisha nikamkaribisha mezani. Akaniambia kashiba.
Mh, Niliguna tuu. Nikitamani kujua Fadhili anaendeleaje maana nilimuacha akiwa kalewa na kalala. Nilipiga simu kuona kma atapokea. Iliita sana bila mafanikio.Nikaandika msg,Vipi diaa uko poa?
naomba ukipata msg nipigie.

Loading....ITAENDELEA SEHEMU YA TANO (post #13)
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
121,827
2,000
View attachment 1119134

Nilitamani sana kumjua vyema Fadhili. Ni mwanaume kijana,kama anazidi miaka 35 ni bahati. Lakini anawezaje kumiliki lodge kubwa kiasi hiki?Lakini mke wake yupo wapi?mbona hii nyumba nzuri hivi haiishi mtu?Tena nilipokuwa nakagua haraka haraka sioni kama ni nyumba ambayo mwanamke anaweza kuwepo hapo. Si pachafu lakini hapana usafi wa kuonyesha mwanamke yupo hapo. Nilimtazama Fadhili usoni nikamwambia, Navutiwa na wewe sana.
Aliniambia Karibu. Kisha akanishika mkono na Kunitembez taratibu hadi kqenye balcon kwa nnje. Hapo kuna viti viwili tukakaa. Na meza nzuri tuu. Akaniambia You know what mamii,Hii ni maneja house. Hapa atakaa meneja wa lodge.yetu.
Ahaaa,Nikajibu.
Aliniambia nina hamu sana na unachotaka kuniuliza, enhe.. endelea mama yangu
Aliniambia kisha nikakohoa kidogo kama ninayetengeneza sauti. Kisha nikamwambia,
Kama nitakuwa navuka mipaka nisamehe,Ila natamani sana kujua juu ya Familia yako.
Akinitazama na kuniambia unataka kujua nini hasa mama yangu?Aliongea kwa upole sana.kisha akaniambia,Unafikiri nikikuambia huajiskia vibaya?
Hapana,Sitajiskia vibaya,Niambie tuu.
Okay. Alichukua simu yake na baada ya hapo akaifungua na kunipatia. Akaniambia angalia hizi picha hapa. Nakuja.
Alisimama na kuelekea ndani.
Kisha akarudi na glasi mkono wa kushoto na mkono wa kulia kashikilia chupa ya pombe kali.NiJackdaniel hiyo. Nikumiminie kidogo mama?
Ops.. sorry unatumia dawa bado eee...
Ngoja nije just a moment,Wacha nikuletee vitu laini kama wewe.
Aliondoka na kurudi tena na chupa ya soda ya fanta na glass. Kisha akanimimini na kunipatia Na sasa hivi hakukaa kwenye kiti bali alikaa chini kabisa na kukunja miguu yake kama anayekula pilau la idi.
Kisha akanitazama. Akaniambia umeona hizo picha eee.
Huyo ni mke wangu na hao ni watoto wetu. Nina watoto 4. Na Huyo ndo mke wangu.
Enhe,Kingine mama?
Aliniuliza.
Sikuwa na haraka. Niliona picha nzuri sana za mwabamke mrembo sana. Yani mwanamke mzuri. Mimi ni mwnamke na.tumezoea mwanaume akichepuka ana mke hohe hahe. Lakini sio kwa mwanamke huyo niliyemuona kwa simu. Ni mrembo hasa. Na watoto wazuri wenye furaha.
Kidogo nikama napoteza pozi. Maana mke mke hasa. Sasa kakosa nini huyu mwanaumw jamani?Akili kama zinarudi fulani hivi.
Mamii mbona kama hujaniuliz kitu. Kingine ni nini mama?
Hapana. Asante. Una mke mzuri sana.
Nilimwambia.
Asante. Ila hakufikii hata kodogo. Wewe mzuri sana. Napenda umbo lako,rangi yako,sura yako na sasa nina raha kwa sababu nategemea na Penzi lako nilipende.Fadhili aliniambia. Na kisha akasimama na kuniambia mamii muda muda. Nikitazama simu yangu ni saa kumi na.nusu jioni.
Akaniambia dah.. Yani wewe mwanamke ninavyopenda mazoezi lakini naacha kwa ajili yako. Dah. Nakupenda sana. Aliniambia enhe... Niambie lini utakuwa na nafasi ya siku nzima. Nataka kukaa na.wewe siku nxima. Unipikie,Unilishe,uniogeshe Niambie lini mamiii.
Nilitabasamu nikamwambia hata kesho.
Akacheka. Akaniambia serious?
Yes. I mean it. Nilimkahkikishia ninachokisema nakimaanisha.
Basi sawa kabisa.
Basi naomba nikuwahishe mama yangu. Alafu kesho saa nne tukutane hapa kwa raha zetu. Akitabasamu na kuninyanyua. Kisha tukatoka kuelekea kwenye gari.
Akaniambia niendeshe mpaka pale njia panda kisha Dogo aje kukupick pale.
Sijui kuendesha gari. Nilimjibu.
What?Yes. Sijui kuendesha gari.
Nilirudia tena.
Aiseee.. Mwanamke mzuri hivi hujui kuendesha gari?why?
Nilitabasamu na kusema wacha nichomekeeee. Nikamwambia Mwalimu natoa wapi pesa ya gari?
Akanitazama akatabasamu. Kisha akasema hembu ngoja .Akashika simu yake akabonyeza bonyeza na kuniambia Nikikupa gari utasemaje kwa Hitla wako?
Nilinyamaza dakika moja tu na kumwambia nitamwambia nimekopa. Uwii. Nitafurahi sana sana.Akaniambia basi anza shule,Ila noooo. ..Nitakufundisha mwenyewe. Nitakufundisha peke yangu. Nakupenda sana wewe mwanamke. Nilikuwa nakung'atia tu meno.
Tulifika njia panda. Dogo alinichukua na kunipeleka mpaka anaponishusha siku zoote.Nilishuka na kutembea na mguu hadi nyumbani.
Nilifika nyumbani Mr alikuwa hajafika bado.
Niliandaa chakula na baadae nikala na watoto na kwenda kitandani.
Nilikuwa nogopa sana kupiga simu kwa Fadhili kwani nikiogopa mke wake lakini pia niliogopa Baba Davis asije akafumania msg ataniua.
Hivyo sikuwa na tabia ya kuandika msg. Lakini nikaona wacha nimsimulie mama Karisa .Saa nne nikaanza kuongea na mama Karisa nikampa umbea woote. Akacheka sana na kuniambia bado. Utafurahi sana. Namjua Fadhili ni Alwatani wa mapenzi. Pale umefika mamii. shida ya ndoa yako imeisha. Na ndio sasa usiache kumjali mumeo. Mimi nimeishi na Mpenzi wangu mwaka wa saba huu na mr hajui kabisa. kazi ni kwako. Sawa mamiii. Sawa mrs Fadhili... Kisha akaachia cheko, ha ha ha.... Hongera nyonda.
Alisema hivyo na tukaagana.
Dah. Kupendwa raha sana.
Saa nane mr hajafika. Saa tisa, Mara asbh hii hapa.
Hajafika.
Nikachukia sana. Nikajiandaa na kuelekea kazini. Lakini lengo ni ifike saa nne tukakutane na Fadhili.
Tukikubaliana saa nne. Nilimpigia simu nikaanza kulia nikimuelezea juu ya Mr kutorudi kwake nyumbani.
