Naiona CHADEMA ikifutika katika ramani ya siasa za TZ

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Iko dhahiri kabisa hivi sasa kwamba chama chetu hiki kilichowika sana miaka miwili mitatu iliyopita, tena wiko la mazuri kwa mabaya kinaenda kufutika katika siasa za Tanzania kama andiko la penseli.

Nasema haya kwa misingi ya ukweli uwazi na uhuru wa mawazo kwamba ubabe udikteta na upyupyu uliokuwa unafanywa na viongozi wa chama hiki ndio umekuwa kaburi lake rasmi. Tulishuhudia Lowassa akipewa zawadi ya kugombea urais kupitia taasisi hiyo nyeti ya mtu binafsi, kama haitoshi wakawapokea na makapi mengine kibao yaliyokosa mvuto kwenye siasa za ushawishi hapa nchini.

Leo hii hatumuoni wala kumsikia tena Dr wa ukweli, Slaa ambaye alifanya siasa za hoja. Leo hii hatumuoni tena Zitto Kabwe kijana machachari kwenye jukwaa na kwenye hoja. Wamepotea wote waliokuwa ndio msingi wa chama chetu, leo kimekuwa kichaka cha kufika mafisadi na majizi. Ee Mungu wee tuliipenda sana CHADEMA lakini wewe umeipenda zaidi.

Yuko wapi mtembea na sumu mfukoni Ben wa saa Nane???
 
Siasa za tanzania upinzani wana NAFASI YA kufanya vizuri Sana japo kushinda kwao ni vigumu Lakini watajitengenezea NAFASI nzuri zaid endapo wataendelea kuwa WAMOJA yaani wakabaki na umoja Wao.. Kwa siasa za Africa zilivyofika nadhani hivi vyama vya ukombozi kama CCM wako Hali mbaya wananchi wameamka watakataa tu hasa kundi kubwa LA vijana wakijitokeza.. Kiufupi CCM wamebaki na ushawishi Kwa watu waliozaliwa nyuma ya miaka ya 1980.. Vijana wengi hasa wasomi ndio chachu ya mabadiliko.. Mtoa Maada nadhani HAUPO SAWA Kwa mtizamo wangu chadema bado wana mvuto Sana tusubiri 2020.. Ila Kwa Hali iliyopo ni ngumu CCM kukubali chadema washinde. Tumeshuhudia chaguzi za meya na ule WA zenji
[HASHTAG]#justice[/HASHTAG] for lema #
[HASHTAG]#free[/HASHTAG] our max #
[HASHTAG]#bring[/HASHTAG] back our ben#
 
Back
Top Bottom