Naiona vita ya Zitto Kabwe na Kafulila, Kafulila akitengenezwa kuwa mbadala wa Zitto

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,872
2,000
Hii ni vita nyingine ya nani awe juu ya mwingine kwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Uzalendo kwa Taifa. Mambo yanaonekana kumwendea vizuri KAFULILA siyo tu anapambana mwenyewe bali kwa sababu anapambana akiwa ndani ya UKAWA na hivyo kupata msaada kutoka kwenye makundi yanaunga mkono UKAWA na hasa CHADEMA.

jana kuna mada iliwekwa humu ikiwa na kichwa cha habari TAMKO LA "IPTL BRING BACK OUR MONEY"(IBBOM) , Pamoja na ,mambo mengine tamko hili lilipongeza taasisi zifuatazo kwa kutambua mchango wa DAVID KAFULILA katika kusimamia ipasavyo hoja ya TEGETA ESCROW.

1.Kituo cha kutetea haki za Binadamu

2. Kituo cha sheria na haki za Binadamu

3. Wananchi wa Kahama kwa kumsimika kuwa Chifu wa Wasukuma

4. Wananchi wa kigoma Kusini kwa kumpata Mbunge Mwelewa na kuwaomba wamchague tena ambapo jumla ya shilingi mil.5 zilichangwa ili kumchukulia fomu.

Hapana shaka kwamba pongezi hizi ni mahsusi siyo tu kumjenga KAFULILA kuwa mbadala wa ZITTO KABWE lakini pia kumpoteza kabisa Kabisa Zitto kisiasa na zaidi kumfanya KAFULILA asahau kabisa makubaliano yake ni ZITTO ya kuhamia ACT kama ambavyo Zitto mwenyewe amekuwa akiuaminisha Umma kuwa KAFULILA atahamia huko.

Siasa ni mchezo(game), juzi nilimsikia Katibu Mkuu wa CHADEMA akisema hawatarudia makosa ya 2010, walimtegemea SAMWEL SITTA kuhamia CHADEMA na kugombea urais kupitia chama hicho lakini akawaacha kwenye mataa dakika za mwisho. Tayari KAFULILA alishakanusa kuwa hana mpango wa kuhamia ACT, hii ni changamoto kwa ZITTO na ACT kwa ujumla, Zitto alishasema wabunge wengi kutoka Upinzani na chama Tawala watahamia ACT.

Kwa jinsi Kafulila anavyojengwa na mitandao inayounga mkono hapana shaka CHADEMA na siyo UKAWA, sijui kama Zitto bado ana ndoto hiyo. Na kama ndoto hiyo imeanza kupotea, je Zitto anafikiri umaarufu wake bado utaendelea kuwa juu?

Tusuviri tuone, vita ni vita, na katika hili naweza kuwapongeza CHADEMA kuwa wanakaribia kushinda. Tahadhari; CHADEMA wataendelea kushinda vita hii kama tu UKAWA utaendelea kuwepo, kwani bila UKAWA hakuna Kafulila wa kumfunika Zitto.

Lakini Zitto Kashtuka kuwa anafunikwa na KAFULILA kupitia kwa mahasimu wake wakuu wa CHADEMA, sasa atafanyaje?

Hawezi tena kuwashambulia CHADEMA ila namna pekee ni kujisafisha kuwa hatumiwi na CCM, na hili liko wazi kuwa hatumiwi na CCM ilkuwa ni hofu tu ya CHADEMA labla hawajapata njia mbadala ya kummaliza, lakini je atawaaminishaje watanzania kuwa hatumiwi na CCM?

Mashambulizi ni lazima ayaelekeze kwa wana CCM waliotangaza nia na hasa wale ambao ni dhahiri wakipitishwa kupeperusha bendera ya CCM hapo mwezi Oktoba, CCM hatakuwa na kazi kubwa ya kuwanadi. Zitto anaona kuwa kitendo cha yeye(na siyo UKAWA) kuwa na ubavu wa kusema chochote kitakachowadhoofisha watangaza nia hawa wa CCM atakuwa amevuta hisia za watanzania kuwa ndiye mwenye siasa pekee wa upinzani mwenye uthubutu.

Je kwa mbinu zinazotumiwa na pande zote mbili nani ataweza kushinda?
 
chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
354
1,000
KAFULILA achangiwa milioni 5 na wanaharakati walioshirikiana naye katika harakati za sakata la Escrow hawa si wengine ni wanakundi la IPTL- BRING BACK OUR MONEY(IBBOM)
ili achukue fomu kwa ajili ya kuwania
nafasi ya Ubunge tena jimboni kwake
#MTANZANIA #JU
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,992
2,000
TataMadiba

Bado unaamini siku hizi tunaishi kwenye ulimwengu wa propaganda za kizee za ccm? Kama ni karata umelamba galasa kajipange ama wafuate wanakijiji wanaokuja kwenye mikutano ya ccm bila kunywa chai wakisubiri muwape shilingi 5000 huku wakishangaa maVX v8 mnayowakoga nayo huku ukiwapa hiyo hekaya yako hapo juu.
 