Sikia mamii,Usiwe unaniambia mambo ya huyo bedui kabisa. Ninaweza kumfanya kitu mbaya. Please sitaki kusikia anakutesa kabisa. Pole. Ndio maana nipo mimi kuhakisha usalama wako. Na ni kwa vile naogopa tuu kukuambia Uachane naye maana sijajua unamaagano gani na yeye,ila sio mwanaume huyo. Sio kabisa.
Aliniambia naomba nije kukuchukua.
Sawa niliitikia. Hapo nilikuwa nalia sana. Moyo umejaa uchungu na hasira za hali ya juu. Saa nne aliniambia nimkute mahali. Nilifika na atukaondoka. Akinihurumia sana na akaniambia,
Nakuonya mpenzi wangu. Sitaki kusikia juu ya huyo mwanaume akikufanyia unyanyasaji. Sawa mama. Nataka ukikutana na mimi tuongee maisha ya Raha tuuuu. Ufurahie maisha sawa mama. Usilie kabisa. Uko na Real man. Sawa mpenzi. Nyamaza. Nilijifuta machozi. Nikasema jamani mwanaume ndio huyu sasa. Aliniambia nataka tuongie supermarket tununue chakula. Enhe mamsapu,Nitume sasa. Niambie chakula gani unataka nikanunue. Samaki,kuku na kingine?
Nilitabasamu nikamwambia sawa kabisa na beef filet usisahau.
Aliingia supermarket akatoka na mazaga zaga kibao.
Haoo tukaanza safari ya kuelekea BEMBEA LODGE. Bado ninatafakari,Huyo mke ana kasoro gani jamani?Huyo mke mbona haonekani kuwa karibu na huyu mwanaume?
Any way. Atajijua. Hata mimi nimekwapuliwa wangu. Atajijua. Wacha nivute raha zangu.Haoo tuliendesha mpaka tukafika. Tukaingia ndani ya mjengo.
Alitoa mfuko ambao ulikuwa na nguo. Akaniambia mami najua unahofu. Huo mfuko una khanga,na nguo zingine nimekununulia zawadi. Nilitabasamu. Mh.. Nikaguna. Nilichukua na kuangalia. Kulikuwa na nguo blauzi mbili nzuri na Khanga mpya pair 2.
Na nguo za ndani.
Huyu mwanaume ni wa aina gani?Huyu baba jamani katoka wapi?Nilitafakari haraka. Mbona upendo uliokithiri huuu jamani?Dah.
Aliniambia you can change mamii. Chumba hicho hapo. Jiskie huru kabisa.
Na yeye alingia ndani na kuvua nguo alizokuwa kavalia na shati la kadeti ambalo lilikuwa ni uniform ya kazini. Na kuvaa singland na kaptula. Sasa nikaqeza kuona mwili wake barabara ukivyogawanyika.
Akaniambia Go and change,jiskie huru mama yangu. Nami nikaingia ndani na kubadilisha nguo. Khanga moja mamii.. kazi kweli kweli.. Akijisemea. Nilitabasamu na kutoka nami nimebadilisha nguo. E waaaa... sasa Unaonekana mwanamke wa Fadhili sasa. look at you mamii.
Mwanamke hasa. Hivi wanaume wengine wakoje?Mwanamke kama wewe ni adimu sana kuparikana duniani humu dah. Aisee umeumbika hasaa mama.
Ingia jikoni sasa mhudumie mume wako. Kisha nina wageni wangu watakuja kula lunch sawa mamii.
Moyo ukafanya paaaa... Wageni tena?
Ndio. Usiigope. Uko kwenye mikono salama. Usiogope kabisa. Nitakulinda. Nataka penzi letu lidumu milele.
Usiogope kabisa.
Nilijiuliza ni wageni gani? Nikiingia jikoni na kuanza kupika. Nilipika wali na samaki na njegere. Kisha tukatengeneza juice.
Baadaa ya hapo nikaandaa mezani. Akaniambia kaaa hapa mamii upumzike. Sema nikupatie kinywaji gani,Nikamwambia nitakunywa juice.Ok... Yeye akachukua tena pombe yake na kujimiminia na kuanza kunywa.
Muda mwingi alikuwa akiwasiliana na simu za kazini. Akitoa maelekezo kwa wafanyakazi.
Lakini sikuona wala kusikia hata simu moja akiwasilina na mke wake.
Kuna mwanaume natamani sana akuone na mimi. Najua hataamini na aliniapia siwezi kukupata. sasa nataka aje aone kabisa uko na mimi.
Akicheka akagonga na mimi. Kisha akaniambia hao wanakuja,Nilimuuliza ni kina nani na hakusema. Dah. Nilikuwa dirishani nachungulia wakati yeye katoka kwenda kuwapokea. Nilicheka kuona ni Mama Karisa na Mchepuko wake. Nilicheka sana.
Wliingia nikasalimiana nao. Na story zikaanza na tukala.
Japo mama Karisa akionekana hana raha kabisa. Sasa sijui shida ilikuwa wapi. Lakini akionekana sio yule. Nilimuuliza na akaniambia hana neno kabisa.

*************************
Tulikula, Wakunywa wakanywa. Wakulala wakalala. Na baada ya kupumzika Tuliamka na kujiandaa kuondoka . Mungu wangu,Nimezini kwa mara ya kwanza tangu niolewe. Niliwaza sana akilini. Sikuwa na furaha hata kidogo. Moyoni nilisikia majuto. Lakini najikaza tuuu. Fadhili aliniona sina raha. Nina uhakika alijua kabisa nimepata hofu. Lakini pia aliniambia Nisiogope ni mwanzo. Nitazoea tuu. Uwiii. Sikuamini kabisa kama inawezekana mimi siku moja kuzini. Nilipata mawazo sana. Utazoe,Usiogope Mamii. Fadhili alisisitiza.
Nimezini bila kupima afya, Lakini Fadhili he ia health. Ilikuwaje hata nikakubali mimi sijui. Mbwembwe zake ndizo zilinifanya nikajikuta nakubaliana naye tena kwa hiyari kabisa bila kulazimishwa.
Baada ya hapo Tuliondoka. Na sasa nikiondoka na Mama Karisa haoo mpaka nyumbani kwangu. Njiani tuliongea mambo mengi sana ya maisha na ya ndoa. Na aliniashusha nyumbani kisha akaondoka zake akaniacha.
Niliingia ndani ni saa mbili kasoro . Na mr hajarudi. Na hatuwasiliani kabisa na simu.Nilisema na mimi sitampigia. Moyo wangu ukawa unaniuma sana. Hivi kumbe hata ukipata mchepuko bado mume akikosea unaumia ee. Nilijiambia. Nimepata mwanaume,Anayenipenda sana, anayenipa pesa na mapenzi,lakini mbona bado naumia Juu ya mume wangu?Huyu baba Davis jamani mbona harudi nyumbani?'Nilikuwa najiuliza alipo. Niliumia sana nikajikaza tuu.
Asbh niliamka na kujiandaa kwenda kazini. Siku mbili sijaenda kazini. Nilifika kazini nikafanya kazi zangu lakini akili ikiwa inazunguka. Upande huu unawaza penzi jipya. Upande huu inawaza kutendwa na mume. Niliumia sana nikiwa ofcn.Fadhili sio mwanaume wa msg wala kupiga simu kama hutampigia.
