Magnesium
JF-Expert Member
- Nov 9, 2014
- 317
- 185
Wanabodi habari za muda huu. Ni muda mrefu tumekuwa tukiona wapinzani wakibezwa na kupuuzwa pale wanapoamua kusimama kidete kupigania maslahi ya nchi. Ilifika hatua hata baadhi ya wanasiasa kuonekana ni maadui kisa tu kuisimamia na kuipinga serikali inapokosea.
Maana ya upinzani sasa hatimaye imeanza kuonekana. Hii inakuja baada ya kuona wabunge wa upinzani kutoka vyama tofauti vya ACT na wale wa umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiungana kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Ni juzi tu tumeona Zitto Kabwe akiungana na UKAWA kupinga suala la TBC kutorusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live). Na leo hii pia tumeshuhudia Zitto Kabwe na Tundu Lissu wakiungana kupinga juu ya bunge kujadili mpango wa maendeleo wa 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao haujakidhi matakwa ya kanuni za bunge.
Hili ndio tunalotaka watanzania. Tunahitaji kuungana kwa ajili ya Tanzania na sio vyama vyetu. Kupitia hili wabunge wa CCM wana la kujifunza (kuwa sio kinacholetwa na serikali ya CCM ni sahihi na hakina kasoro).
Heko wabunge wa upinzani na huo ndio UPINZANI WA KWELI.
MAgnesium