Naiona nia njema ya rais Samia

Naiona nia njema ya rais Samia

Storywriter

Senior Member
Joined
Jan 8, 2023
Posts
175
Reaction score
390
Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita nchi yetu haikuwa na sura nzuri katika swala la demokrasia, haki za watu na mahusiaono ya nje.

Ki-ukweli kabisa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, rais Samia anaonesha mwelekeo mzuri katika kuleta mageuzi makubwa katika nchi hii.

Jambo alilolifanya juzi halikuwa dogo. Yeye ameamua kuiheshimu katiba. Hatua hii itachochea maendeleo ya haraka sana katika taifa. Jambo moja tu limebaki, kama atarekebisha ufumo wa utoaji haki katika nchi hii , basi nchi itapata maendeleo ya haraka. Watu wenye mitaji yao duniani wataanza kuileta hapa kwetu. Naiona Tanzania yenye maendeleo ya kweli siku chache zijazo.

Tumtie moyo rais Samia ana nia njema.
 
WEWE kweli storywriter.ni hadithi,hakuna rangi ya kijani mwenye Nia njema,,na wakifanya "mazuri" ujue ndani yake inawahakikishia kitu Fulani mifukoni mwao
 
WEWE kweli storywriter.ni hadithi,hakuna rangi ya kijani mwenye Nia njema,,na wakifanya "mazuri" ujue ndani yake inawahakikishia kitu Fulani mifukoni mwao
Hapana watu wema bado wapo duniani. Huyu mama anaweza kuwa miongoni mwao.
 
Back
Top Bottom