Na makubaliano yetu ilikuwa ni kukutana tu kwenye Mjengo wake,BEMBEA LODGE.
nikajiuliza mbona mke wakw haji,nikajua lazima atakuwa aiza ni mwanamke ambaye ni mzembe ama la mume anaweza kuwa hataki mke ajue vitu vyake. Lakini kwenye picha mwanamke anaonekana ni mjanja na mshapu. Any way... Watajijua.
Nikikumbuka Fadhili aliniahidi gari. Nikasema hivi kweli alimaanisha ama ni feki feki tuu?
Nitamkumbusha.
Nimeshaanza kumzoea,natamani hata nionane naye tena. Ni mwanaume wa kunifaaa. Jioni inafika na Sijaongea na Fadhili wala kuonana naye.
Niliamua kumpigia simu.
Nilipiga mara kwa kwanza ikakatwa, nikapiga tena ikakatwa,Nikapiga tena ikakatwa. Badae akaniambia am home honey.... pleasw dont call.
Nikaelewa. Ila nili mmisi. Nikatamani hata angenisalimia.
Baada ya nusu saa nikaona ya nini niteseke,Nikamuandikia msg kwamba ninampenda na nina mmisi. Hakujibu msg.
Na nikaamua kupiga simu. Nilipiga simu yake na alikata na akazima kabisa.
Niliumia sana kwa nini anizimie simu. Nilitamani pakuche ili niongee naye.
Siku zikasonga,sijaonana naye.Nikimuuliza mama Karisa ananiambia he ia busy. Mbona hajaniambia?
Mama Karisa akaniambia mwanamke naona unataka ndoa wewe, Huyo mume wa mtu mama. Tulizana.
Nilikuwa nammisi hasa.Baada ya siku kama nne hivi Akapiga simu na Kuniambia tukutane Bembea Lodge kama kawaida. Yani ilikuwa ni siku ya jumapili wala sikujali. Na mr alikuwepo lakini sikujali. Nilivyo mmiss Fadhili naachaje kwenda. Mr alikuwepo nikamwambia naenda Salon. Akanijibu dry,Sikujali. Huyooo nikaking'oa hadi mahali Pa kukutania.
Nikafika tukakutana na Fadhili nikapanda gari haooo mpaka maskani. Tukikunywa,tukala,tukalala tukaamka.
Nilikunywa sana pombe kwa sababu nilikuwa na.stress za kutosha. Mpaka saa moja ndio nashtuka ,Nakurupuka na kuanza kujiandaaa. Niliangalia simu ya Mr ina missed call kama 20 hivi. Kapiga mpka kashaa. Anajua salon ambayo huwa naenda kila siku. Bila shaka alienda hapo. Maana Dada wa Salon aliniandikia msg na Kusema Mr wako kaja hapa tumjibuje maana atarudi. Akiandika kama msg 10 lakini sikuona. Maana nilikuwa chumbani na Fadhili.
Niliogopa.sana.
Fadhili alikuwa kalewa sana. Alikunywa sana hii siku. Nikamuomba anipeleke akaniambia nimuite Dogo. Dogo akaniambia yuko mbali sana. Hatafika kwa wakati. Nilijiskia kulia. Fadhili alikuwa kweli kachoka sanaa. Nilichukua simu nikampigia mtu wa taksii. Nikamuelekeza na baada ya dakika kama 50 hivi akafika.
Nilichukia sana lakini sikuwa na namna.
Nilipofika home Mr alikuwa ndani. Akanitazama na kuniambia,Mama Davis unanitafutia Mada. Umetoka wapi?Kwa vile nilikuwa na woga nikasingizia vikoba. Anajua napenda vikoba.
Aliniambia bahati yako. Leo nimelala vizuri. Ila naomba tabia za kuja kwangu usiku sitaki kabisa.
Sawa mume wangu. Niliitikia.
Kisha nikamkaribisha mezani. Akaniambia kashiba.
Mh, Niliguna tuu. Nikitamani kujua Fadhili anaendeleaje maana nilimuacha akiwa kalewa na kalala. Nilipiga simu kuona kma atapokea. Iliita sana bila mafanikio.Nikaandika msg,Vipi diaa uko poa?
naomba ukipata msg nipigie.

Loading....ITAENDELEA SEHEMU YA TANO
Fadhili huyu

Coco babe endelea bwana
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
FB_IMG_1559779875096.jpgSasa nilitulia ili kuona kama nitapata majibu, na kila simu ilipolia nilikimbilia kuangalia kulikoni kwani jumbe nilizokuwa natamani ziingie ni za Fadhili tu. Hali niliyomuacha nayo ya ulevi ni kali sana, alikunywa sana, kwa raha, nilipata muda mzuri sana wa kukaa naye, Nilifurahi sana japo nilikuwa na stress lakini nilipata muda mzuri sana wa kukaa naye. Na kwa kiasi nilifurahi sana kwani nilikuwa niko na mpenzxi wangu, Na niliamini kabisa kwamba Fadhilii ananipenda kutoka moyoni.
Hivi mtu atoe pesa zake, muda wake , mwili wake awe na wewe je si jambo la kupendeka hili? Tena kaacha kabisa mke na wanawe nyumbani na kakuchukua, ukakae naye, tena kwenye lodge yake ambayo anakuambia hiyo nyumba unayokaa humo ndani hata mke wake hajawahi kupafika na hapajui. Mke ambaye ameishi naye si chini ya miaka 9. Lakini hata hapo BEMBEA LODGE Hajawahi kupaingia.
“Sikia mamii, nakupenda sana, yani wewe mwanamke hata sijui umenifanya nini, hapa kwenye hii nyumba hata yule mke wangu hajawahi kupaingia, lakini wew mpaka kitanda umeshakilalia.. mtoto wa kipare unataka kuniua eeee..”Nakumbuka haya maneno aliongea Fadhili kuniambia kwamba nyumba hiyo ambao aliita menaja house hata mke wake hajawahi kupangia.
Kweli ni upendo wa dhati huu. Fadhili ananipenda sana, na mimi nampenda.
Nilikuwa nimekaa tu chumbani kwenye dressing table huku natafakari haya. Kumbuka mume tumetengana vyumba, nilitabasamu na kujiambia moyoni, nimepata bahati sana kupata mwanaume ambaye ana mapenzi ya dhati na mimi.
Nilipanda kitandani na kulala. Nilikuwa nina pesa asubuhi. Fadhili alinipa elfu 60 akaniambia ni ya nauli, Nilitoa elfu 20 nikampatia dada, nikamuachia na maelezo ya kununua vitu. Kisha nikaondoka kuelekea kazini. Mr alisikia nikiwa natoa maelezo, Mara zote siku za nyuma ilikuwa hata akinifanya nini lazima nitamuomba pesa, sasa nimuombe za nini na mimi ninazo, Atajijua, akitoa atoe asipotoa nitatoa maana kuna mwanaume anayenipenda na kunihudumia.
Nilitoka na kuelekea kazini.
Kazini nina walimu wenzangu ambao ni marafiki zangu, wa kuambiana kila kitu, lakini hili swala la Fadhili ninaogopa kabisa kuliongea, ni mume wamtu huyu, lakini na mimi ni mke wa mtu, naanzia wapi kuliongea? Niliona haifai kuonge, na kwa vile tayari nina mwanamke wa kushare naye hizi stori ambaye ni mama Karisa basi huyo tutakuwa tukishare naye.