Last edited by a moderator:

MTRANSPARENT

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
740
0
Zitto n maaruf by nature na wanaoota kuwa ZZK atakuja apotee waamke kumeshakucha waachane na ndoto izo..... wakat lisu anatangaza kumfukuza ZZK alitokwa na mapovu mengi akijua kammalizza ZZK lkn je kwa sasa nan zaid kat ya lisu na ZZK? Aliambiwa yy n kifaranga kwenye game hakuelewa lkn nadhan sasa ashaanza elewa...
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367

Huwezi mlinganisha Lissu na huyo Yuda
 
STDVII

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,588
2,000
Kuna upande wa Tatu ambao ni CCM wao ndiyo wanapanga na kugawa Majimbo, Jimbo la Kafulila tayari limegawanywa inaonyesha Kafulila angependa kugombea upande wa Ziwa Tanganyika ambako kuna Wahamiaji wengi na kumekua na mgogoro kati yake na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza juu ya Wahamiaji toka DRC kabila la Wabembe, hawa wamekuwepo miaka mingi sana katika maeneo haya, walikimbia Vita na Utawala mbaya wa Mobutu Seseseko wengine walihamia kwa shughuli za Uvuvi na maisha magumu kwao kwa sababu hakuna miundo mbinu yoyote iliyojengwa na Serikali yao ya Afya na Elimu. Kwa hiyo Mpinzani siyo

Zitto tu bali pia CCM ndiye adui yake namba moja hasa kwa hoja zake zinazoambatana na maneno ya moja kwa moja yasiopoozwa, jambo la kujiuliza amejipangaje katika hili Je wapiga Kura wake wamejiandikisha? ilimkulinda nafasi yake kama ni kinyume chake amekwenda na maji.
 
TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Hii ni moja kati ya post makini nilizokutana nazo,kwa mara ya kwanza mwandishi wa hii mada amekiri uwezo wa kiwango cha juu wa kimikakati walio nao wapinzani katika kuzichanga karata zao za kisiasa, Zitto ni mnafiki hakuna asiyemjua,acha apotezwe tu kwenye ulimwengu wa kisiasa maana taifa hili halitaendelea likiendelea kuwa na wasiasa wenye sura mbili kama Zitto.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,494
2,000
Zitto n maaruf by nature na wanaoota kuwa ZZK atakuja apotee waamke kumeshakucha waachane na ndoto izo..... wakat lisu anatangaza kumfukuza ZZK alitokwa na mapovu mengi akijua kammalizza ZZK lkn je kwa sasa nan zaid kat ya lisu na ZZK? Aliambiwa yy n kifaranga kwenye game hakuelewa lkn nadhan sasa ashaanza elewa...

Hivi kwa akili yako ndogo unataka kumlinganisha zzk na lisu?zzk ni sawa na mjusi tu kwa lisu na hakuna hasiye lijua hilo.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,494
2,000
Zitto n maaruf by nature na wanaoota kuwa ZZK atakuja apotee waamke kumeshakucha waachane na ndoto izo..... wakat lisu anatangaza kumfukuza ZZK alitokwa na mapovu mengi akijua kammalizza ZZK lkn je kwa sasa nan zaid kat ya lisu na ZZK? Aliambiwa yy n kifaranga kwenye game hakuelewa lkn nadhan sasa ashaanza elewa...

Umaarufu wa zzk ulikuwa mwandiga tena kupitia cdm,sasa amebakia kutegemea nguvu za kalimanzira tu
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,494
2,000
Hii ni moja kati ya post makini nilizokutana nazo,kwa mara ya kwanza mwandishi wa hii mada amekiri uwezo wa kiwango cha juu wa kimikakati walio nao wapinzani katika kuzichanga karata zao za kisiasa, Zitto ni mnafiki hakuna asiyemjua,acha apotezwe tu kwenye ulimwengu wa kisiasa maana taifa hili halitaendelea likiendelea kuwa na wasiasa wenye sura mbili kama Zitto.

Anakuwa sawa na popo
 
hexacyanoferrate

JF-Expert Member
May 15, 2014
1,230
2,000
TataMadiba

Uzi wako huu siyo wakumuelezea Zitto,ila uliitaka zaidi chadema,maana kila unapotoa mada ni chadema,hata kama haiihusu lazima tu utaitaja,kwa taarifa yako chadema ipo kabla ya ukawa au zito na itaendelea kuwepo na kushika dola!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom