TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Hii ni vita nyingine ya nani awe juu ya mwingine kwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Uzalendo kwa Taifa. Mambo yanaonekana kumwendea vizuri KAFULILA siyo tu anapambana mwenyewe bali kwa sababu anapambana akiwa ndani ya UKAWA na hivyo kupata msaada kutoka kwenye makundi yanaunga mkono UKAWA na hasa CHADEMA.
jana kuna mada iliwekwa humu ikiwa na kichwa cha habari TAMKO LA "IPTL BRING BACK OUR MONEY"(IBBOM) , Pamoja na ,mambo mengine tamko hili lilipongeza taasisi zifuatazo kwa kutambua mchango wa DAVID KAFULILA katika kusimamia ipasavyo hoja ya TEGETA ESCROW.
1.Kituo cha kutetea haki za Binadamu
2. Kituo cha sheria na haki za Binadamu
3. Wananchi wa Kahama kwa kumsimika kuwa Chifu wa Wasukuma
4. Wananchi wa kigoma Kusini kwa kumpata Mbunge Mwelewa na kuwaomba wamchague tena ambapo jumla ya shilingi mil.5 zilichangwa ili kumchukulia fomu.
Hapana shaka kwamba pongezi hizi ni mahsusi siyo tu kumjenga KAFULILA kuwa mbadala wa ZITTO KABWE lakini pia kumpoteza kabisa Kabisa Zitto kisiasa na zaidi kumfanya KAFULILA asahau kabisa makubaliano yake ni ZITTO ya kuhamia ACT kama ambavyo Zitto mwenyewe amekuwa akiuaminisha Umma kuwa KAFULILA atahamia huko.
Siasa ni mchezo(game), juzi nilimsikia Katibu Mkuu wa CHADEMA akisema hawatarudia makosa ya 2010, walimtegemea SAMWEL SITTA kuhamia CHADEMA na kugombea urais kupitia chama hicho lakini akawaacha kwenye mataa dakika za mwisho. Tayari KAFULILA alishakanusa kuwa hana mpango wa kuhamia ACT, hii ni changamoto kwa ZITTO na ACT kwa ujumla, Zitto alishasema wabunge wengi kutoka Upinzani na chama Tawala watahamia ACT.
Kwa jinsi Kafulila anavyojengwa na mitandao inayounga mkono hapana shaka CHADEMA na siyo UKAWA, sijui kama Zitto bado ana ndoto hiyo. Na kama ndoto hiyo imeanza kupotea, je Zitto anafikiri umaarufu wake bado utaendelea kuwa juu?
Tusuviri tuone, vita ni vita, na katika hili naweza kuwapongeza CHADEMA kuwa wanakaribia kushinda. Tahadhari; CHADEMA wataendelea kushinda vita hii kama tu UKAWA utaendelea kuwepo, kwani bila UKAWA hakuna Kafulila wa kumfunika Zitto.
Lakini Zitto Kashtuka kuwa anafunikwa na KAFULILA kupitia kwa mahasimu wake wakuu wa CHADEMA, sasa atafanyaje?
Hawezi tena kuwashambulia CHADEMA ila namna pekee ni kujisafisha kuwa hatumiwi na CCM, na hili liko wazi kuwa hatumiwi na CCM ilkuwa ni hofu tu ya CHADEMA labla hawajapata njia mbadala ya kummaliza, lakini je atawaaminishaje watanzania kuwa hatumiwi na CCM?
Mashambulizi ni lazima ayaelekeze kwa wana CCM waliotangaza nia na hasa wale ambao ni dhahiri wakipitishwa kupeperusha bendera ya CCM hapo mwezi Oktoba, CCM hatakuwa na kazi kubwa ya kuwanadi. Zitto anaona kuwa kitendo cha yeye(na siyo UKAWA) kuwa na ubavu wa kusema chochote kitakachowadhoofisha watangaza nia hawa wa CCM atakuwa amevuta hisia za watanzania kuwa ndiye mwenye siasa pekee wa upinzani mwenye uthubutu.
Je kwa mbinu zinazotumiwa na pande zote mbili nani ataweza kushinda?