Mama Karisa ni mfanya biashara, ana duka la kuuza nguo na viatu na vipodozi. Hajawahi kuajiriwa, ni mwanamke mfanya biashara, na huwa anasafiri kwenda Uganda kuchukua mizigo yake, na biashara kwake imekuwa nzuri sana kwani hata ana maendeleo, na ana usafiri wake wa kumtoa nyumbani kumpeleka ofcn kwake lakini pia kuzungukia wateja wake. Nilijuana na mama Karisa kwenye kikoba, kikoba cha wanawake wa mtaaani, hivyo akawa rafiki na mtu wa karibu, Lakini ni kwa vile pia ni mwanamke mwenye kujitoa sana kwenye mambo ya wenzake, kama mtu akifiwa yani wana kikundi wote 20 wanaweza wasiweze kufika na kuwakilisha lakini mama Karisa atafika, na atatumia gari yake hata kubeba majirani, Ni mwanamke niliyempenda sana, Lakini anajipenda sana na anaonekana wakati wote ana furaha. Haijalishi tunajua mume wake amezaa na mwanamke, lakini hata siku moja sio mwanamke wa kushika tama na kusiskitika, ila atacheka, na kujinywea bia zake na kucheka na wanawake wengine, Nikawa najiuliza sana amewezaje hili?
Na ndipo sasa nilipokaa karibu naye akaniambia kuwa ana Mwanaume wake ambaye anampa tia raha za maisha.Na kwake swala la kulizwa na ndoa alishalisahau.
Mh,, nilikuwa tu ofcn najiwazia mambo mengiii,
Na ndipo nikasikia simu yangu ikiita, niliichukua nan i Fadhili alikuwa akipiga.
Hi Diaa, pole, nimeona missed calls zako, pole sana. Hujambo?
Ni Fadhili huyu, Nilitoka nje mbali kidogo kupokea simu hiyo.
Ndio sijambo, yani wee jamani umeniacha roho yangu juu juu, Hujambo lakini?
Sijambo mamsup, nimechoka bado sijatoka huku, Nimepumzika tu, na kazini sitaenda kabisa, Jana umenichosha sana wewe mwanamke huna huruma?
Aliniambia Fadhili akimaanisha penzi langu la jana limemchosha..
Nilijichekea na kumwambia yani wewe jamani,,, hembu amka bwana.
Aliniambia ataamka, lakini pia akaniambia atasafiri jumatano, ataenda kufuata mizigo yake ya lodge China. Akaniambia ni safari ya ghafla hakuwa ameipanga ila atasafiri jumatano.
Nilimuuitikia na kumtakia safari njema.
Mbona unanitakia safari njema kienyeji jamani? Aliniambia.
Nilimwambia ulitakaje ? Akaniambia Noo usiseme hivyo don’t be hursh… yani maneno hayo ndo unamwambia mpenzi wako,, NILITAKAJE? Hujui unatakiwa umfanyieje mpenzi wako akisafiri? Lakini sio makosa yako,, huyo Hitla ndiye kakuharibu mamii.
Enhe,,, niambie mambo mengine?
Nilijiskia aibu sana alivyonikosaoa,, nikamwambia Am sorry, nisamehe mpenzi.
Akasema dah… wewe mwanamke ndio maana nakupenda na utanifanya hata niache mke jamani.. Sijawahi kuombwa msamaha, dah…. Asante sana, nimekusamehe na nyongeza na nikienda China nilipanga kukununulia zawadi lakin naongeza na zawadi ingine .
Asante nilijibu. Nikiwa naongea na Simu, Thea mwalimu mwenzangu tunayefundisha naye alikuwa akiniangalia sana nisijue ananiangalia. Kisha nilipomaliza kuongea na simu huyo nikawa natembea kuelekea body room kwa ajili ya chai ya saa nne.
Thea alinitazama na akaniambia, Madam, ile simu nani alikuwa anapiga maana si kwa mapozi yale, ulikuwa unazunguka kama unatongozwa,, nilicheka nay eye akacheka.
Nikashindwa kuvumilia, nikamwambia, nilikuwa naongea na Mwanaume anayejeua thamani ya mwanamke. Kisha nikachukua donati yangu na kikombe cha chai nikasogea pembeni kunywa.
Thea alionekana kutaka kujua zaidi, akanisogelea na kuniambia wacha weee,, huyo mwanaume mbona mwanaume maana mama ulikuwa unajizungusha hasa.
Ndio mamii… yani sijui hata nikuambieje,, lakini ninapendeka san asana .
Ni nani huyo? Thea aliuliza.
Nilitabasamu na kumwambia, wewe, sijaribu kukuambia maana mjini hapa mama.
Tulicheka na kukatiza story baada ya Sir Peter kuingia.
Ratiba za kazi ziliendelea.
Kisha nikamaliza ratiba ya siku na nikarudi nyumbani mapema sana kwani kuna kazi ya muhimu sana ya wanafunzi nilikuwa nayo ya kuandaa na muda shuleni haukuwa rafiki sana.
Nilifika nyumbani na kuanza kufanya kazi hiyo ambayo ilinichukua mudamrefu kuimaliza ndani ya masaa matatu nilikuwa nikiifanya.
Baada ya kumaliza dada akaniambia mama baba alisema hatarudi, aliniaga akasema hatarudi.
Msichana wangu wa kazi aliniambia.
Mh… niliguna, nikasema wacha aende kabisa, na mimi nipate muda wa kumuaga Fadhili. Japo moyoni nilisema hivyo, lakini nikamuuliza aliondoka na begi?
Ndio aliondoka na begi na viatu kwenye mfuko wa pembeni. Akaniachia hizi pesa hapa akasema anko Adrian akija nimpatie. Msichana wa kazi aliniambia.
Pesa ziko wapi? Msichana wa kazi aliniletea kiasi cha shilingi milioni tatu kazishika mkononi tena bila hata kuwekwa kwenye bahasha. Nilishtuka sana,
Mungu wangu! Huyu mwanaume ana akili kweli? Anawezaja kumpatia msichana wa kazi pesa nyingi hivi? Yesu wangu.
Lakini ni za nini? Mh, niliendelea kutafakari, Nilizichukua mikononi mwa dada kwa ajili ya usalama zaidi. Uwii niliogopa sana.
Kwa nini asinipe niweke? Kwa nini asimuite huyo Adrian akampatia mwenyewe? Niliwaza mambo mengi sana nisipate jibu zaidi ya kwamba hatuna mawasiliano maxzuri ndio sababu akaamua kumpatia Msichana wa kazi.
Mama na mimi baba kanipa zangu hizi hapa akaniambia ninunue kitu chochote.
Msichana wa kazi alinionyesha elfu 70 kapewa na baba, na mshahara wake ni elfu 50. Na hixzo ni za zawadi , Mh..
Hakukuambia kitu chochote? Hapana hajaniambia kitu mama alinipa tu akaniambia atanipigia simu nisiwe nazima na akiniuliza kitu nimwambie ukweli.
Ahaa… akili yangu ikaniambia kaweka mlinzi huyu na anataka kumtumia dada ili ajue ninarudi saa ngapi nyumbani, Sasa wacha nijiongeze.
Nilishukuru walau dada kaniambia.
Na sikutaka mr ajue nimeongea na dada, nikamwambia dada Anko akipiga simu kutaka pesa basi utanijulisha mwanangu sawa eee. Si vizuri kukaa na pesa nyingi hivi.
Sawa mama binti aliniambia.

