Naiona maana halisi ya 'Upinzani' sasa

Naiona maana halisi ya 'Upinzani' sasa

Huwa nakaa nawaza laiti kama hapa Tanzania kusingekuwapo na vyama vingi hali ingekuwaje? Vyama vya upinzani vimesaidia sana hata wananchi wengi wakajua haki zao.Ni vyema tukaendelea kuwatia moyo ili wapate nguvu ya kutupambania.
 
nyie ndio mnaoufanya upinzani udharaulike, mapovu yote yale kwa ajili ya tbc kutoonesha bunge live, ningewapa pointi nyingi kama wangetoka bungeni kushinikiza xray kwenye hosp zote za mikoa..
Kwa kuwa hufahamu maana basi hupaswi kuelezwa maana
 
Kwa haya anayoyafanya huyu abunuas kuanzia sasa natafuta chama cha kuhamia ila siyo chadema.
 
Wanabodi habari za muda huu. Ni muda mrefu tumekuwa tukiona wapinzani wakibezwa na kupuuzwa pale wanapoamua kusimama kidete kupigania maslahi ya nchi. Ilifika hatua hata baadhi ya wanasiasa kuonekana ni maadui kisa tu kuisimamia na kuipinga serikali inapokosea.

Maana ya upinzani sasa hatimaye imeanza kuonekana. Hii inakuja baada ya kuona wabunge wa upinzani kutoka vyama tofauti vya ACT na wale wa umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiungana kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Ni juzi tu tumeona Zitto Kabwe akiungana na UKAWA kupinga suala la TBC kutorusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live). Na leo hii pia tumeshuhudia Zitto Kabwe na Tundu Lissu wakiungana kupinga juu ya bunge kujadili mpango wa maendeleo wa 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao haujakidhi matakwa ya kanuni za bunge.

Hili ndio tunalotaka watanzania. Tunahitaji kuungana kwa ajili ya Tanzania na sio vyama vyetu. Kupitia hili wabunge wa CCM wana la kujifunza (kuwa sio kinacholetwa na serikali ya CCM ni sahihi na hakina kasoro).

Heko wabunge wa upinzani na huo ndio UPINZANI WA KWELI.

MAgnesium
Hutaki tena "hapa kazi tu"
 
Tanzania inaongoza kuwa na mimba za watoto hiyo ni very simple statement implications zake ni kwamba asilimia kubwa ya hawa watoto wanaozaa watakuwa masikini mpaka ukubwani kwa sababu ya kukatishwa masomo mapema na kujipunguzia future life chances.

Alikadhalika hao watoto zao nao kwakuwa watalelewa na wazazi wasio na uwezo ni probability chances kubwa ni kwamba watakosa emphasis za ndani na pengine kuanza kazi za kusaidia wazazi wao at early age kama awatokimbia kuwa watoto wa mitaani (tatizo lingine la vijana wasio na maadili wengi wao kwa kukosa proper socialization processes).

Nyongeza ya hapo elimu yenyewe ya sasa ni mgogoro aitayarishi vijana kuweza kupambana na dunia ya leo ambapo viwango vina minimum standards of awareness not just in understanding but work attitude too ushahidi tabia za wawekezaji kupenda kuajiri wageni dhidi ya watanzania kwa sababu wazijuazo wao despite having to pay higher salaries that is enough of a concern to any serious government kutaka kujua wapi wanakosea kwenye kutayarisha human capital.

Kuna maswala ya ujambazi yaliyokithiri kutokana na umaskini wa jamiii na lack opportunities kwa wahitimu, ukosefu wa maarifa ya vijana to name a few halafu wewe unasifia watu kwa sababu ya bunge kuwa live tu wakati kuna hoja chungumtele za kuibana serikari na zenye tija za siasa; akili zetu zina ambatana na hali yetu ya uchumi huo ndio uhalisia wenyewe maana atajui hata priority zetu ni zipi za kuibana serikari.
 
Wanabodi habari za muda huu. Ni muda mrefu tumekuwa tukiona wapinzani wakibezwa na kupuuzwa pale wanapoamua kusimama kidete kupigania maslahi ya nchi. Ilifika hatua hata baadhi ya wanasiasa kuonekana ni maadui kisa tu kuisimamia na kuipinga serikali inapokosea.

Maana ya upinzani sasa hatimaye imeanza kuonekana. Hii inakuja baada ya kuona wabunge wa upinzani kutoka vyama tofauti vya ACT na wale wa umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiungana kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Ni juzi tu tumeona Zitto Kabwe akiungana na UKAWA kupinga suala la TBC kutorusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live). Na leo hii pia tumeshuhudia Zitto Kabwe na Tundu Lissu wakiungana kupinga juu ya bunge kujadili mpango wa maendeleo wa 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao haujakidhi matakwa ya kanuni za bunge.

Hili ndio tunalotaka watanzania. Tunahitaji kuungana kwa ajili ya Tanzania na sio vyama vyetu. Kupitia hili wabunge wa CCM wana la kujifunza (kuwa sio kinacholetwa na serikali ya CCM ni sahihi na hakina kasoro).

Heko wabunge wa upinzani na huo ndio UPINZANI WA KWELI.

MAgnesium
Kweli hali ni ngumu.
Hadi chadema wamekubali kukaa na zitto huku wakichekacheka.
Ama kweli zitto kiboko du!
 
Kumshangilia lowasa inabidi upimwe akil
Huwezi kukaa duniani bila kusafiria nyota za watu.kwanza umeandika kwa kuiga mtiririko mwenzio ukaugeuza mpasho kwa mfalme wa siasa za tz kwa sasa edo wa monduli kwa akina sokoine.
 
Mimi nauunga upinzani tangu 1995.Bila upinzan nisingejitambua
 
Huwezi kukaa duniani bila kusafiria nyota za watu.kwanza umeandika kwa kuiga mtiririko mwenzio ukaugeuza mpasho kwa mfalme wa siasa za tz kwa sasa edo wa monduli kwa akina sokoine.
Mfalme yupi huyo au hujui maana ya mfalme
 
Maslahi ni muhimu sana kwenye uundwaji wa vyama...huwezi kuwa mpinga ufisadi halafu uungane na fisadi hutafanikiwa...hilo ni somo la uchaguzi 2015
We kilaza si ulidhani Arusha na Hai itaenda CCM?
 
Kweli hali ni ngumu.
Hadi chadema wamekubali kukaa na zitto huku wakichekacheka.
Ama kweli zitto kiboko du!
zitto kafanya vizuri kujikomba kwa chadema huku akiinamisha kichwa chini uzuri ametambua umoja ni nguvu karudi kwa Mbowe na alimwambia utarudi tu
 
nyie ndio mnaoufanya upinzani udharaulike, mapovu yote yale kwa ajili ya tbc kutoonesha bunge live, ningewapa pointi nyingi kama wangetoka bungeni kushinikiza xray kwenye hosp zote za mikoa..
Hivi watu hamuoni aibu kuonyesha ujinga hadharani? Yaani pamoja na masomo yote yanayotolewa hapa JF kuhusu hilo bado huelewi tuu? Halafu unajiita GT?
 
Back
Top Bottom