****************************
Nilikula na kujilaza , sikuwa na muda wala wa kutaka kuzungumza na Baba Davis, kwanza hana hata aibu, anawezaje kuondoka nyumbani kwake asiniage mimi mke wake? Nilichukia sana, alafu hata chakula asiache pesa jamani?
Mwanaume huyu ni mwanaume gani lakini? Si bure anaitwa Hitla. Niliwaza nikachukia sana,
Lakini akili yangu ikakumbuka maneno ya Fadhili …
Wewe ni mwanamke wa aina yake, ninapaswa nikuonyeshe mapenzi ya dhati, mpaka ujue thamani ya mwanamke duniani. Nakupenda mamii” Maneno hayo yalikuwa yakijirudia rudia akilini mwangu.
Nilichukua simu yangu na kumuandikia Fadhili ujumbe, Nakupenda mpenzi.
Nilijikuta tu naandika hivyo.
Na baada ya kama Dakika chache sana kama sio tatu nikapata majibu,Nakupenda pia mpenzi.
Nilifurahi sana, Nikasema sitadelete huu ujumbe maana nikisoma nasikia faraja rohoni, Nilichofanya nikaweka pw kwenye simu, kwenye msg password kali kabisa, kali sana yenye namba na maneno kabisa.
Kisha nikampigia mama Karisa kutaka kumueleza juu ya Mr kuondoka bila kuaga.
… haloo mama Kei, mambo mamiii?
… poa, hujambo? Simu usiku huu kwema?
Aliuliza,,, wema utoke wapi mama? Baba Davis kaondoka kasafiri sijui kasafiria wapi, na hajaniaga, amemuaga tu dada, hivi huyu mwanaume lakini ana nini ?
Ha ha ha… Mama Kei alicheka kwenye simu.
Na kuniambia hivi wewe unakunywaga savanna ama unakunywaga nini?
Kwenye friji huna savanna nikutumishie? Maana naona una kiu ya pombe,
Hembu ngoja nikuletee hapo mara moja, unataka ya baridi ama ya moto?
Mama Kei aliniambia, (ambaye ndiye mama Karisa huwa nafupisha namuita mama Kei)
Sijui alikuwa wapi, lakini baada ya muda kama nusu saa nilisikia honi zikilia, na nilitoka kufungua,
Nilimfungulia na akaingia,,, Shoga yangu hili geti lako mbona bado la kufungua kishamba hivi. Watu tunatumia mageti yak u slaidi mama.. Geti mtelezo… akacheka kisha akaingia na gari yake na kuipaki…. Gari mpya ambayo sijaiona kabisa.
Akashuka akiwa kavalia tu night dress nyepesi sana ambayo hata maungo utayaona, na akashuka ameshikilia savanaa 4 amezikumbatia. Huku akionekana kama aliyekuwa kalala kabisa ila kaamshwa kwa jambo la muhimu.
Mh.. nilimwambia umetoka wapi kwani? Akacheka na kuniambia nimetoka nyumbani kwani vipi?
Nikamwambia umemachaje baba Karisa? Akacheka akaniambia wewe naye… kalaga baho, yani hembu kwanza kunywa savanna akili ikukae sawa alafu tuongeee.
Maana nimesha kuonya juu ya kunililia na huyo baba Davis wako lakini husikii, yani wewe jamani lini utakomaa na ujiachi? Mwanaume anaondoka hakuagi bado tu unajikondea, wewe ukienda kwa Fadhili unamuaga? Jumapili ulivyoenda kushinda kwa Fadhili ulimuaga? Akaachia cheko la nguvu la kilevi,, ha ha ha,, haloo ya Consooo, nicheke miye Mtoto wa watu.. Conso miye….
Aliniambia hayo maneno na kusimama na khanga aliyofunga ikadondoka na akairusha huko wala asijali, kisha akapita moja kwa moja mpaka jikoni na kuchukua glass na kuketi Dinning na kuanza kufungua zile pombe zote nne, akaniambia ngoja nikuambie, hembu kwanza kunywa.
Kweli nilikuwa na kiu, ni saa nne usiku, tukaanza kunywa,
Akaniambia sikia, nilikuwa na Diaa leo, akisema Diaa anamaanisha mwanaume wake Yule anayechepuka naye. Yani nilikuwa nakutafuta sana maana Diaa kaniambia Fadhili anasafiri jumatano na nimemuomba aniletee vitu vyangu vya dukani, sasa sikia, Ndio mguu huu wako, nimekuja kukuuliza hivi huwa Fadhili anakupa pesa ama umekaa tu kama nunda?
Mh,, nikamwambia ndio ananipa pesa,..
Enhe, mpaka sasa hiviumepewa shilingi ngapi? Mh.. nikamwambia huwa ananipa elfu 70 ama 80 .
Ha ha ha ha… wewe Mama Davis una akili? Unapewa hela gani hizo jamani? Yule mwanaume sikia nikuambie ana pesa chafuuuu, alafu mshamba sana wa mapenzi hajui kitu kabisa, yani mshamba hasa, sikia nichukulie pesa hapo. Yani sasa ngoja nikuambie leo, alikuwa anakutaka siku nyingi sana, lakini nilikuwa najiuliza nitakuingiaje, ana pesa chafu mjini, naomba tu chukua pesa pale,
Na ninataka umuonyeshe mapenzi hasa, ona mimi Dia wangu wala hana pesa kivile lakini ona nimeshabadilisha gari, juzi kanipa milioni 4 nikaongezea na zangu nikanunua gari na ananisaidia kurejesha mkopo niliochukua bank, sikia , Fadhili ana pesa chukua pesa. Mh, niliguna, nachukuaje? Kwanza ndio mapenzi tumeanza juzi tu nachukuajee?
Aliniambia sikia, Fadhili ana kimwanafunzi cha chuo, najua hakijui mapenzi, sasa zubaa hapo uchekwe, Wewe sio mwanachuo bwana useme unataka mapenzi ya lunch boxes na simu, hembu haraka toa wazo la biashara, sijui kama unanielewa, yani kwanza hembu nipe simu yako.
Mama Kei alinipokonya simu, wakati huo moyo ukiwa unadunda kwa mbali,,,
Fadhili ana kisichana cha chuo? Mungu wangu, serious? Moyo wangu ukaniuma sana nikiwa nawaza hayo tayari alichukua simu yangu na akawa anaandika msg, nisiweze kumpokonya, aliniambia tu subiri,, nitakuonyesha nikishamaliza kuandika… Mama Karisa aliniambia, Kisha akaniuliza, Fadhili kakuaga kwamba anasafiri kwenda China?
Ndio nilijibu,, akasema safi,, mwanaume mzuri huyu.
Sikia, nataka kumuomba kitu, maana najua wewe ni mzubavu, mjini hapa bwana, tumekutana kimjini mjini tuishi kimjini mjini…. Ha ha ha. Akacheka tena.
Akiwa anacheka nikamuuliza, Mama Karisa umesema Fadhili ana msichana wa chuuo?
Ndio anaye kwani vipi? Huwezi amini machozi yakanitoka, nikajikuta nalia kabisa…
Wewe? Mama Karisa aliweka simu chini na kunitazama nikiwa nalia na wakati huo nakimbilia chumbani…
Wewe mama Davis, unalia nini?
Nilikuwa nalia na kumwambia, kweli Fadhili ana mwanamke?
Mama Karisa alinitazama na kuniambia, Mama yangu! Mama Davis unalia kweli ama ni macho yangu? Unalizwa na Fadhili? Kwisha habari yako,Serious unalia? Uwiii.
Wewe huna sababu ya kulia, sasa ulifikiri ni wewe peke yake tu yuko na wewe?
Yani aache mke wake ndani akufuate wewe ambaye mara leo uko na mume, kesho sijui uko wapi, wewe jamani, Mama Davis unamaanisha kulia maa?
Sikia, mume wa mtu haliliwi jamani wewe mwanamke, Makubwa Consolatha..
Mama Karisa aliendelea kuongea akinishanga nalia nini.
Wazo likanijia, nikamuuambia huyo msichana anamjua?
Ndio ni kisichana Fulani hivi kitoto toto tu, ambacho nina uhakika hakijamdatisha jamaa ndio maana jamaa kachachawa na wewe na anakusifia sana una heshima, una nidhamu, sasa unalia nini wewe mwanamke?
Mume wa mtu Yule mama, Mume wa mtu haliliwi, anatakiwa wee ndiye akulilie,
Ama hujui mapenzi? Maana nilichukia sana juzi ulikuwa naye alafu nakuja kusikia alikuwa na hicho kisichana tena, hembu kwanza hembu tuongeee,,,
Mama Karisa alionekana ana mambo mengii ya kutaka kuniambia.
Unajua na wewe sijui ni wa kufundishwa mapenzi, maana naona umezubaaa sana.
Kwani kabla ya Fadhili ulikuwa unatoka na nani? Usikute kuna mtu ulikuwa unatoka naye kakufunga…. Na yeye anakulilia.. ha ha ha,, haloooo… Mama Karisa alisema.
Nikamjibu, huku nalia,, Mama Karisa, sijawahi kuwa na mwanaume zaidi ya Bada Davis, sijawahi… Mungu wangu! Mama Karisa alishika mikono kichwani akaniambia serious? Basi kweli wewe mgeni wa mapenzi,
Sasa sikia shoga yangu, futa machozi iko hivi,
Mume wa mtu haliliwi, ila anatakiwa akulilie wewe, yani haiwezekani mumeo akulize na mume wa mtu akulize, lazima ujiongeze, kama mapenzi huwezi ziko njia nyingi sana za kufanya . Ama! Alisema hivyo na akawa kama kasita Fulani.
Kisha akaniambia hembu ngoja nije, akatoka haraka akitembea huyoo na kuchukua simu yake, na kuiwasha maana alikuwa kaizima, ni saa sita usiku, karibu inaenda saa saba , yuko kwangu, mume wake kamuacha na nani sijui, na wala haonyeshi kuogopa hata kidogo, akafungua haraka simu yake sehemu ya kuhifadhi picha na akanifungulia picha, nikaangia na kuona picha ya msichana mdogo tu wa rika ambalo sio zaidi ya miaka 25.
Saa sikia hiki ndicho kifaa cha Fadhili, haka ndiko kasichana kanakomuendesha, kamesababisha Fadhili hana raha na familia yake, ameshagombana na mke wake na mke wake yuko kwao hajarudi mpaka sasa hivi, kama karudi basin i leo asbh. Ila funga mdomo wako nikufundishe maisha.
Mh.. nilishikwa na butwaaa.. Kaachana na mke wake? Nakuambia hivi, shika mdomo wako na akili ikushike. Nimekuwambia Fadhili ana stress za maisha, ni mwanaume mwenye pesa, nakama unavyomuona ni bonge la handsome na ni mchapa kazi sana, ila ndio hivyo. Hajakuambia tu ila ataskuambia, na ndino maana nimeona nikuambie saa hivi usije ukanililia baadae. Ni rafiki wa karibu sana na Diaa, anamheshimu sana Diaa na anamuita kaka. Ndio maana mambo yote ya Fadhili nayafahamu, japo kuna vitu hajaniambia na usije kumuuliza, wewe akili kichwani.
Upo mamiii?
Dah sikuamini, niliumia sana moyo wangu, Niliangalia ile picha ya Yule dada na nikamuchukua jina lake nikafungua instagram nikamuona vyema namna alivyo.

ITAENDELEA SEHEMU YA SITA (post #14)
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
FB_IMG_1559779888947.jpgMama Karisa alikuwa anaongea lakin mimi moyo wangu ukahamia kwa kale kasichana, kasichana ka mwaka wa pili chuoni. Niliumia sana, nifanyeje sasa?
Nimuulize huyu msichana nimwambie koma na mpenzi wangu ama namwambiaje?
Nilisikia maumivu sana moyoni, nililia sana, sana nililia.
Lakini Mama Karisa kaniambia kabisa nisimtaje maana anamheshimu sana Diaa wake na ndiye aliyemuambia juu ya habari za Fadhili, nan i mambo ya siri sana, lakini Diaa akamuamwambia mpenzi wake, akili yangu imejaa, yani Fadhili na mbwembwe zote zile jamani ana mwanamke mwingine?
Lakini Mama Karisa kaniambia nisikubali niyajue mapenzi, niyajueje sasa? Hivi mapenzi yanajulikanaje sasa? Alafu mbona aliniambia yuko home nisipige? Ama ndo alikuwa na huyo dada? Nilijiuliza maswali mengi.
Sasa sina sababu ya kubishana, kesho asbh namdamkia, yani kesho atanitambua.
Niliendelea kulia sana, Mama Karisa aliondoka zake na kuniacha, huku akiwa na gari yake mpya kapewa na Diaa wake pesa anunue kwa makubaliano yay eye kukopa kisha atasaidiwa kulipa pole pole, na kanunua gari ya milioni 18.
Moyo wangu ulijaa huzuni.
Fadhili aliniambia namuagaje, hivi kama angekuwa hanipendi si angetaka kukaa na huyo binti, maana kale ni kabinti maana yake anauwezo wa kumpata wakati wowote, lakini mbona ameniuliza nitamuagaje? Ama alijua kabisa nitakamatika?
Hapana ananipenda, ananipenda sana,
Nilichukua simu yangu, nilikuta kuna msg ambayo haijatumwa ile ambayo mama Karisa alikuwa anaiandika, nikaisoma na kuidelete, haikuwa na mashiko, kwanza aliandika kilevi kilevi.
Nilichukua simu yangu na kumuandikia ujumbe Fadhili, Naomba kuonana na wewe tuongee nina serious talk, Asante,
Kisha nikaituma.
Baada ya kuituma nikakumbuka hivi huyu si mume wa mtu, hivi ninavyomkomandi hivyo na tayari ana masstress yake si ndio nitaachwwa kabisa, kwanza ana kasichana kake, uwii… nilijisikia aibu na nikajiambia, Hujui mapenzi eeee.
Nilichukua simu yangu ambayo wakati huo ilikuwa imeshaingiza msg za majibu kutoka kwa Fadhili, nilifungua na kuisoma, Sawa Dia, chagua tukae wapi tuongeee.Niko free kuna invoice nazishughulikia nitazimaliza usiku huu, kisha niambie tuu.
Naona unaamka na mimi leo.
Alituma hiyo msg nikamwambia can we talk?
Akanijibu o yes mamsup.
Nikamuuliza uko wapi?
Akaniambia niko Bembea Lodge.
Mbona upo huko saa hizi? Wife yuko na nani?
Akaniambia, she is not at home, ….
Mhh.. nilishangaa sana, (Fadhili ana akili sana nisijue ana akili, hakuwahi kuniambia juu ya mke wake kuhusu kuachana, alafu asbh sbh nikamuandikia msg niko nataka kuongea naye serious talk, naona kaamua kujiongeza bila mimi kujua akaanza kunijibu kama alijua nataka kujua nini, huyu mwanaume ni kiboko)
Mh,, baada ya msg hiyo nikajiuliza moyoni huyu kaka anataka kuniambia nini?
Nikamuuliza tena kwa msg,,, yuko wapi?
Akaniambia long story mamii… utajua wakati ukifika.
Uwiii,, nikajikuta natamani sasa kumpigia simu.
Lakini nina angalizo akilini, hivi Consolatha si kaniambia nisisem eee, okay sitasema, nitamlindia heshima shoga yangu.
Ilikuwa ni saa tisa usiku, naona hata muda hauendi.
Alinitext tena akaniammbia nikupigie? Mh… nikamwambia ndio nipigie.
Akapiga na kuanza kuongea.
Nilipata uchungu sana nikaanza kulia, nikamwambia, Fadhili ndoa yangu inanitesa, naomba na wewe usije uje ukanitesa, naomba sana, kama una mwanamke mwingine zaidi ya mke wako naomba kabisa usinitese nafsi yangu.
Fadhili akashangaa nalia, nini akaniambia wewe mwanamke ungejua ninavyokupenda na ungejua jinsi ambavyo moyo wangu unakupenda wala usingelia, bali ungenionyesha tu mapenzi basi, yani Tuliza moyo wako kwangu basi, Moyo wako umefika mahali salama kabisa mamiii. Niamini.
Nilikuwa nashangaa anaongeaje hayo maneno,
Nikajiuliza hivi si anamaanisha kunipenda, kama ingekuwa ni mwanaume Malaya na mke hayupo ina maana huyo mwanafunzi angekuwa naye mida hii. Mbona yuko mwenyewe/
Nilijipa moyo, Kisha akaniambia, najua mumeo hayupo kasafiri, ama uongo?
Mh nikashangaa, ndio kasafiri,,, ama nije hapo kwako kukuchukua sasa hivi ili uamini kama nakupenda? Nilishangaa sana,, amejuaje?
Kweli ananifuatilia..
Umejuaje mr kasafiri?
Nitaachaje kujua ili hali nakupenda? Usalama wa maisha yako uko mikononi mwangu, ndio maana namfuatilia , umejaa akilini kwangu, ama unataka niaambie alipoenda? Nilishangaa sana,,,
Nije kukuchukua sasa hivi mamii?
Alafu unipeleke wapi? Nilimuuliza,,, Twende hata hotelini ukaniambie hiyo serious talk yako maana nina hamu sana kusikia unataka kuniambia nini..
Am coming honey,, nipe lisaa limoja.
Uwii, sikuamini, Nilikata simu, nikaingia bafuni kuoga haraka sana, nikajiandaa ili Fadhili aje kunichukua.
Nilipomaliza kujiandaa nay eye alipiga simu akaniambia nakuja na mguu, sitaki kuja na gari hapo sitaki lionekane hapo, anza kutoka, ama unaogopa?
Wala sikuwa na woga hata kidogo , moyo wangu ulikuwa na masumbufu ya hali ya juu, nilitamani kumuona tu, nilieee weee, anibembeleze na anihakikishie usalama wa maisha yangu na penzi kutoka kwake.
Nilianza kutoka kweli, yani kweli Dhambi ikikuingia inaanza kuota mapembe, Yani natoka kabisa chumbani, huyo sebuleni, na sebuleni kwang kuna picha ya harusi kubwa nimepiga na mr nimeiweka juu ya shelfu, kwanza nikaitoa kuifunikiza pembeni maana nilihisi kama ananiona, na nikairudisha chumbani, kisha huyoo nikafungua mlango, nikafungua geti na kutoka nje,,
Nilisimama nje ya geti kama mwanga, saa kumi kumetulia sanaa, Fadhili alinipigia simu na kuniambia nakuona toka tu. Uko salama.
Nilianza kutembea pole pole nay eye akawa ananifuata. Akanifikia akanikumbatia, nikaanza kulia,, noooo, usilie, noooo. Kisha akampigia mtu simu akamwambia sogeza gari. Kumbe alikuwa na mtu.Ambaye ni dereva wake ni Dogo.
Alisogeza gari na kunifikia. Kisha tukapanda gari akaniambia nimeshindwa kutulia kabisa, yani niambie tu kitu gani unataka kuongea na miimi? Kwa sababu usingizi hatas nisingepata, sijalala usiku kucha kuna kazi nilikuwa nafanya, nikasema nitapumnzika kidogo na wewe ukanitumia ujumbe wako uchovu na usingizi ukakata ghafla. Pole usilie, natamani kujua sana unasemaje mamiii.
Wakati huo kanikumbatia ananibembeleza huku ndevu zake zilizoanza kuota akizisugua sugu shingoni mwangu na hapo ndipo naona eeee,,, mapenzi haya sasa, yani maana sijakumbatiwa na mume karibu mamiaka, kila leo ugomvi tu, hakuna amani kabisa, unaishi na mume ndani lakini unakuwa kama unaishi na chatu looh.
Nami nikajilegeza vyema mikononi na kifuani kwa Fadhili huku najiambia liwalo na liwe, kwani nini bwana, lakini huku akili inaniambia zile story za Mama Karisa ni za ukweli ama ?
Sasa hii serious talk niianzeje? Saa mbili natakiwa ofcn, nina kazi ya kufanya ya muhimu sana, Kesho Fadhili anasafiri nitaongeaje naye? Mr hayupo akirudi nitapata nafasi ya kukaa na Fadhili na kuongea naye?
Mambo mengi muda mchacheNi,, nilijisemea, Waiii, Ngoja nianze na limoja baada ya jingine.
Nikasema wacha nitaomba ruhusa ya kuchelewa kazini, ili niongee na Fadhili. Yani mwanaume huyu anajali sana, Tuliendesha kisha tukafika karibu kabisa na hotel moja ya kitali, nzuri sana, Akapaki gari yake hapo na kuniambia ngoja nakuja. Alishuka na kuingia humo ndani kisha baada ya dakika tano akaniambia njoo muache Dogo aondoke.
Nikashuka kwenye gari nikamfuata alipokuwa, ni Hotel nzuri sana, huwa naiona na kuisoma tu kwenye mitandao, hotel kubwa mnooo. Tuliingia humo na akaniambia hapa napapenda sana, huwa nikiwa nimechoka ndipo mahali napenda kuja kupumzika, Yani maisha yana mambo mengi mamiii , ni mchaka mchaka tu, pesa hazijai, dah.
Ni kweli pole. Asante aliitika.
Alijitupa kwenye kitanda na kusema, nimechoka sana, lakini nisingeweza kutulia kwa sababu uliniambia una serious talk na mimi,, ningewezaje kutulia,, maana ni siku chache tu nimekujua lakini moyo wangu umekuwa na amani sana, nimekuwa na furaha sana, Nikuombe tu usije ukaniacha mamii.. sawa? Usiniache, nakupenda sana wewe mwanamke.
Uwi, akaanza tena maneno yake ya mapenzi ambayo ndiyo huwa yananimaliza najikuta sina ujanja mbele yake.
Aliketi na kutengeneza kahawa, akanigeukia akaniambia, milk coffe ama black? Aliniuliza,
Noo, asante, Akatabasamu, akaniambia Mami, ukipewa kitu na mpenzi wao usikatae, unachukua unaonja alafu unarudisha,,, Kisha akacheka…
Na mimi nikajikuta ninacheka.
Akasema sio kosa lako, najua ulikuwa unaishi Ki Hitla hitla sana, lakini usijali,,, kila kitu kitakaa sawa,, nina kazi ya kukufundisha mapenzi… kisha akacheka tena.Na kuniambia karibu kahawa. Ilibidi nichukue na kuinywa,, kisha na mimi nikamwambia asante sana . Akacheka.
Alikunywa kikombe kimoja akamaliza, akaenda kuswaki na kurudi , huku akiwa anafuta uso wake. Nilikuwa nimekaa kitandani na miguu yangu ilikuwa imekanyaga zulia zuri sana la kitanda cha hiyo lodge. Alikuja na kujichomeka kati kati ya miguu yangu, kama mtu ambaye anasukwa, tena Kilimanjaro nywele za usogoni. Kisha akanitazama akiwa kapiga magoti,, akaniambia Nihakikishie hutaniacha kwa sababu najua unayo serious talk, lakini kabla hujaniambia nihakikishe hutaniacha ili nikujibu ukweli na nisikudanganye kwa lolote.Mh nilishangaaa, kisha nikamtazama usoni, alikuwa anamaanisha sana, Nikamwambia sitakuacha ila naomba uniambie mwana chuo uliyenaye umemuacha?
Aliniambie ndio nimeucha baada ya kukupata wewe.
Mh,,, alinijibu kirahisi sana, Akaniambia Mamii nakufahamu sana, muda mrefu nimekuwa nikimuona bro wangu na Conso , na Conso nimekuwa nikikuona naye sana muda mrefu nikakupenda tu, napenda wanawake wapole kama wewe sana, niamini nakupenda.
Enhe lingine?
Aliniambia hivyo hasira zikaniisha. Nikamwambia lingine mkeo yuko wapi?
Akaniambia, nisikilize, kuna mambo sipendi kuyaongelea, ikiwa ni pamoja na hilo, na nimekuambia sitaki kukudanganya, ila sitaliongelea hili. Hembu tuliache kwanza hili, Nasafiri kesho sitaki kuumiza akili sawa mamii.
Aliniambia hivyo kisha akaonekana mwenye mawazo sana.
Moyoni kuna kitu kinaniambia mhurumie, kingine kinaniambia mwongo huyo.
Nikamwambia nikuombe kitu dia, akaniambia niombe.
Nikamwambia naomba simu yako.
Akatabamu kisha akaniambia, Hapana, hapana. Simu hapana.
(Yani ushamba wa kudanga jamani nataka kujimilikish ha ha ha ha)
Kama unanipenda naomba simu yako, please.
Akaniambia, sikia, mimi ni mwanaume wako, unajua wanaume tuna mambo mengi sana, kazi nyingi, tunadai tunadaiwa, sasa kuna mambo ambayo sio mabaya lakini kwa vile wewe ni mpenzi wangu ukiyaona utaanza kunishauri labda acha ama utaogopa nk. Lakini sina mambo yoyote mabaya kabisa niamini, Nakupenda full stop.
Aliniambia hivyo lakini bado nikawa natamani anipe simu yake ili nione kama kuna msg za mapenzi za wanawake.
Aliniangalia akatabasamu akasema nakuhurumia sana mamii, una wivu eee, sasa mbona bado sijakuonyesha mapenzi, utapata kichaaa,,,, Alicheka na kisha akasimama akaniambia simama, nikasiama, akaniambia nikumbatie alfu niambie kitu kizuriiiiiiii sana.
Nikasimama nikamkumbatia, nikamwambia nakupenda sana, Akaniambia toa sauti, sikusikii, Nikamwambia Nakupenda sana, Naye akaniambia nakupenda pia, sana niamini, alafu nataka kukununulia gari.. sipendi unavyotembea na miguu, mwanamke mzuri kama wewe hupaswi kutembea na miguu, ukiwa mpenzi wa Fadhili lazima ufurahie maisha, jina langu Fadhili nami nataka kukufadhili.. sawa mamiii.Sawa niliiitika, nikajikuta nalia sana. Akanibembeleza na kuniambia unaenda saa ngapi kazini? Wakati huo ni saa kumi na mbili asbh, Nikamwambia saa mbili.
Akaniambia, Niombee nifanikiwe tu, huu ualimu haukufai, unatakiwa uwe nashughuli ambayo inakupa uhuru nikikuhitaji nakupata wakati wowote, Ndio maana lazima ujue na uamini nakupenda, kwa sababu ningekuwa sikupendi wanawake wako wengi, tena wengi sanaa, si unaniona nilivyo lakini? Alisimama akaniaambia nitazeme, si unaona nilivyo mwanaume wa haja eee,, pesa ninayo, afya ninayo na mapenzi ninayo,,, nikitaka mwanamke yeyote simkosi ila najua kuchagua wanawake wazuri ndio maana nikaacha wooote nikakufuata wewe, Wewe ni mzuri sana kwangu, Naomba usiniache.
Nilikuwa nashangaa huyu mwanaume anatoa wapi maneno mazuri hivi jamani, yani mpaka nikawa natamani, mume wangu afe na mke wake afe tubaki wenyewe tuoane.
Mapenzi ndio haya. Dah.
Aliniambia mimi nitakuwa hapa hotelini mpaka jioni, please ukipata muda uje uniage maana kesho naenda airport asbh sanaa saa kumi asbh.
Sawa nilimjibu, kisha tukaendelea kupiga story na ilipofika saa moja nikaita taksi nikaondoka. Pale hotelini nilikutana na watu kama wanne ninaowafahamu ambao ni wafanyakazi wa hpo, lakini nilivyojikausha watajijua wenyewe.
Siku yangu imekuwa nzuri sana, nimehakikishiwa kupendwa na Fadhili, intake nini tena, Nimehakikishiwa kununuliwa gari, intake ninitena? Uwiii kupendwa ndiko huku.
Niliona siwezi kukaa na umbea huu mwenyewe, nilimuita ticha Thea ili nimsimulie,
Alionekana naye kutaka kusikia ninachotaka kumwambia, nilikuwa nina rah asana, yani najisikia kama DUNIA YOTE YANGU. Kununuliwa gari mchezo nini?
Sio wote wenye magari, yani ghafla tuu unaambiwa nakunuanulia gari, uwii.Mama Karisa mwenyewe ni kubuhu lakini gari kapewa la mkopo,, mimi Napata gari kirahisiiii.
Nasubiri gari, nasubiri gari.

ITAENDELEA SEHEMU YA SABA (post #25)
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,646
2,000
Moderator, Paw... Tunaomba hizo chapters ziunganishwe ili kuwepo na mtiririko mzuri.
Mimi sioni haja hiyo na sikubaliani na unatalotaka.

Mtu akisoma ataona mwishoni post inaendelea namba ngapi.

Mtu akitoka kwenye uzi na kurudi tena huwa anapelekwa pale post mpya zimeanzia.. iweje mtu haangaike kurudi kwenye post namba moja kuhangaika kusaka wapi aendelee na stori ni ndefu sanaaaaaa.

Miaka yote hii humu kumbe hujui mengi yamebadilika. Tulia burudika kwa muda wako

Moderator Paw naomba muache uzi ulivyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom